Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Paradox Of Choice

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vema.

Mpendwa msomaji, napenda kutumia fursa hii kuwaalika tena katika makala yetu ya leo. Leo nitakwenda kukushirikusha uchambuzi wa kitabu cha Paradox of choice. Karibu tuweze kujifunzs wote kwa pamoja.
Mambo muhimu niliyoweza kujifunza kupitia kitabu cha The Paradox of Choice kilichoandikwa na B. Schwartz.
Yafuatayo ni mambo 20 niliyojifunza kupitia kitabu hiki;

1. Katika ulimwengu wa sasa watu wanakwenda sana katika vituo vya manunuzi yaani shopping center ukilinganisha na kwenda katika nyumba za ibada. Hii inaonesha kuwa watu wengi wamekufa kiroho na wametawaliwa sana na dunia. Watu wanajitoa kuhudumia matumbo kuliko roho. Ukweli ni kwamba mwili haufai kitu hii itakuja kujidhihirisha pale mwili wako unapojitenganisha na roho.
Hatua ya kuchukua;
Usitawaliwe sana na mambo ya kidunia. Ni muhimu kukua kiroho na kumrudia Mungu wako.

2. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano imerahisisha maisha ya watu. Kazi zimerahisishwa ukilinganish na apo awali. Tuna mengi ya kujivunia katika ukuaji wa teknolojia. Ukuaji wa teknolojia una faida zake na hasara zake. Umakini unahitajika juu ya hili.
Hatua ya kuchua; tumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika mambo chanya yatakayobadilisha maisha yako na watu wengine.

3. Kila kitu katika maisha yetu ni chaguo. Tunachagua kuamka asubuhi, kutoka kitandani, kupiga mswaki,kuoga,kuvaa nguo gani nk.
Maisha yetu yako katika kuchagua kwenye kila kitu. Maisha ni kuchagua hivyo basi,chagua kila siku kuwa bora na kupata kilicho bora.

4. Amua na chagua.
Amua kuwa na malengo na chagua pia kuwa na aina ya malengo. Unataka kuwa na malengo ya aina gani? Unataka nini katika hii dunia? Majibu ya maswali haya unayo wewe mwenyewe. Hivyo basi, fanya uamuzi wa kuchagua kile unachotaka hapa duniani.

Biashara ni matangazo. Ili biashara yako iwafikie watu wengi na kujulikana unatakiwa kuitangaza.
Na matangazo mazuri ni yale ya ushuhuda yaani unatafuta mtu uliyetatua tatizo lake kupitia huduma au biashara unayofanya/unayotoa.
Toa huduma bora na tangaza biashara yako.

5. Ulimwengu wa sasa wa zama za taarifa na mawasiliano mtu akiwa na kompyuta na intanet basi anauwezo wa kuandika chochote anachojisikia.
Hapa mtu huyu anaweza kuandika kile anachojua na asichokijua.
Hivyo basi, ni vema kuwa makini na taarifa sahihi na kile unachowasilisha kwenye mtandao ili kuepuka kupotosha watu kulingana na kitu unachoweka.

6. Taarifa zinaonesha kuwa watu wengi wanaotoa ushauri au kuandika kwenye tovuti kuhusiana na mambo ya afya wengi si matabibu.
Taarifa nyingi zinazoandikwa katika tovuti mbalimbali kuhusiana na mambo ya afya huwa zinakuwa na upungufu wa taarifa.

7. Makadirio ya tafiti nyingi zinaonesha kuwa idadi ya namba kubwa za matokeo ya vifo zinatokana na ajali za barabarani,majanga ya asili n.k.
Hii inaonesha kuwa ajali za barabarani ndio zinaongoza sana kuchangia idadi ya vifo vingi vinavyotokea.
Ni vema kuwa makini na elimu juu ya usalama barabarani itolewe kwa watu wote wanaotumia vyombo vya moto barabarani.
Mimi na wewe tuwe balozi wazuri katika kufuata kanuni na sheria unapokua barabarani.

8. Njia nzuri ya kuwa bora ni kuwa na ubora.
Ukitaka kuwa bora jaribu kuwa na ubora wali juu.
Usitegemee kuwa bora kama hauna ubora.
Kama unataka kuwa mtu fulani hakikisha kile unachofanya kina ubora.
Ubora ndio utakufanya kuwa bora zaidi.

9. Kuchagua ni uhuru. Tunachagua kuwa na mahitaji mbalimbali katika maisha yetu kama vile, chakula,malazi, nguo na nk.
Maisha ni machaguo hivyo ni vema kuwa huru katika kufanya maamuzi ya kuchagua.
Usitawaliwe katika kufanya maamuzi bali fanya maamuzi yako mwenyewe katika maisha yako.

10. Jinsi tunavyochagua machaguo mbalimbali katika maishe yetu ndiyo yanatueleza sisi ni kina nani hapa duniani.
Kile unachochagua ndicho kiwakilishi chako duniani.
Utajulikana kulingana na chaguo lako la kitu fulani.

11. Faida moja wapo ya kuchagua ni unajiandaa kisaikolojia kuwa unachagua kitu ambacho unakitaka.
Kuchagua ni faida kisaikolojia. Jambo ulilojiandaa nalo kisaikolojia ni rahisi kulishinda mbeleni.

12. Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaoishi katika nchi masikini ndio zinaongoza kwa kukosa furaha duniani.
Na watu wanaoishi katika nchi tajiri huwa wanakuwa na furaha ukilinganisha na wengine. Je nini kinawafanya watu wawe na furaha? Je ni fedha? Au furaha. Ukweli ni kwamba fedha haileti furaha bali
furaha inaleta fedha.

13. Watu waliooa, waliojenga mahusiano mazuri na Mungu, ambao wako karibu na familia zao,waliokuwa na marafiki wazuri nk. Huwa na furaha ukilinganisha na wengine.

14. Watu wenye furaha wanakuwa ni watu wanaosambaza furaha na upendo kwa watu.
Watu wenye furaha huonesha tabasamu zuri kwa watu wengine hivyo basi,furaha hiyo hugeuka kuwa upendo kwa watu wengine. Inaokoa nafsi za watu waliokuwa na huzuni na waliokata tamaa.

15. Ili kuanzisha uhusiano na mtu ni lazima kwanza mm. Mfano kama ni marafiki, watu wanaotaka kuwa wapenzi ili waanzishe uhusiano lazima kwanza wajuane.
Muda ndio utakaokuwa unatumika katika kujenga uhusiano naye. Jinsi unavyompa mwenzako muda ndio unampa nafasi ya kukujua. Hivyo unahitaji muda kuuendeleza uhusiano.

16. Bora kumililki sehemu yako yAko ya kuishi kuliko kuendelea kulipa kodi ya kupangisha.
Kulipa gharama za kupangisha ni sawa na kutupa fedha zako dirishani.
Kuwa mmiliki ni bora zaidi kuliko kuwa kulipa sehemu ya kupangisha.

17. Uwekezaji mzuri ni kumiliki ya kwako. Kuwa mmililiki wa majengo yako kwani utakua unaokoa hela za kwenda kulipia sehemu zingine.
Kama ukiwa mmiliki wa nyumba yako itakusaidia kupunguza gharama na ile hela ambayo unapaswa kulipa itakusaidia kwa mambo mengine.
Kama wewe ni mlaji wa hotelini ili kupunguza gharama kubwa anza kujipikia ili kupunguza gharama.

18. Kujifunza kuchagua ni ngumu. Na kujifunza kuchagua vizuri ni ngumu pia. Na katila dunia hii ya sasa iliyojaa uwezekano usiokuwa na mipaka bado ni ngumu sana kuchagua.
Dunia ina mambo mengi ya kuchagua na ukilinganisha kwa sasa tuko katika zama za taarifa.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101505
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: