
Kiasili hakuna kitu kibaya wala kizuri hapa duniani.
Mara nyingi huwa tunapokea kile tunachotoa.
Leo nataka nikupe sheria moja ambayo ukiifuata utakua na maisha mazuri na ukienda kinyume nayo utakua na maisha magumu.
Sheria hiyo inaitwa karma. Karma ni sheria ya asili ambayo inamrudishia mtu kile ambacho amekitoa kwa mwingine. Kwa mfano, ukimfanyia mtu kizuri, uzuri utakurudia, ukimfanyia mtu kitu kibaya ubaya utakurudia.
Mara zote kuwa makini kwenye hii dunia, usiwatendee wengine kile ambacho wewe hupendi kutendewa.
Kama kazi yako ni kukwamisha mambo ya wengine, jua na wewe kuna mambo mengine asili itakukwamishia.
Huna unachoweza kukwepa kwenye hii dunia, kile unachotoa kwa wengine ndiyo kinakurudia.
Malipo yapo hapa hapa duniani, usifikiri mpaka uende mbinguni. Dunia inaanza kukuadhibu hapa hapa duniani, moto unaowawashia wengine utakurudia na wewe.
Maisha ni mafupi, hangaika na yale yenye maana kwako. Usiharibu maisha ya watu, usijaribu kuharibu ndoto za watu.
Jiulize kila siku kazi yako ni kusaidia watu kwenda mbele kupitia kile unachofanya au kazi yako ni kurudisha nyuma watu?
Machozi ya wale unaowafanyia ubaya hayawezi kukuacha salama.
Usiisababishie familia yako kubeba dhambi zako, maana mabaya unayofanya huwa yanarudi kwenye familia yako, hivyo unapoishi ishi katika uadilifu, uaminifu. Kuwa mwema na tenda mema.
Kila mtu anavuna kile anachopanda, je unapanda mbegu gani ili uweze kuvuna? Kama unapanda mazuri utavuna mazuri na kama unapanda mabaya utavuna mabaya.
Hatua ya kuchukua leo; tumika kuwawezesha watu kupata kile wanachotaka na siyo kwenda kinyume.
Furahia kila siku kuishi maisha kadiri ya misingi ya maadili, sheria za asili na za nchi.
Kumbuka, sheria ya karma huwa haina huruma na mtu, inakulipa hapa hapa duniani, fanya yale mazuri unayotaka yakurudie kwenye maisha yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog