Mara nyingi tunapokutana na changamoto au tatizo huwa tuna kitu ambacho tunakihisi ndiyo kimesababisha au kuna kitu tunafikiria ndiyo kitatatua.
Wakati mwingine tukishaweka mawazo yetu hivyo, tunakuwa hatuwezi kujifunza tena njia mbadala za kutatua au kusababisha.
Unahitaji kuwa tayari kujikosoa wewe mwenyewe, kujiambia kwamba unachofikiri siyo pekee na hivyo kufikiri zaidi na kuona njia unayofikiri ni suluhisho siyo ili uweze kuona njia nyingine zaidi.
Kuwa tayari kujikosoa hata wewe mwenyewe kwani kuna wakati matatizo unayokutana nayo unajisababishia wewe mwenyewe.
Unapokuwa tayari kujikosoa mwenyewe na ukajipa nafasi ya kujua kitu kwa undani zaidi, utakuja kuona ukweli wenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; kabla ya kuwakamata wengine, jikamate wewe mwenyewe na kujikosoa.
Kwahiyo, usiwe mtu wa kuwalaumu wengine kwa kile kilichotokea bali jihoji na ujione na wewe umekosea wapi kwa kile kilichotokea.
Kwenye kila tatizo linalotokea, jiulize na wewe umechangiaje?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog