William Arthur Ward aliwahi kusema, “kujisikia kutoa shukrani na kutoitoa ni kama kufunga zawadi na kutoitoa.” Rafiki yangu, Natumia nafasi hii kukushukuru kwa kuwa mshirika mkubwa wa kazi zangu za uandishi katika mwaka 2019.Bila wewe kazi zangu hazina kazi. Kushukuru ni kuomba tena. Hivyo ninakuomba tena tuendelee kuwa pamoja mwaka 2020 tuendelee kushirikishana maarifa mazuri …
Category Archives: Uncategorized
Hizi Ndiyo Siku Mbili katika mwaka ambapo hakuna Kinachofanyika
Kuna siku mbili katika mwaka ambapo watu huwa wanajidanganya sana katika siku hizi.Huenda katika mwaka kila siku watu huwa wanajipa matumaini mbalimbali lakini cha kushangaza hakuna anayefanikiwa ndani ya siku hizo. Huenda hata wewe umeshajidanganya sana Katika siku hizi mbili ambazo ni Jana na kesho. Kamwe kesho haitokuja kutokea katika maisha yako. Umejipotezea mengi sana …
Continue reading “Hizi Ndiyo Siku Mbili katika mwaka ambapo hakuna Kinachofanyika”
Unaweza Kukubali Kushindwa Lakini…
Aliyekuwa bingwa wa mchezo wa kikapu Michael Jodarn aliwahi kunukuliwa akisema ” ninaweza kukubali kushindwa lakini siwezi kukubali kutokujaribu. Huwa tukishindwa mara ya kwanza ni kama vile tumepewa tiketi ya kushindwa milele.Kushindwa kwa mara ya kwanza imewafanya watu wengi sana kutokuthubutu na kujaribu tena. Kuna watu ni ving’ang’anizi wa kujaribu mpaka wapate matokeo ndiyo wataweza …
Hapa Ndiyo Mahali Ambapo Dunia Inazaliwa
Kila mmoja wetu hapa duniani amezaliwa katika familia. Ni mpango wa Mungu kila mwanadamu kuzaliwa katika familia.Na kupitia familia ndiyo mahali dunia inapozaliwa. Kupitia familia zetu, tunajipatia miito mbalimbali duniani. Familia ndiyo nyumba ya dunia ambayo kila mmoja wetu anaishi na kujifunza misingi ya dunia. Familia zetu zikiwa takatifu zinafananishwa na mbingu ndogo hapa duniani. …
Nimewashinda Maadui Zangu Kwa Kuwafanya Kuwa Marafiki Zangu
Dalai Lama enzi za uhai wake aliwahi kusema kuwa nimewashinda maadui zangu kwa kuwafanya kuwa marafiki zangu. Hii ni kauli yenye nguvu sana katika mambo ya msamaha. Moja ya mbinu nzuri ya kuwavuta maadui zetu ni kuwafanya kuwa marafiki zetu kwa njia hii tunakuwa tunawamaliza bila kutumia nguvu. Hatuwezi kumaliza chuki kwa chuki bali tunaweza …
Continue reading “Nimewashinda Maadui Zangu Kwa Kuwafanya Kuwa Marafiki Zangu”
Kuanza Upya Siyo Ujinga
Hutakiwi kujilaumu pale mambo yanapokuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Kwa lolote tunalofanya , basi chochote kinaweza kutokea. Hakuna mkataba kuwa kila tunalofanya basi mambo yataenda kama vile tunavyotaka sisi. Huko ni kujidanganya kweli, Mambo yanaenda vile yanavyotaka yenyewe. Unapo,pokea na kupoteza shukuru na jifunze tena. Na ikibadi anza upya kwani kuanza upya siyo ujinga. Huenda ulipanga …
Kuwa Kiherehere Wa Maisha Yako
Kama kila mtu angekuwa kiherehere wa maisha yake, basi mambo yangekuwa mazuri kweli. Watu wengi siyo vinara wa kufuatilia mambo yao binafsi bali watu ni vinara kwa kufuatilia maisha ya watu wengine. Tunatumia muda na gharama kubwa katika kufuatilia mambo ya watu wengine huku ya kwetu tukiyaacha bila kuyafanyia kazi. Kabla hujaanza zoezi la kumfuatilia …
Hiki Ndiyo Kitu Cha Uhakika Katika Biashara
Mara nyingi tunapoanza kufanya kitu tunakuwa na mategemeo fulani. Kama ni kufanya biashara huwa tunategemea kupata faida. Ni kawaida ya watu wengi kujiandaa na kuwa na mategemeo ya kupata faida kwenye kile wanachofanya. Ni kweli faida ni ushindi tunaopata baada ya kufanikiwa katika kile tunachofanya. Lakini kitu cha uhakika kabisa katika biashara ni changamoto. Kama …
Continue reading “Hiki Ndiyo Kitu Cha Uhakika Katika Biashara”
Hii Ndiyo Njia Ya uhakika Ya Kipato
Kipato ni kile ambacho mtu analipwa baada ya kutoa thamani fulani. Iko njia moja inayopendwa na watu wengi ya kuingiza kipato ambayo ni njia ya moja kwa moja yaani active income. Kwa mfano, ajira au mtu aliyejiajiri ambaye asipokuwepo kazini moja kwa moja hakuna kipato kitakachoingia. Njia hii inapendwa na wengi na wengi ndiyo wako …
Mambo Mawili Ambayo Yanakukwamisha Kwenye Maisha Yako
Kama unaweka juhudi kila siku halafu hupati kile unachotaka basi ziko sehemu mbili zinazokukwamisha na leo ndiyo siku pekee ya kuzijua sehemu hizo. Kama umekwama kuna vitu viwili vinavyokuwa vimekukwamisha navyo ni ; Moja ni kile unachojua au kutokujua. Huenda kile unachojua hujakifanya inavyotakiwa ndiyo maana umekwama au unapata matokeo hasi labda kwa sababu ya …
Continue reading “Mambo Mawili Ambayo Yanakukwamisha Kwenye Maisha Yako”