Biashara yoyote ambayo haina wateja ina hatari ya kuanguka.
Kwa sababu wateja ndiyo wanaoleta fedha kwenye biashara na fedha ndiyo damu ya biashara, pata picha wewe kama binadamu mwili wako hauna damu moyo unaweza kufanya kazi?
Unapata majibu kwamba mauzo ndiyo moyo wa biashara. Hivyo, kwa chochote unachofanya kwenye biashara jiulize kinachangiaje kuongeza MAUZO?
Ziko nyingi za kupata wateja kwenye biashara yako na njia rahisi na ya kupata wateja ni ya rufaa.
Rufaa ikoje kwani?
Iko hivi, yaani pale mteja anaponunua na kusema asante kwa huduma yako, unamwomba akusaidie mtu wake wa karibu ambaye anaweza kunufaika na huduma yako.
Na kama umetoa huduma nzuri, hawezi kuacha kukupendekezea atakuambia, kwa sababu kila mteja unayemwona nyuma wake ana watu zaidi ya 250.
Kumbe basi, ukimhudumia mteja mmoja vizuri atakusambazia kwa watu wake na ukimhudumia vibaya vivyo hivyo atakwenda kuwaambia na wengine.
Kwahiyo, njia ya rufaa ni njia bora kupata wateja. Na ni rahisi na ya kivivu kabisa haina gharama.
Hatua ya kuchukua leo; kwa kila mteja anayekuja leo kwenye biashara yako, hakikisha unamwomba akusaidie mtu wake wa karibu ambaye anaweza kunufaika na kile unachouza.
Kumbuka, ongea na watu uvae viatu , hivyo kazi ni kwako kufanyia kazi haya uliyojifunza leo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog