Njia Rahisi Ya Kuanza Biashara

Kwa wale ambao hawajui ni biashara gani wafanye, Wale ambao wanataka kuingia kwenye biashara lakini hawajui waanzie wapi, Na hata kwa wale ambao wanataka kuingia kwenye biashara lakini hawana mtaji wa kuanza biashara, Zipo njia mbili za kuingia kwenye biashara na hata kuanza biashara yoyote. Njia ya kwanza ni kununua halafu kuuza, au hata kutengeneza …

Kamwe Usitosheke

Rafiki, Kwenye maisha yako unapaswa kuwa na falsafa ya kamwe usitosheke. Unapoishi msingi wa kamwe usitosheke, utakua unajisukuma zaidi kwenda mbele na kukataa kurudi nyuma. Kamwe usitosheke, itakusaidia wewe kupata mafanikio makubwa na kuepuka kupata mafanikio ya kawaida.Sisi binadamu ni watu wa kuridhika, huwa tunaridhika na kile tunachopata, huwa hatuweki juhudi zaidi ya kwenda mbele. …

Hakuna Maisha Yenye Gharama Kama Haya

Rafiki, Sisi binadamu tunao uwezo wa kuishi kwa kiasi chochote kile cha pesa tunachopata. Akili yetu huwa inatusukuma kununua manunuzi kulingana na fedha tuliyokuwa nayo. Kama tukiwa na elfu tano, tutaishi kadiri ya elfu tano. Na mara nyingi kadiri unavyokuwa na fedha zaidi, ndiyo na matumizi pia yanaongezeka. Hakuna maisha yenye gharama kama maisha ya …

Tuache Utoto

Rafiki, Sisi binadamu ni watu ambao hatupendi kuchukua hatua mpaka tuambiwe tuchukue hatua ndiyo tunachukua. Tumekuwa ni watu wa kusubiri kwanza tuwepe ruhusa ndiyo tuweze kuchukua hatua.Ulivyokuwa mdogo au unasoma shule, ulikuwa unaongozwa na kufanyiwa maamuzi. Tena ulikuwa unaongozwa na kengele. Unajua kabisa, kengele fulani ikipigwa, inaashiria kitu gani. Hii imetuathiri sana katika maisha yetu, …

Jiweke Kitimoto Wewe Mwenyewe

Kuna wakati mwandishi wa kitabu cha How I Raised Myself from Failure to Success in Selling Frank Bettger alikuwa anapitia kipindi kigumu sana cha mauzo duni kwenye biashara yake. Familia yake ilikuwa inahitaji mahitaji mbalimbali na yeye hana hela. Siku moja aliamua kujiweka kitimoto yeye mwenyewe kwa hali ambayo anapitia. Aliwasha gari na kwenda nje …

Msingi Mkuu Wa Maisha

Rafiki yangu nikupendaye, Msingi mkuu wa maisha ya mafanikio ni uadilifu. Unapaswa kuwa na uadilifu usiovunjika wala usiotiliwa shaka kabisa. Uadilifu ni hali ya kutokuwa na rangi mbili, yaani maisha yako ya faraghani na hadharani yasitofautiane. Ukisema unaishi uadilifu, siyo tu kwa nje watu wanakuona hata maisha yako ya siri ambayo watu hawakuoni. Unakuwa na …

Watu Hawajawahi Kuishiwa Kitu Hiki

Rafiki, Usipokee ushauri ambao haujaomba kwa mtu.Na pili, usitoe ushauri ambao haujaombwa kutoa ushauri. Unaweza kuona mtu anahitaji kweli ushauri, lakini kama hajakuomba usimpe ushauri kwa sababu hatoufanyia kazi. Nimeanza kukuambia hivyo kwa sababu watu hawajawahi kuishiwa maoni.Ukimwomba mtu akupe ushauri hakosi huwa hakosi maoni ya kukupa. Watu wako bize kutoa maoni yao juu ya …

Hii Ndiyo Tabia Ya Watu Kama Ulikuwa Huijui

Rafiki, Watu wakiwa na shida watanyenyekea sana ili wapate kile wanachotaka. Watu wakiwa katika mchakato wa kutafuta kitu mwanzoni wanakuwa na utii sana, wanajituma na kufuata misingi yote. Hata katika mahusiano tunaona, watu wakiwa katika uchumba, kila mmoja anapenda kuonekana yuko vizuri mbele ya mwenzake. Lakini pale ambapo kila mmoja anapokuwa ameshapata kile alichokuwa anataka, …

Wewe Ndiye Unayeumia Zaidi

Rafiki, Ni kawaida yetu sisi binadamu kutoelewana na baadhi ya watu ambao tunahusiana nao. Na kamwe hatuwezi kuwa sawa muda wote, kuna wakati hali ya kutoelewana inakuja tu.Kuna mwingine anaweza kukuchukia tu kwa sababu zake mwenyewe. Na huku wewe hata ukiwa hujui kama umemkosea, utashangaa mahusiano yanakuwa hafifu, mtu ambaye mlikuwa katika mahusiano mazuri anaanza …

Design a site like this with WordPress.com
Get started