Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Madhara Ya Ubinafsi Katika Jamii Yetu Ya Leo

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko salama na unaendelea vizuri na ratiba zako za kila siku.

Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja madhara ya ubinafsi katika maisha yetu.
Kwanza kabisa ubinafsi ni hali ya kujiona wewe ndio unastahili zaidi kuliko mwingine. Hali hii ya ubinafsi imekuwa ikiwatafuna watu wengi katika jamii yetu. Ubinafsi wa kutopenda mwingine apate kama wewe. Au kutopenda watu wengine wafanikiwe kama wewe ulivyofanikiwa.

Ubinafsi hauwezi kujaza dunia kama vile tunavyotaka. Dunia bado ina njaa sana Mimi na wewe tunawajibika kuijaza lakini dunia hatuwezi kuijaza kama tukiendelea kuishi katika falsafa ya umimi. Kama wavumbuzi wote wa mambo wangekuwa wabinafsi basi leo hii hata Mimi na wewe tusingekuwa tunawasiliana kama hivi tunavyowasiliana.

Tabia ya ubinafsi ni umasikini mkubwa sana badala ya kuzalisha maendeleo kwa watu wote unazalisha maendeleo kwa mtu mmoja. Mtu mwenye Tabia ya umimi hapendi kumuona mwenzake awe juu hata siku moja.

Furaha ya watu wabinafsi ni kuona wewe ukianguka badala ya kupanda. Muda mwingine wanafurahi hata pale unapopata matatizo kwani moyo wake unafurahi.

Ubinafsi unaanzia kwa mtu mmoja,kwenye familia mpaka jamii nzima. Watoto wanafundishwa falsafa za umimi tokea wakiwa wadogo. Umimi unawagawa hata ndugu katika familia kwa mfano, watoto wa ndugu X wanapandikizwa chuki dhidi ya ndugu Y. Utasikia sisi familia yetu ni bora kuliko wale kwa sababu sisi tunauwezo wa kifedha na wale hawana uwezo wa kifedha.

Ubinafsi unatafuna koo nyingi katika jamii yetu. Watu wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo kwa pamoja kwa sababu ya ubinafsi wa kujiona yeye ni bora kuliko wengine.

Ubinafsi unajenga matabaka makubwa katika jamii yetu. Kwa sababu ya ubinafsi unapelekea hata watu wengine kujiona wao ni bora kuliko wengine hatimaye kushindwa kushiriki kwa pamoja hata shughuli za kijamii.

Watu wana maarifa mbalimbali lakini hawataki hata kuwasaidia wengine huku wakiendelea kuwa kama bahari mfu yaani dead sea iliyoko pale mashariki na kati.

Mpendwa rafiki, maisha yetu hayawezi kuwa ya maana hapa duniani kama kila mmoja akijiangalia yeye kama yeye. Kama kila mtu akiwa kama bahari mfu ambaye yeye ni kutaka kupokea tu kuliko kutoa.

Kama tukiacha ubinafsi katika maisha yetu tutajenga duniani iliyo bora sana. Tuache ubinafsi tujitoe kwa maisha ya wengine na ya kwetu pia. Tusijiangalie sisi tu bali tuwaangalie na wengine.

Hatua ya kuchukua leo, ubinafsi unasababisha wivu. Na wivu huzaa mauti hivyo anza kuishi maisha yeye maana ya kuwaangalia na wengine siyo kujiangalia wewe tu.
Wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka.
Epuka kupokea tu bila kutoa.

Mwisho, ubinafsi ni alama ya ishara hasi katika dunia. Hatuwezi kuijaza dunia kama kila mtu akiwa mbinafsi kwenye hii dunia. Kila mtu anakitu cha kipekee hapa duniani hivyo kitoe usisubiri kufa nacho. Kila mmoja wetu ameletwa duniani kuja kutumika je wewe dunia inakutumiaje?

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: