Ni maneno ambayo watu huyatumia kujihakikishia usalama pale wanapotoa jambo lao kwa watu wengine.
Usijidanganye kwamba ukimwambia mtu hivyo ndiyo mambo yatakuwa safi bali ndiyo kama vile umemwambia fanya.
Kama una jambo lako na unataka watu wasijue ni bora usiseme kabisa kuliko kusema halafu unamwambia nimekuambia wewe tu lakini usimwambie mtu mwingine.
Wimbo unakuwa ni mmoja kwa kila mtu wa kusambaza habari kwa wengine.
Duniani wako watu zaidi ya bilioni 7, katika watu hao huwezi kukosa mtu mmoja ambaye unamwamini na kumheshimu na ukamwambia mambo yako na akakutunzia siri zako.
Hatua ya kuchukua leo; Kama mtu siyo sahihi kwako usimwambie mambo yako.
Kama kitu siyo sahihi kufanya usifanye.
Unapowaambia watu wasio sahihi kwako mambo yako ni sawa umeupa kazi upepo wa kusambaza habari zako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog