Usitumie Kabisa Fedha Hizi

Usitumie fedha ambazo huna kununua vitu ambavyo huvihitaji kuwafurahisha watu ambao hawana muda au hawajali kwa kile ulichofanya. Hii ina maana gani? Hapa mtu anakuwa ananunua vitu kwa mkopo ili aonekane na yeye ana vitu hivyo au ana uwezo au hadhi fulani, wakati wale anaowaonesha hata hawajali juu ya vile vitu anavyonunua. Yaani hapa utakua …

Kwenye Kila Bure Jiulize Unalipaje?

Ukichunguza kila bure siyo bure kweli. Bure inakuzuia kupata kile unachotaka. Kwa mfano, unaenda kununua kitu unachokitaka halafu unakutana na kitu kingine cha bure lakini mpaka ununue kitu kingine usichotaka ndiyo utaweza kupata hicho kitu cha bure. Kwa mfano, nunua mbili upate moja bure. Kuepuka kuingia kwenye mtego wa bure na baadaye utahitajika kulipa zaidi. …

Hatua Ya Kwanza Kuchukua Kama Unataka Kubadili Maisha Yako

Ni kukubali kwamba kila kitu kwenye maisha yako ni wajibu wako. Wako watu bado wanaamini kuwa jukumu la maisha yao sio lao bali ni la watu wengine. Kwa mfano, ikitokea ndugu mmoja ana uwezo wa kifedha wale ndugu ambao hawana fedha wanaamini kwamba yule ambaye amefanikiwa kifedha ndiyo anatakiwa kubeba jukumu la maisha yao. Hakuna …

Unapotoa Ujumbe Wowote Hakikisha Unazingatia Hili

Kama unatoa ujumbe au unaongea na mtu kwa kumwelekeza kitu fulani ni vema baada ya kumaliza kutoa ujumbe wako upate mrejesho wa kile ulichosema. Siyo watu wote wanaelewa kile unachosema. Kama unatoa tangazo kwenye kadamnasi, hakikisha unapata mrejesho kwenye kadamnasi yako na kuwauliza wameelewa nini? Ukimwelewesha mtu na akakwambia ameelewa, mdake hapo hapo muulize umeelewa …

Kama Unataka Kutoka Kwenye Matatizo Ya Kifedha

Kinachowarudisha watu nyuma ni kutaka kuishi maisha ya kuiga. Watu wananunua vitu ambavyo hawawezi kuvimudu ili tu waonekane nao wapo, waonekane nao wana uwezo. Kama unataka kutoka kwenye matatizo ya kifedha ambayo unayo, lazima uache kwanza kuiga maisha ya wengine na uanze kuishi uhalisia wako. Chagua kuishi maisha yako mwenyewe. Kuwa tayari kuchekwa na kuonekana …

Fursa Mpya Zitaua Ndoto Zako

Nimeshafanya kila kitu lakini sifanikiwi. Ni kauli za watu ambao wamejaribu kila kitu, wamejaribu kila biashara unayojua wewe lakini cha ajabu hakuna walichopata zaidi ya kulalamika. Unajua ni kwanini? Ni kwa sababu ya ugonjwa wa fursa mpya. Watu wamekuwa hawatulii kwenye kitu kimoja, wanaanzisha hiki, kabla hata hawajapata matokeo wanaacha na wanakwenda kwenye kitu kingine. …

Wekeza Kwa Ajili Ya Kitu Hiki

Wekeza kwa ajili ya kustaafu kwako. Unatakiwa kuizidi serikali akili, badala ya kusubiria mafao yanayotolewa na mifuko ya kijamii anza kujiwekezea kwa ajili yako binafsi. Nafikiri unaona ni kwa namna gani unaona watu wengi wanavyokuwa wanasumbuliwa na mafao yao.Yaani kila siku hii mifuko ya mafao sheria zake zinabadilishwa. Unatakiwa ujiandae na mafao yako binafsi na …

Epuka Kwenda Sehemu Hii Ili Usife

Mwekezaji Charles Munger anasema hivi, anachotaka kujua ni wapi akienda atakufa, ili aepuke kwenda sehemu hiyo. Angalia ni hatari gani kwenye kila eneo la maisha yako zipo na epuka hatari hizo. Kabla hujaanza biashara fulani zijue changamoto za biashara hiyo ili ukiingia changamoto zisikuyumbishe kwa kuwa tayari umeshazijua. Kwenye eneo la kiafya jua ni changamato …

Jamii Itakuambia Usijisumbue Sana

Pale unapofanya kazi muda wa ziada, Pale unapokuwa mtu wa kuzungumzia fedha mara kwa mara, Pale unapoweka mipango ya mikubwa ya mabilioni, na pale unapofanya kazi au biashara zaidi ya moja. Pale unapokuwa ni mtu wa msimamo. Pale unapokuwa unaishi maisha yako hukusi watu watakaokuambia unaenda kinyume na jamii. Jamii huwa inapenda uende kama wengine …

Vumilia Vitu Vyote Lakini Siyo Hiki

Kitu usichopenda. Usivumilie kitu ambacho hukipendi kwenye maisha yako. Hata kama kila mtu anavumilia, hata kama kila mtu anakichukulia kawaida. Kama kitu hukipendi, au kama unaona siyo viwango vyako,usikubaliane nacho.Wewe fanya kazi kupata kile unachotaka, kile ambacho ni viwango vyako. Waliozoea shida watakushawishi na wewe uzoee shida. Walioshindwa kwenye ndoa watakushawishi uone ndoa ni mbaya …

Design a site like this with WordPress.com
Get started