Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifahamu Nguvu Ya Kujitamkia Matashi Mema

Mpendwa rafiki yangu,

Kuna wakati mwingine unahitaji tu kujitamkia maneno chanya wewe mwenyewe.
Mafanikio yako, yapo katika kinywa chako. Jinsi unavyojitamkia mwili, akili na roho vinapokea na kuwa kama vile unavyotamka. Mazingira ya kua vile unavyotaka kua yanaanza kujitengeneza yenyewe.

Tunaamua maisha tunayotaka kua kwa vinywa vyetu wenyewe. Ukiwa ni mtu wa kujitakia matashi mema utajiona ni mtu wa bahati sana kila siku kwa mfano, anza sasa kujiambia wewe ni mtu mwenye bahati sana halafu baada ya muda utakuja kuniambia ni kwa namna gani bahati zinavyoingia kwenye maisha yako.

Sisi wenyewe tumepewa mamlaka makubwa ya kubariki na kulaani. Huhitaji nabii wa kutoka nje wakati nabii wa maisha yako ni wewe mwenyewe.

Kadiri ya imani yako umekuwa ni mtu wa kusali, sasa muda mwingine huhitaji hata kusali badala yake ongea. Kuongea kwa kujitamkia maneno chanya ni kusali pia. Sema, ongea vile unavyotaka kua na asili itakutengenezea mazingira ya kukutana na bahati yako.

Usitegemee kuona mabadiliko mazuri yanakwenda kutokea katika maisha yako kama wewe mwenyewe unajitamkia mabaya badala ya mazuri.

Ushindi huwa unaanza ndani yetu kabla hata hatujakwenda kuthubutu kwa nje.
Ukishajikubali wewe kwa ndani hakuna mtu wa nje atakayeweza kujikataa.
Hakuna kitu kibaya kama kujikataa wewe mwenyewe kwa ndani. Maumivu ya kujikataa wewe mwenyewe kwa ndani yanatesa sana ukilinganisha na kukataliwa kwa nje.

Sema kitu chochote chanya juu ya maisha leo bila kujali ukubwa au uzito wa kile unachotaka.

Ondoa milima au vikwazo vilivyoko ndani yako, weka imani yako katika matendo, utaishia kupoteza muda kama hujajiruhusu ndani yako kupokea mafanikio au kile unachotaka.
Ruhusu kwa ndani kupokea , lakini kama umefunga ndani kwa maneno hasi usitegemee muujiza kutokea.

Hatua ya chukua leo; jitamkie maneno chanya na kila siku jiambie vile unavyotaka kuwa.

Kwahiyo, nenda kalifanyie kazi zoezi hili. Kama ulikuwa umeshazoea kujitamkia mabaya vunja leo na anza kujifikiria maneno mazuri na kujinenea mambo mazuri.
Unaweza kujipunguzia matatizo kwa kujifikiria mambo chanya lakini kama unataka mazuri na hutaki kufikiria mazuri utaishia kupata matokeo mabaya.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani haykunan jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl.Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: