Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri rafiki yangu. Mpendwa msomaji, tumebakiza siku moja tu kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. Je mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka gani kwako? Na ungependa mwaka 2017 kuwa mwaka gani kwako? Hayo ni maswali muhimu unayopaswa kujiuliza kabla ya mwaka kuisha.
Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Leo tutakwenda kujifunza tafakari ya mwaka 2017 kwa kujiuliza swali hili ‘’ je mwaka 2017 ni mwka gani kwako yaani unataka mwaka 2017 uwe ni mwaka wa aina gani kwako?
Kwahiyo, maamuzi yako mikononi mwako kuamua vile unavyotaka kuwa kwani maisha ni kuchagua vile unavyotaka kua. Katika mwaka 2017 lazima uchague unataka uwe ni mwaka gani kwako kwa mfano, ‘’ mwaka 2017 nataka uwe ni mwaka wa kupaa kimafanikio katika mafiga matatu yaani kiroho, kimwili na kiakili na pia, kuthubutu kufanya vile vitu ambavyo sijawahi kufanya’’.
SOMA; Maeneo Matatu (03) Muhimu Ya Kufanyia Usafi Ndani Ya Siku Kumi Zilizobaki Kabla Ya Mwaka 2016 Kuisha
Mpendwa rafiki, usipojichangulia kitu unachotaka kumbuka kupata kitu ambacho hukutarajia kukipata hivyo ni lazima uchague unataka nini. Kwa mfano, huwezi kwenda mahali ukapata huduma kama hujasema wewe unataka kuhudumiwa kitu gani.
Katika mwaka 2017 unatakiwa kuwa vitu hivi muhimu vya kukupa hamasa katika yale mambo unayofanya;
Kwanza kabisa, unatakiwa kuwa na kauli mbiu itakayokuwa inakuongoza na kukupa hamasa ndani ya mwaka mzima. Hamasa ni kichocheo chanya katika kazi tunazofanya kila siku katika maisha yetu hapa duniani. Chagua kauli mbiu yako ya hamasa na iweke chumbani kwako kila unapoingia na kutoka unaisoma.
Pili, unatakiwa kuchagua watu wa kuambatana nao katika mwaka huo. Kama unataka kufanikiwa kifedha tafuta mtu aliyefanikiwa kifedha atakupa mwongozo chanya, kama unataka kukua kiroho tafuta mtu aliyekua kiroho. Kila eneo unalotaka kwenda tafuta mtu chanya unayeweza kwenda naye mpaka kileleni. Kama ulikuwa kwenye makundi hasi toka mara moja na fukuza marafiki wote ambao hawana mchango chanya kwenye maisha yako.
Aidha, ni vema kuwa silaha muhimu inayoweza kukulinda katika safari yako ya mwako mzima. Silaha hiyo ni maarifa. Unatakiwa kuwa na maarifa sahihi na kwa wakati sahihi ili uweze kufanikiwa. Ujinga ni ugonjwa unao watawala watu wengi. Kila mtu amezaliwa mjinga hajui chochote hivyo ili uweze kuondoka na ujinga unatakiwa kujifunza kila siku. Hapa unatakiwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina, kuwa katika makundi makini yaani chanya, walimu wa kukuongoza na n.k.
Hatua ya kuchukua leo, andaa kauli mbiu ya hamasa itakayokuongoza mwaka 2017. Changua watu wa kuambatana nao, tafuta maarifa chanya na fukuza watu hasi katika maisha yako na wakaribishe watu chanya.
SOMA; Moto Wa Hamasa Utakaokuwezesha Kupata Nafasi Ya Kazi Sehemu Yoyote Duniani
Mwisho, hakuna kitu kitakachoweza kubadilika kwenye maisha yako kama wewe mwenyewe hujweza kubadilika. Utaendelea kuchekesha tu kila mwaka kama unataka mambo mzuri halafu wewe hutaki kubadilika.
Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Pia, Hakikisha unapenda ukurasa wetu wa facebook kwa maarifa zaidi.
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com