Ni kawaida watu kupigwa kwenye suala la fedha. Wale wanaotafuta mafanikio ya haraka kwao kupigwa fedha ni jambo la kawaida sana.
Wengi wamelizwa na matapeli kwenye eneo la fedha, wengine wameibiwa na kutapeliwa fedha kwa njia ya simu na nk.
Baada ya kutapeliwa fedha huwa tunakua na maumivu makubwa sana. Kama tunavyojua tena kutoa pesa ni kitendo kinachouma sana na kama ulikuwa hujapangalia fedha zako ziende wapi.
Je ni namna gani tunaweza kupunguza maumivu ya fedha?
Pale tunapotapeliwa au kuibiwa fedha zetu?
Jawabu; chukulia fedha yoyote unayopoteza kama vile umetoa sadaka. Hivi ukitoa sadaka baadaye utakuja kujilaumu kwanini ulitoa sadaka? Kwanza haitokuuma kwa sababu unajua umetoa sadaka.
Iandae akili yako kwa namna hiyo, pale unapojikuta umepoteza fedha wala usisononeke kwa kupoteza fedha bali wewe furahia kwa kuwa umetoa sadaka na chukulia kwamba fedha uliyotoa umekwenda kusaidia watu wenye uhitaji.
Uwe makini sana kwenye kitu kinachohusiana na fedha, usitume fedha kwa mtu ambaye huna uhakika naye kwa mfano, wale wanaotafuta wasaidizi wa kazi, huwa wanaambiwa mara nyingi, tuma nauli na mtu bila hata kujiridhisha anajikuta anatuma nauli na baadaye hapati kile alichokuwa anataka na hela tayari inakuwa imeliwa.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa makini na fedha zako, pale unapokuwa umetapeliwa chukulia tu kama umetoa sadaka.
Kwahiyo, watu wengi kwa sasa wanatapeliwa, watu wanapenda mafanikio ya haraka bila kuyafanyia kazi. Mtu akija kwako na ukimuona humwelewi na anakuambia juu ya mambo ya fedha mfukuze haraka.
Ukiona mtu ananukia harufu ya utapeli usicheke naye na kuwa makini sana katika fedha zako na wale wanaojihusisha na biashara muwe makini kwenye suala la fedha.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo