Design a site like this with WordPress.com
Get started

Uchambuzi Wa Kitabu; Mambo 20 Muhimu Ya Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Warren Buffett Way

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi nzuri sana ya Siku hii ya leo kwani leo ni Siku bora na ya kipekee kwako kwenda kufanya makubwa na kutarajia kupata makubwa.

Rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyokuandalia. Ndugu msomaji leo ninakwenda kukushirikisha mambo muhimu niliyojifunza kutoka katika kitabu cha The Warren Buffett Way. Kitabu hiki kimeandikwa na Robert G. Hagstrom. Karibu sana rafiki na msomaji wangu nikushirikishe uchambuzi huu mzuri wa kitabu hiki hivyo basi, kwa namna ya pekee tusafiri kimawazo hadi pale tamati ya kipindi chetu cha leo.

Uchambuzi Wa Kitabu; THE WARREN BUFFETT WAY Second Edition, kilichoandikwa na mwandishi ROBERT G. HAGSTROM. Na mambo 20 niliyojifunza kupitia kitabu hiki ni kama ifuatavyo;

Mwandishi anaelezea safari ya maisha ya uwekezaji ya mwekezaji na bilionea Warren Buffet. Katika Kitabu hiki kuna mambo mengi mazuri na miongoni ni machache kati ya niliyojifunza;

1. Nuhu hakuanza kujenga safina wakati mvua tayari ilikuwa imenyeesha , hii ni moja ya kauli ya Warren Buffet aliyokuwa akimwambia mwandishi wa Kitabu hiki. Kauli hii inatufundisha kuwa unatakiwa kuwekeza mapema kabla ya majanga hayajakukuta. Usisubiri uzeeke ndiyo uanze kuwekeza bali wekeza mapema ndiyo maana aliutumia msemo huu kuwa nuhuu alijenga safina kabla hata mvua haijanyeesha.

2. Mwandishi anatualika kuwa tutumie kitabu hiki kujifunza yale muhimu lakini kutaka kuwa kama warren Buffett. Hauwezi kuwa warren Buffett na kama ukiiga utaishia kuumia.
Hapa tunajifunza kuwa tumia maarifa utakayopata na mawazo uliyokuwa nayo kufanya uwekezaji. Unaweza kuwa wewe na unakitu ambacho unaweza kufanya tofauti na mtu mwingine hivyo usiige bali kuwa wewe.

3. Historia ya warren Edward Buffett inatuonesha kuwa alizaliwa mwaka 1930 tarehe 30 ya mwezi wa nane katika mji wa ohama katika jimbo la Nebraska huko nchini marekani.
Alikuwa ameanza kujifunza mambo ya uwekezaji kwa kusoma kitabu cha baba yake wakati akiwa na umri wa miaka nane.

4. Historia kupitia kitabu hiki inatuonesha kuwa warren Edward Buffett alianza uwekezaji katika hisa akiwa na miaka kumi na tatu, hii inatuonesha kuwa ni namna gani unapoanza mapema ndiyo unajitengenezea njia nzuri katika uwekezaji. Hapo ulipo hutakiwi kukata tamaa kwa kufanya kitu kwa muda mchache na kutaka mafanikio ya haraka ndani ya muda mfupi, kiukweli siyo kazi rahisi tunahitaji kuweka juhudi za muda mrefu.

5. Buffett anasema mtu ambaye ananunua hisa katika kampuni hivyo anamiliki kampuni kwahiyo, anamjali mteja kwa kuvaa viatu vya wateja wake. Pia, ni mtu anayezalisha ripoti nzuri kwa wateja wake kwa kuwa anaamini kuwa ndiyo wamiliki wa kampuni.
Somo; tukivaa viatu vya wateja wetu basi, tutatatua matatizo mengi kwa wateja.

6. Katika kufanya kazi zake za uwekezaji anawatu makini wanaomwongoza na kumpa elimu. Hata falsafa yake ya uwekezaji ameweza kuipata kwa mwalimu wake Benjamin Graham. Benjamin Graham ndiye moja washauri wake naye ni mwadili wa mambo ya uchambuzi wa fedha katika uwekezaji wake.
Somo; kila kitu kinahitaji watu makini wakukushauri ili upate matokeo ya unayoyataka. Usiogope kulipia gharama kama unahitaji ushauri mzuri kutoka kwa watu makini.

7. Graham anatushirikisha kanuni mbili za uwekezaji nazo ni;
1. Usipoteze na ya pili inasema rejea kanuni namba moja.
Ukiwa katika uwekezaji unapotaka kupoteza katika uwekezaji wa hisa basi rudia kanuni hizo. Hizi kanuni ndiyo zilizompelekea kuwa na motto wake wa margin safety akiwa na maana ya kwamba mstari wa usalama au mstari salama.

8. Ili mwekezaji aweze kufanya maamuzi mazuri kuhusu uwekezaji basi, anaalikwa kujifunza mambo yanayohusiana na uwekezaji.
Biashara ya uwekezaji inahitaji kujifunza sana, unatakiwa kusoma ili uweze kuielewa biashara hii kwa undani Fisher alimshauri Buffett kuwa siyo vizuri kuweka mayai kwenye vikapu vingi kwa sababu itakuwa ni kazi kuangalia mayai yote hayo katika kila kikapu. Hii ni nadharia katika uwekezaji kuliko kuwekeza katika mingi ya hisa ni bora kutafuta mifuko michache na ukaweka nguvu kwenye hiyo na baadae kuja kupata matokeo mazuri.

10. Buffett yeye anasema ni asilimia 15 ya fisher na 85 ni Benjamin Graham.
Somo; maarifa ukiyatumia hayawezi kukuacha kama ulivyo hata siku moja.
Kuwa na wataalamu wanaokushauri ni moja ya njia ya kufanikiwa katika kile unachofanya.

11. Kununua hisa maana yake ni kununua biashara. Hisa ni biashara kama biashara kama biashara nyingine kwa sababu zinahitaji nidhamu ile ile kama ilivyo kwa biashara nyingine unazozijua wewe.

12. Nunua biashara na siyo hisa, tafuta kampuni ambayo unaweza ukaimiliki daima. Kwa mfano, moja ya kampuni ambayo ameichagua buffet katika uwekezaji wake ni coca cola kwa sababu cocacola ni kampuni kubwa iliyoenea karibu duniani kote na imeenea nchi zaidi ya 198.
Hivyo, hii inamfanya aendelee kumiliki kampuni kwa sababu ya kuchagua kampuni bora ya kununua hisa.

14. Njia rahisi ya kumilili kampuni na kuwa mwekezaji na mfanyabiashara basi ni kununua hisa za kampuni husika.
Hisa zako ndiyo zitakuwa sehemu ya umiliki wako katika kampuni. Kumbe basi, hata kama huwezi kufanya biashara nyingine basi hisa ni sehemu sahihi kwa mtu ambaye anataka kuwekeza kwa sababu wewe hausiki katika uendeshaji wa kampuni bali pesa yako ndiyo inakufanyia kazi wakati wewe ukiendelea na mambo mengine.

15. Buffet anapendelea kununua katika kampuni ambayo anaipenda na anaamini atafanikiwa na kupata faida ya muda mrefu.
Hivyo somo kubwa tunalopata hapa ni kuangalia sehemu nzuri ya uwekezaji ambayo utaweza kupata mafanikio lakini pia faida ya muda mrefu.

16. Mwandishi anatumia mfano wa kampuni ya coca cola ambayo imeweza kukaa muda mrefu katika soko yaani ni kampuni imeonesha kuwa king’ang’anizi tangu karni ya kumi na tisa.
Unapochagua kampuni unaweza kuangalia kampuni iliyokuwa na msimamo kwa muda mrefu kama coca cola na imeenea karibu dunia nzima na kwa picha hii inatupa mwelekeo mzuri.

17. Kila kampuni inafanya makosa. Makosa yanaweza kufanyika katika ripoti na mambo mengine.
Ripoti nyingi huwa zinakuwa hazina ubora. Mapungufu yapo kila sehemu hivyo ni vizuri kulijua hilo na kulifanyia kazi.

18. Katika kuwafanyia watu tathimini unaangalia vitu vitatu nazo ni;
Uadilifu, akili na nguvu.
Kama mtu akipoteza tu uadilifu basi amepoteza yote. Kwahiyo, hivyo ni vitu vya msingi vya kuangalia ubora wa kumtathimini mtu.

19. Kadiri ya warren buffett anasema bei ni kile unacholipia na na thamani ni kile unachopata.
Unalipa kiasi fulani ili uweze kupata thamani ya kile kitu unachotaka. Na bei huashiria thamani ya kitu unachotegeme kupata.

20. Unapotaka kuwekeza katika kampuni usiangalie bei bali angalia matokeo ya kampuni unayotaka kufanya nayo biashara. Hapa kwa lugha rahisi ni kwamba usiangalie bei ya kitu angalia thamani ya kitu unachopata baada ya kulipia. Usiangalie bei bali angalia thamani.

Nakutakia kila la heri yangu na fanyia kazi haya uliyojifunza. Kupata vitabu vingine vya kujisome kwa lugha ya kiswahili tafadhali wasiliana nasi kupitia namba 0717101505/0767101504.

Ni mimi Rafiki na Mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: