Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Kikwazo Kikubwa Katika Mafanikio

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri kuwajibika katika majukumu yako ya kila siku. Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo lakini pia tunamshukuru Mungu kwa kuweza kutustahilisha kuiona siku hii ya leo. Hivyo ni vema na haki kutumia vizuri zawadi hii ya siku hii ya leo. Kumbuka kutumia muda wako katika mambo chanya na siyo hasi.

Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza kikwazo kikubwa katika mafanikio. Rafiki nakusihi sana uweze kuambatana na mimi mwanzo hadi mwisho ili uweze kufahamu yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Je uko tayari rafiki? Basi karibu tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Image result for TO WORSHIP WEALTH

Mpendwa rafiki, katika maisha yetu ya kila siku ni lazima tutumie hela ili tuweze kuendesha maisha yetu. Fedha ni chombo muhimu sana katika maisha yetu hii imedhihirishwa hata katika kitabu cha Biblia kuwa fedha ni jawabu la mambo yote. Kama fedha ni jawabu la mambo yote hivyo ni muhimu sana kuwa na pesa. Hivyo ni vema na haki pia kuongeza juhudi ili tuweze kuzipata.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Paradox Of Choices

Mwandishi na rafiki yangu Makirita Amani anatualikwa kwa kusema mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa. Ooh! Kumbe basi, mimi na wewe kufanikiwa ni haki yetu ya kuzaliwa hapa duniani hivyo hutakiwi kukata tamaa bali ni kuendelea kupambana na kuweza kufika juu ya kilele. Habari njema ni kwamba duniani kuna fedha nyingi kuliko watu walioko. Utajiri wa Aliko Dangote ni mkubwa kuliko idadi ya watu duniani hivyo kama akiamua leo anaweza kumgawia kila mtu kiasi cha dola moja.

Mpendwa msomaji, turudi katika malengo mahususi ya somo letu la leo ambapo hapo mwanzo niliweza kukuhabarisha kuwa kikwazo kikubwa katika mafaniko ndio malengo mahususi ya somo letu la leo. Mpendwa rafiki kama mafanikio ni haki yetu ya kuzaliwa kwahiyo ni muhimu kila mtu kuwa na mali lakini kumbuka ya kwamba kikwazo kikubwa katika mafanikio ni kuabudu mali.

Rafiki, ule usemi wa kuabudu masanamu ndio huu sasa wa kuabudu mali yaani mtu anakuwa anatawaliwa na mali badala ya kuzitawala mali. Ngoja kwanza nikushirikishe alichokisema mwandishi Albert Nyaluke Sanga katika kitabu chake cha Gia Kubwa. Anasema ‘’ ukimiliki mali aina yoyote iwe miradi, maduka, magari, mashamba n.k usiingie kwenye mtego wa kuziweka mali zako moyoni. Mali zako zikiwa moyoni upende usipende lazima utaziabudu tu. Kuabudu mali ni pale unapoambatanisha moyo wako na mali zako.

SOMA; Fahamu Kitu Muhimu Ambacho Familia Yako Inakosa

Mpendwa msomaji, mwandishi sanga aliweza pia kutoa mfano katika biashara yake ya magari aliyokuwa akifanya jinsi na yeye alivyoweza kudakwa na mtego huu wa kuabudu mali. Kilichokuwa kinamtokea ni kwamba magari yanapokuwa yanaondoka asubuhi moyo wake unaondoka na magari. Yaani akili yake yote inakuwa kwenye magari yaani anakuwa hana amani hata dakika moja kwa muda wote magari yanapokuwa mbali naye.

Mpendwa msomaji, hivyo tunaona madhara ya kuabudu mali. Yanakufanya unakosa utulivu hata wa mambo mengine wewe akili inakuwa imebeba mali na hivyo kukupelekea kuziabaudu. Hivyo ni vema kuepuka hii hali iliweze kufurahia maisha.
Hatua ya kuchukua leo, acha tabia ya kuabudu mali kwani kuabudu mali inakupotezea umakini na ushirikiano katika idara nyingine katika maisha yako. Huwezi kufurahia maisha kama wewe ni mtu wa kuziabudu mali zako hata kama una utajiri mkubwa kiasi gani. Maisha ni furaha hivyo furahia maisha siyo kupata mateso , huzuni juu ya mali na tafuta mali lakini kamwe usiziabudu.

Kwa kuhitimisha, somo letu la leo linatualika sisi sote kuweza kuacha kuziabudu mali tulizonazo. Kuziabudu mali ni ishara ya mtazamo hasi kwenye maisha unaokupelekea hata kupoteza mahusiano mazuri na familia yako, na watu watu walikuzunguka na n.k.
Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: