Mwandishi Deepak Chopra anasema hakuna ajali, ila kuna kusudi ambalo bado hatujalijua.
Mara nyingi mambo yanapotokea kwenye maisha yako bila ya wewe kutegemea kutokea huwa yanapotokea unasema ni ajali.
Lakini Chopra anatuambia hakuna ajali, badala yake kuna kusudi ambalo bado hatujalijua.
Kila kinachotokea kwenye maisha yako, iwe ni kizuri au kibaya jua kimekuja na kusudi fulani.
Unapopatwa na kitu ambacho hukutegemea kitokee, badala ya kulia, kuhuzunika au kufurahia unahitaji kukaa chini na kujiuliza hiki kilichotokea ambacho sikutegemea kama kingetokea kimekuja na kusudi gani kwangu?
Huwa tunaona mambo ni magumu kweli kama yakitokea pasipo sisi kupenda lakini tukiwa tunajiuliza hiki kimekuja kwangu kwa kusudi gani tunapata mlango wa kutokea.
Hakuna kitu kinachokuja kwako kama ajali, chunguza kila kinachotokea na utajua kusudi lake.
Hatua ya kuchukua leo; kaa chini na jitafakari kwa kila jambo linalokuja kwako na jiulize jambo hili limekuja kwangu kwa kusudi gani?
Kumbuka hakuna ajali, ila kuna kusudi ambalo bado HUJALIJUA, hivyo pata picha kila jambo linalotokea unajiuliza limekuja kwako kwa kusudi gani na utapata mengi ambayo ulikuwa hujui na mwanzo uliona ni kama ajali.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog