Unapokutana na changamoto hutakiwi kutaharuki badala yake unatakiwa kununua utulivu wa hali ya juu.

Kwani, unapotaharuki uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi kifikra unakuwa chini na hisia zinakuwa juu.
Huwezi kuamua jambo wakati fikra zako zikiwa chini na hisia zikiwa juu.
Unahitaji sana utulivu wa hali ya juu, ulione tatizo lililotokea ni dogo, unatakiwa ulidogishe tatizo hilo ili lisikuvuruge na uweze kufanya maamuzi sahihi.
Na ili ufanye maamuzi sahihi kifikra, hisia zinapaswa kuwa chini na fikra kuwa juu.
Kila mtu anakutana na changamoto na siyo jambo geni katika maisha ya mwanadamu. Lakini unapotaharuki ndiyo unaongeza tatizo zaidi.
Hatua ya kuchukua leo; nunua utulivu pale unapokutana na changamoto, usitaharuki bali tulia kwanza, vuta pumzi ndani na kutoa nje huku ukipata utulivu halafu fikiria namna sahihi ya kusaidia kile kilichotokea.
Kwahiyo, kwenye maisha yako usiwe mtu wa kutaharuki badala kuwa mtu ambaye ana utulivu wa akili, unaituliza akili yako na kuweza kupata suluhisho.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog