Kiburi Cha Mafanikio

Watu wengi wakifanikiwa huwa wanakuwa na kiburi cha mafanikio na kusahau mchango wa bahati kwenye mafanikio yao. Tambua mchango wa bahati. Ukiwa mnyenyekevu na kutambua mchango wa bahati, kiburi cha mafanikio hakitakuangusha. Mafanikio huwa yanadanganya sana na ndiyo maana wengi huanguka vibaya baada ya kufanikiwa. Hiyo inatokana na kiburi ambacho watu wanakipata wanapofanikiwa, kwa kuona …

Pata Ushindi Ndiyo Uamini

Rafiki, Usiamini kitu kwa sababu tu kila mtu anakiamini, pata ushahidi ndiyo uamini.Siyo kila kitu ambacho watu wengi wanakiamini ndiyo sahihi. Kuwa mtu wa kuthibitisha wewe mwenyewe na siyo kutegemea watu wengi. Ishi kwa falsafa hii, amini lakini, thibitisha. Kuthibitisha ndiyo kupata ushindi. Kama inafanya kazi au haifanyi utajua kwa kuthibitisha. Waache watu waamini vile …

Kukubali Majukumu Yako

Rafiki, Kuna watu wa aina mbili hapa duniani, wapo watu ambao wanayakubali majukumu yao na kuchukua hatua. Na wapo watu ambao wanayakataa kabisa majukumu yao na kutafuta sababu kwa nini hawawezi kuchukua hatua.Kumbuka, ni rahisi kukimbia majukumu yako lakini ni ngumu kukimbia matokeo yake. Mafanikio hayajawahi kwenda kwa mtu yeyote ambaye siyo wa kukubali majukumu. …

Kuwa Imara Zaidi

Rafiki, Pale yasiyotegemewa yanapotokea kwa watu, huwa wengine wanavurugwa kabisa au wengine wanaimarika kabisa. Mambo usiyoyategemea yakitokea, yanakuwa yanawaacha watu katika matokeo haya matatu. Moja, kuvunjika moyo na kukata tamaa kabisa. Hapa mtu anaanguka kabisa kiasi cha kushindwa kurudi tena kwenye mapambano. Mbili, ni kuwa mstahimilivu. Hapa mtu anarudi tena kwenye mapambano licha ya kuwa …

Namna Nzuri Ya Kumkosoa Mtu

Rafiki, Huwa tuna tabia fulani ya kukosoa kwenye maisha yetu. Wako watu ambao huwa hawaoni mazuri ya mtu hata siku moja. Hata mtu akifanya kitu, hata kiwe kizuri yeye ataona upande hasi.Katika falsafa ya Ustoa tumejifunza kwamba, kiasili kila kitu kipo sawa, hakuna kitu kizuri wala kibaya bali mtazamo wetu ndiyo unapelekea kitu kuonekana kizuri …

Watu Wananunua Kwa Sababu Hii Hapa

Rafiki, Kwenye mauzo, watu wananunua kwa sababu zao binafsi na siyo kwa sababu ya kukuonea wewe huruma kwenye kile unachouza. Huwezi kumkuta mtu amekaa zake, na kumwambia naomba ununue kwa sababu nataka nipate hela ya kumlipia mtoto ada.Watu wanapokuwa na mahitaji yao ndiyo yanawasukuma kununua. Watu hawanunui kwa sababu ya bei, wananunua kwa sababu ya …

Chagua Kimoja Kati Ya Hivi

Kwenye haya maisha ni bora uchague kimoja, upambane ushinde kweli au usipambane kwa uhakika uteseke kweli. Maandiko ya kiimani yanasema, ni heri kuwa moto au kuwa baridi lakini usiwe vuguvugu, maana kuwa vuguvugu ni kubaya kuliko hata kuwa baridi. Hata kwenye mafanikio pia, ni heri uweke juhudi zako zote kabisa na ufanikiwe kwa uhakika au …

Mauzo Ndiyo Njia Ya Maisha

Rafiki, Mauzo ndiyo njia ya maisha, mauzo ni hitaji muhimu la maisha, ili ule lazima uuze, na lazima pia watu wakuuzie kitu.Huwezi kukwepa mauzo kwenye maisha yako. Kila mtu anauziwa na anauza. Yaani UZA au utauziwa. Kama uko hai basi kuna kitu unauza, hakuna mtu ambaye anaendesha maisha yake bila kuuza. Kama kuna kitu kimoja …

Njia Rahisi Ya Kukuza Kipato Chako

Rafiki, Mtu ambaye ameondoka hapa duniani miaka 2 iliyopita, akifufuka leo atakutana na mabadiliko makubwa sana.Mabadiliko yanatokea kwa kasi sana, kama mabadiliko yanatokea na sisi pia tunapaswa kubadilika ili kunufaika na mabadiliko yanatokea. Na kuwa mbele kwa mabadiliko yanatokea ndiyo fursa kubwa lakini ukiwa nyuma ya mabadiliko inakuwa hasara. Gharama za maisha zimekuwa juu ni …

Ukiwa Na Maandalizi Lazima Utakutana Na Bahati

Rafiki yangu nikupendaye, Sisi binadamu ni miongoni mwa viumbe ambavyo tumebarikiwa sana. Hongera sana kwa kustahilishwa na kuwa na baraka hizo. Kila mmoja wetu tayari ana baraka ndani yake. Yaani kitendo tu cha mimba yako kutungwa, tayari una baraka. Maana rahisi ya baraka ni nguvu ya asili ya kutenda miujiza ambayo ipo kwa kila mmoja …

Design a site like this with WordPress.com
Get started