Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuepuka Kuwa Na Maadui Wengi

Wape watu nafasi ya kujielezea wao zaidi kuliko wewe. Usiwe mtu wa kupenda kujisifia sana pale unapokuwa na watu huwa wanakereka na tabia hii.

Usipende kuibua wivu usiokuwa wa maana kwa kitendo cha kujisifia mafanikio yako mbele za watu.
Mafanikio binafsi usiyaanike kwa watu maana utaibua wivu na matokeo yake mahusiano yanavunjika.

Unapokuwa mtu wa kuongea mambo yako zaidi watu watakukwepa hata kuongea na wewe maana wanajua wakiongea na wewe unajisifia tu na hata huwapi nafasi wengine kuelezea mafanikio yao badala ya wewe kutawala tu mazungumzo.

Watu hufurahi pale wanapopewa nafasi ya kuelezea kile wanachojua. Wanakuwa wanahisi kuthaminiwa na kuonekana wa muhimu.

Mwanafalsafa Rochefoucauld aliwahi kusema, Kama unataka maadui fanikiwa zaidi kuliko marafiki zako, na kama unataka marafiki waache marafiki zako wafanikiwe kuliko wewe.

Ondoka na hili leo, kwenye mazungumzo yoyote yale usiwe mtu wa kujisifia mafanikio yako bali waache marafiki zako wajisifie wao hapo hutoweza hata kuibua wivu.

Sina maana kwamba usipambane kutafuta mafanikio hapana, pambana lakini usiwe mtu wa kujionesha kwa mafanikio ambayo unayo kwani kufanya hivyo hutoweza kuibua wivu ndani yao.

Ni kweli huwa tunaibua wivu ambao hata haupo kwa sababu ya midomo yetu wenyewe. Na wengine wanajikuta wanaongea kwa kujisifia kuliko hata mafanikio yenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; wape nafasi watu wengine ya kushinda zaidi pale mnapokuwa pamoja, Kama kwenye mazungumzo mwachie aongee zaidi yeye hapo hamtaweza kugombana ila mtakubaliana zaidi.

Kwahiyo, fuata ushauri wa mwanafalsafa Rochefoucauld wa kupenda kumwacha rafiki yako afanikiwe zaidi kuliko wewe. Yaani wewe hata kama ukiwa na kitu usijivunie na kujisifia kuwa tu kawaida na wala hamtogombana zaidi ya kuwa marafiki.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: