Pata picha umeenda stendi na kupanda gari halafu unamuuliza swali dereva, hii gari inaenda wapi?
Dereva anakujibu sijui hata inaenda wapi.
Hatua ya kwanza utakayochukua kabla ya mengine ni kushuka kwanza ili usije ukapotea zaidi.
Hii ina maana gani?
Kama bado hujajua kule unakokwenda ni bora usiendelee na safari. Kwa sababu utaendelea kupotea zaidi.
Usiongeze mwendo kama bado hujajua wapi unaenda. Unaongeza mwendo pale unapojua kule unakokwenda.
Jitahidi sana kujifanyia tathmini kwenye kila unachofanya ili uweze kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma.
Kumbuka, kwenye maisha hakuna kusimama ni aidha uende mbele au urudi nyuma.
Na shabaha ya makala ya leo ni kukupa wewe tahadhari, kabla hujaendelea kufanya kile unachofanya jifanyie kwanza
tathmini uone mwenendo wako kabla hujaendelea na safari.
Hatua ya kuchukua leo; kabla hujaendelea na kile unachofanya jifanyie kwanza tathmini uone afya ya kile unachofanya je, uko sehemu sahihi au la.
Kwahiyo, maisha ambayo hayatathiminiwi ni maisha ambayo hayana maana kuishi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog