Huwa tunajidanganya sana kuwa pale tunapomiliki vitu vingi ndiyo tunajiona kuwa sisi ndiyo matajiri.
Kumbe siyo, utajiri hauko kwenye kuwa na vingi bali utajiri uko sehemu moja pekee ambayo ni utajiri wa kutoa.
Utajiri unaotoa ndiyo utajiri unaodumu. Unapomsaidia mtu wewe unaweza kuona kama ni kawaida lakini wale wanaopokea msaada wako ndiyo watu wanaokumbuka sana hata kama wewe hukumbuki.
Tunapaswa kutoa kuliko kupokea, unapotoa ndiyo unapokea zaidi.
Tunapotoa ndiyo tunakuwa tunapanda mbegu ya kudumu ya utajiri.
Ukitaka kuwa na utajiri wa kudumu na wa kipekee ni ule wa kutoa.
Ukishakuwa wewe ni mtu wa kupokea tu, mwisho wa siku utakua huna thamani kwa mfano, kuna bahari moja ambayo iko mashariki na kati, huwa inapokea tu maji bila kutoa mpaka imefikia mahali maji yake hayafai tena kwa matumizi ya kibinadamu.
Mwanafalsafa Marcus Aurelius aliwahi kusema, utajiri pekee ambao utadumu ni ule wa kutoa.
Ni sheria ya asili kwamba huwezi kupokea bila kutoa. Tunapokuwa watu wa kutoa tunaacha alama na kitendo hicho kinafanya tuendelee kukumbukwa na jamii.
Ukitaka kukumbukwa uwe mtoaji kwa wengine. Watu watakulilia pale utakapogusa maisha yao na siyo kugusa maisha yako. Kwa mfano, ni Rahisi muuza chips kukumbukwa mtaani kwako kuliko wewe uliyejenga nyumba. Kwanini? Muuza chips amegusa maisha ya watu kupitia huduma ya chips anayotoa hivyo jamii inakuwa inamtegemea kwa chips anazouza lakini nyumba ni alama binafsi ambayo hujawagusa watu.
Fanya kile ambacho unaweza kugusa maisha ya watu na usiwe mtu wa kujiangalia wewe tu bali angalia watu wengine watanufaikaje na kile unachofanya.
Hatua ya kuchukua leo; utajiri pekee ambao utadumu ni ule unaotoa kwa wengine.
Usijivunie vile unavyomiliki jivunie umewasaidiaje watu kwa vile ambavyo unavyo na kubadilisha maisha yao?
Kwahiyo, Kama unataka utajiri wa kudumu, kuwa mtu wa kutoa utajiri wako kwa wengine. Hii ina maana kwamba sehemu ya utajiri wako unairudisha kwa jamii kwa kusaidia wengine.
Ukiwa bora, wasaidie wengine kufanikiwa kwenye kile wanachotaka.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo