Falsafa ya Ustoa Inayokupa Uhuru, Utulivu na Ujasiri wa Kuishi Maisha Halisia Kwenye falsafa ya Ustoa (Stoicism), kuna wazo moja la kipekee, lenye nguvu kuliko malalamiko yote ya mwanadamu, na lenye uwezo wa kubadilisha maisha yako kabisa.Wazo hilo linaitwa Amor Fati, tafsiri yake: “Penda hatima yako.” Si kukubali tu kinachokupata.Si kuvumilia tu kinachotokea.Ni zaidi ya …
Category Archives: FALSAFA
Ukichaa Wa Muda
Rafiki yangu nikupendaye, Hisia zinapokuwa juu, fikra zinakuwa chini. Na fikra zikiwa chini, uwezo wetu wa kufanya maamuzi unakuwa chini. Kila mmoja kuna wakati anakua na ukichaa wa muda. Na ukichaa wa muda ni hasira. Hasira ni ukichaa wa muda, wakati una hasira, fikra zinakuwa chini ndiyo maana inapelekea kufanya maamuzi yasiyofaa. Ndiyo maana unashangaa …
Rafiki Wa Kweli
Kwenye maisha ukitaka kufika haraka, basi nenda peke yako.Na ukitaka kufika mbali, nenda na wenzako. Kwa maana hiyo basi, tunahitaji marafiki sana au kifupi tunahitaji watu wa kushirikiana nao ili tuweze kufika mbali. Lakini watu wa kushirikiana nao wamekuwa changamoto kubwa kwetu. Kazi zipo lakini watu wa kufanya nao kazi ndiyo shida. Kuna mtu mmoja …
Usiende Kinyume Na Asili
Mpendwa rafiki yangu, Kama utayaendesha maisha yako kadiri ya asili basi hautakuwa na maisha magumu. Kinachofanya maisha kuwa magumu, ni watu kuhangaika na vitu vingi. Kiasili, mahitaji ya msingi ni machache lakini anasa ndiyo zinafanya maisha kuwa magumu. Maisha tayari ni magumu, usiyafanye kuwa magumu zaidi kwa kuhangaika na mambo mengi.Jitafute na ukishajipata, tulia kwenye …
Jinsi Ya Kukabiliana Na Hali Pale Mambo Yanapoenda Vibaya
Ni wazi kabisa mambo hayawezi kwenda kama vile unavyotaka wewe. Dunia haiwezi kwenda kadiri ya matakwa yako. Dunia inaenda kadiri ya vile inavyotaka. Mambo yanatokea kama yalivyopangwa kutokea. Unawezaje kukubaliana na mambo pale yanapokwenda vibaya? Jibu, ni wewe kutokwenda vibaya kama mambo yalivyoenda. Kumbuka, mambo yameenda vibaya usikubali na hayo mambo yakuendeshe na wewe uwende …
Continue reading “Jinsi Ya Kukabiliana Na Hali Pale Mambo Yanapoenda Vibaya”
Wakati Mzuri Wa Kununua Mwamvuli
Wakati mzuri wa kuandaa paa lako ni wakati jua linawaka. Hii ina maana kwamba muda mzuri wa kujiandaa na kitu ni kabla ya kile kitu hakijatokea. Unaona wazi jinsi mvua inaponyesha miamvuli inauzwa kwa bei kubwa. Kama hutaki kununua mwambie kwa bei kubwa basi nunua kabla ya mvua.Muda mzuri wa kujiandaa na dharura ni kabla …
Usimwambie Mtu, Nimekuambia Wewe Tu
Ni maneno ambayo watu huyatumia kujihakikishia usalama pale wanapotoa jambo lao kwa watu wengine. Usijidanganye kwamba ukimwambia mtu hivyo ndiyo mambo yatakuwa safi bali ndiyo kama vile umemwambia fanya. Kama una jambo lako na unataka watu wasijue ni bora usiseme kabisa kuliko kusema halafu unamwambia nimekuambia wewe tu lakini usimwambie mtu mwingine.Wimbo unakuwa ni mmoja …
Swali Muhimu Sana La Kujiuliza Pale Tu Unapokutana Na Kitu Usichotegemea
Mwandishi Deepak Chopra anasema hakuna ajali, ila kuna kusudi ambalo bado hatujalijua. Mara nyingi mambo yanapotokea kwenye maisha yako bila ya wewe kutegemea kutokea huwa yanapotokea unasema ni ajali. Lakini Chopra anatuambia hakuna ajali, badala yake kuna kusudi ambalo bado hatujalijua. Kila kinachotokea kwenye maisha yako, iwe ni kizuri au kibaya jua kimekuja na kusudi …
Continue reading “Swali Muhimu Sana La Kujiuliza Pale Tu Unapokutana Na Kitu Usichotegemea”
Sheria Unayopaswa Kuiogopa Kwani Haina Huruma Na Mtu
Kiasili hakuna kitu kibaya wala kizuri hapa duniani. Mara nyingi huwa tunapokea kile tunachotoa. Leo nataka nikupe sheria moja ambayo ukiifuata utakua na maisha mazuri na ukienda kinyume nayo utakua na maisha magumu. Sheria hiyo inaitwa karma. Karma ni sheria ya asili ambayo inamrudishia mtu kile ambacho amekitoa kwa mwingine. Kwa mfano, ukimfanyia mtu kizuri, …
Continue reading “Sheria Unayopaswa Kuiogopa Kwani Haina Huruma Na Mtu”
Hakuna Kifo Kibaya Kama Hiki
Memento Mori#2Death is not the greatest loss in life. The greatest loss is what dies inside us while we live. – Norman Cousins Kifo kibaya na kikubwa ni kile ambacho watu huwa wanakufa na utajiri ndani yao wakati wakiwa hai.Kifo siyo kitu kikubwa kama kufa ukiwa hujatimiza ndoto yako ambayo iko ndani yako. Fikiria vitu …