Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hawa Ndiyo Wateja Wazuri

Ukiwa katika mauzo hakuna mteja mzuri kama yule ambaye anajua nini haswa anataka.

Mteja anayejua kile anachotaka ni rahisi kumhudumia na kumpatia huduma bora.

Mteja anayejua kile anachotaka anakuokolea muda. Ukilinganisha na mteja ambaye hajui nini anataka mpaka umweleweshe kila bidhaa kisha achukue maamuzi inachukua muda mrefu kukuelewa na kuchukua hatua ya kufanya manunuzi.

Kila mmoja wetu ni mteja na muuzaji, hivyo basi unapokwenda sokoni hakikisha unajua kile unachotaka ili kuokoa muda na kumpa muda muuzaji kuwahudumia watu wengine kuliko kutumia muda mwingi kuhudumiwa wewe peke yako huku wengine wakiwa wanakosa huduma bora.

Mteja anayejua kile anachotaka mpe kipaumbele kwenye kumpa huduma ya haraka kwani ukimchelewesha huwa wanakasirika na kwenda sehemu nyingine. Wale ambao hawajui kile wanachotaka wasubirishe kwanza kwani watakufanya ushindwe kufanya mauzo na kumpoteza mteja anayejua kile anachotaka.

Wateja wanaojua kile wanachotaka ndiyo wateja wazuri kwani wanakurahisishia kazi. Wale ambao hawajui kile wanachotaka, wanataka muda wako mwingi kiasi kwamba unashindwa kuhudumiwa hata wengine na huenda hata wasinunue licha ya kutumia muda mwingi kumwelewesha.

Mteja anayejua kile anachotaka ni kama msafiri anayejua kule anakokwenda.

Mteja ambaye hajui kile anachotaka ni kama msafiri asiyejua kule anakokwenda kwani utapata shida kumhudumia kile anachotaka.

Kwa mfano, nenda stendi ya magari, msafiri ambaye anaulizwa unaenda wapi na hajui wapi anaenda hawezi kusaidiwa hata kidogo. Na wala watu hawatahangaika na mtu ambaye hajui wapi anaenda.

Hatua ya kuchukua leo; hangaika na wateja wanaojua kile wanachotaka kwa kuwapa kipaumbele kwenye kumpa huduma anayotaka kwani wateja hawa hawachukui muda na wanakupa mauzo ya haraka na uhakika.

Kwenye utoaji wa huduma yoyote ile, inahitaji kazi, uvumilivu kwani kila mteja anakuwa na changamoto yake. Wale ambao wanahitaji muda zaidi kueleweshwa wafanye wawe wa mwisho na anza kuwahudumia wale ambao wanajua nini haswa wanayaka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: