Kitu Ambacho Watu Wengi Wanakisubiria Kwenye Maisha Yao

Kwenye haya maisha utachelewa kufika kule unakotaka kwenda kama ukisuburia kupewa ruhusa ya kufanya kile unachotaka kufanya. Watu wengi wanakaa huku wakisubiria mtu fulani aje awape ruhusa ya kufanya kile wanachotaka kufanya. Dunia haiko hivyo, ukitaka kupata kile unachotaka, usisubiri kupewa ruhusa, jiruhusu mwenyewe kuingia kwenye kile unachotaka kufanya. Watu wengi waliofanya makubwa hawakusubiri ruhusa …

Jinsi Ya Kuwakera Watu

Kwenye hii dunia tunayoishi huwezi kuishi bila kuwakera watu wengine. Hata kama wewe huna lengo wa kuwakera wao wenyewe watajikera kwa yale unayofanya. Kifupi kwa chochote kile utakachofanya lazima kuna watu utawakera. Je, wewe ungechagua kuwakera watu wa namna gani? Kwa mfano, ukifanya kazi kwa bidii lazima utawakera wale wavivu ambao hawataki kufanya kazi. Ukichagua …

Sababu Moja Kwanini Hupaswi Kukosa Semina Ya Kuanza Mwaka 2022 Kiushindi

Usipojiandaa kushinda maana yake umejiandaa kushindwa. Je, umejiandaaje kuanza mwaka 2022? Umejianda kuanza mwaka wako kiushindi au umejiandaa kuanza mwaka wako kimazoea, kiuchovu? Mtu makini yeyote yule anayejua kile anachotaka hawezi kukubali kuanza mwaka wake kama ajali, lazima atataka kuanza mwaka wake kiushindi. Watu wengi huwa wanawasha moto wa hamasa januari mosi, lakini baada ya …

Usilazimishe Matatizo Haya Kwenye Mahusiano Yako

Kila mtu anajua wazi kwamba kuna vitu akivifanya katika mahusiano ya mke na mume basi vinakwenda kuharibu amani ya ndoa. Na watu wanalijua hilo lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukubali kusukumwa na hisia za hasira ndani yake. Kwa mfano, kuna baadhi ya makosa ambayo mwenza wako akikufanyia unaweza ukayapuuzia kwanza na ukaja kuongea …

Kosa Lako Liko Hapa

Unaweza kuona mambo ni magumu kwa sababu umetumia kila mbinu ambayo iliwasaidia watu wengine kuweza kufanikiwa. Wakati mwingine unaweza kutumia kila mbinu ambayo iliwawezesha watu wengine kuweza kufanikiwa na kupata mafanikio makubwa. Lakini hupati matokeo makubwa kama waliyowahi kupata wao. Unajiuliza je, unakosea wapi?Jibu lake, unaweza kuwa umeshindwa kutimiza ndoto zako kwa sababu unatumia mbinu …

Usipoteze Sifa Hizi Mbili Kama Unataka Kuwa Kiongozi Bora

Kiasili kila mtu ni kiongozi wa maisha yake mwenyewe. Hata kama unajihisi wewe siyo kiongozi, basi leo jiambie kuwa wewe ni kiongozi wa maisha yako mwenyewe na jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe kwa sababu mkurugenzi mkuu wa maisha yako ni wewe mwenyewe. Hata kama hujawahi kupata cheo sehemu yoyote ile, leo ondoka na …

Jifunze Kuongeza Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini soda mtaani kwako zinauzwa shilingi mia tano, lakini ukienda sehemu nyingine unakuta soda hiyo hiyo inauzwa mpaka elfu tano? Hapa kitu kikubwa kinachotofautisha ni thamani tu. Ndiyo maana shabaha yangu kubwa ya leo ni kukusihi wewe rafiki yangu ujifunze kuongeza thamani yako. Inawezekana watu wanakuchukulia poa, wanakuona yule yule kwa …

Huu Ndiyo Mwanzo Wa Hekima Zote

Tukiwa na hekima basi tumepata yote. Kwa sababu hekima ndiyo inatusaidia kutumia vizuri vile ambavyo tunavyo. Unaweza ukawa na rasilimali nzuri za kukuwezesha kupiga hatua katika maisha lakini ukakosa hekima za kutumia rasilimali hizo. Aliyekuwa mwanafalsafa Aristotle enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema, kujijua wewe mwenyewe ni mwanzo wa hekima yote. Ni kweli, wako …

Siri Ya Kushinda Mchezo Wowote Ule

Watu huwa wanafikiria mambo ni marahisi sana, mambo siyo marahisi ndiyo maana watu wengi hawafanyi na hawajapata kile wanachotaka. Ukiangalia ndani ya mwaka huu biashara zilizoanzishwa ni nyingi, na tafiti za biashara zinasikitisha sana. Kati ya biashara kumi zilizoanzishwa mwaka huu zinazokua ni mbili au moja. Na ukitaka kuliona hilo angalia mtaani wangapi walianza biashara …

Kuwa Makini Na Maswali Haya

Ukiuliza swali sahihi lazima utapata majibu sahihi.Maswali unayouliza unapaswa uwe nayo makini sana. Kwa sababu yako maswali mengine ukimuuliza mtu utaweza ukaharibu kabisa hali yake kihisia. Kuwa makini na maswali unayomuuliza mtu kwani yanaweza yakasababisha kuharibu hisia zake. Kwa mfano, unamuuliza mtu mbona wewe huna watoto, mbona wewe hujaolewa au hujaoa nk. Ni maswali ya …

Design a site like this with WordPress.com
Get started