Mtu Anayepaswa Kulaumiwa Kwenye Matatizo Yako Ya Kifedha

Siku zote huwa nina amini kuwa matatizo yote ambayo mtu anayo mtu mwenye ndiyo anaweza kuyamaliza lakini siyo mtu mwingine. Mpaka mhusika mwenyewe aamue, hata katika mafanikio yoyote yale lazima mhusika aamue kile anachotaka kwanza kwani kanuni ya kwanza ya mafanikio ni kujua haswa kile unachotaka ndiyo utaweza kufanikiwa. Katika suala la fedha pia,tunaamini kuwa …

Haya Ndiyo Mambo Mawili Ambayo Huwezi Kuyarudisha

Sijawahi kusikia mtu analalamika kuwa bubu yaani mtu ambaye haongei amegombana naye kwa sababu amemwambia moja mbili tatu. Lakini sisi ambao tumepewa midomo inayotoa sauti ndiyo tumekuwa shida sana. Ukiwa mtu wa kukaa kimya na kufunga mdomo wako utaweza kujiepusha na mengi kwani karibu matatizo mengi tunayokutana nayo kwenye mahusiano yetu chanzo chake ni kauli. …

Ni Sisi Binadamu Pekee Ambao Tuna Sifa Hii…

Sisi binadamu tumekuwa ni watu tunaotengeneza picha ya vitu ambavyo hata havipo muda mwingine katika uhalisia. Tunaipa akili picha ambayo inakuja kututesa hapo baadaye.Mara nyingi mambo yote tunayohofia mchezo mzima unatengenezwa kwenye akili. Wanyama wengine wote wanaendesha maisha yao kwa hisia tangu wanazaliwa lakini sisi binadamu tumepewa uwezo wa kufikiri na kubadili mazingira yetu. Uwezo …

Huu Ndiyo Msingi Ambao Kila Kiongozi Anapaswa Kuwa Nao

Habari njema ni kwamba kila mtu ni kiongozi hapa duniani, hata kama huna watu unaowaongoza lakini kuna mtu ambaye unamuongoza ambaye ndiyo wewe mwenyewe.  Kila siku unajiongoza na unafanya vizuri kwa uthibitisho huo wewe ni kiongozi na ni mkurugenzi wa maisha yako. Hivyo ninapokuambia  wewe ni kiongozi furahia na wala usibishe kwani hilo halina ubishi …

Huwezi Kutoa Kama Huna

Kila siku ukiamka, ukisiliza radio, ukiwasha tv, ukitembelea sehemu ambazo watu wanafanya mauzo ya vitu lazima utakutana na watu wanaokushawishi wewe utoe kitu. Na mara nyingi sana dunia inatushawishi kila siku namna ya kutoa fedha zetu. Ni mara ngapi vyombo vya habari vinakutangazia namna ya kupata fedha?Lakini mambo yanakwenda kinyume kabisa matangazo mengi na watu …

Hii Ndiyo Maana Ya ujasiri Kadiri Ya Plato

Katika haya maisha muda mwingine hata kuishi ni ujasiri alisema mwanafalsafa wa kistoa Seneca. Ni kweli kuishi ni ujasiri kwani hizi changamoto za dunia wako wengine wanashindwa kukabiliana nazo na hata kuamua kujiua kabisa. Kumbe basi, kama wewe unaendelea kuishi jipe hongera kwani unakutana na mengi lakini bado unapambana bila kushindwa. Mwanafalsafa Plato naye alikuwa …

Hii Ndiyo Asili Ya Dunia

Rafiki, Hata upange mipango mizuri kiasi gani wala dunia haijali hilo. Unapopanga na dunia inapanga hivyo, haitokufikiria wewe muda wote bali asili huwa inapanga vile inavyotaka na siyo vile tunavyotaka sisi. Tunapaswa kulijua hilo, kama dunia ingekuwa inamsikiliza kila mtu una fikiri mambo yangekuwaje? Mwingine anataka mvua, mwingine jua. Kwa asili dunia inajiendesha kwa misingi …

Hiki Ndiyo Kitu Cha Kuepuka Pale Unapojenga Timu

Pale tunapojenga kitu tunatumia nguvu nyingi, fedha nyingi na muda hivyo ukiangalia ni rasilimali nyingi. Lakini pale unapotaka kubomoa kitu ni dakika tu. Kwa mfano, kujenga jina ni kazi, unatumia kila aina za rasilimali lakini kuvunja jina hachukui sekunde. Vivyo hivyo katika kujenga timu, tunapojenga timu tunatumia nguvu nyingi. Na timu ninazozungumzia hapa ni timu …

Huu Ndiyo Ushauri Wa Mwanafalsafa Epictetus Kwa Wale Wote Wanaotaka Kupiga Hatua

Hakuna kitu ambacho unaweza kufanya na kumfurahisha kila mtu. Kila binadamu ana maoni yake kwenye kila kitu. Haitokuja kutokea hata siku moja utaweza kumfurahisha kila mtu. Ila mtu pekee ambaye unaweza kumfurahisha hapa duniani ni wewe mwenyewe. Katika suala la mafanikio, kila mtu ana njia zake. Kila mtu ana hadithi zake hivyo hadithi zetu katika …

Unaweza, Ni Suala La Kuamua Tu

Katika hii dunia kila mtu anaweza kuwa vile anataka kama mtu huyo akiamua kufanya kile anachotaka. Watu wengi wanaweza ila hawafanyi kwa sababu hawajaamua. Unajua kuamua ndiyo hatua ya kwanza ya kufikia mafanikio yako.Usipoamua hakuna kizuri kitakachokuja kwako. Binadamu wanafanya vizuri sana pale wanapoamua wao wenyewe kufanya. Binadamu hafanyi vizuri kama akilazimishwa kufanya ila akiamua …

Design a site like this with WordPress.com
Get started