Kama Unataka Kufanikiwa, Penda Kitu Hiki Hapa

Rafiki yangu nikupendaye, Huhitaji kufanya kile ambacho unakipenda ndiyo ufanikiwe, bali unahitaji kupenda kile unachofanya sasa. Watu wengi wamekuwa wakijidanganya kwamba pale walipo sasa hawapapendi na hivyo kutoweka juhudi kubwa, mwishowe wanajikuta wamenasa pale pale, iwe ni kazi au biashara. Siri ni hii rafiki, anza kupenda hapo ulipo sasa, anza kuweka juhudi zako zote kwenye …

Mambo 11 Ya Kujifunza Kuhusu Kazi Kutoka Kwa Albert Hubbard Kwenda Kwa Mwajiriwa na Mwajiri

Albert Hubbard alikuwa ni mwandishi wa insha ya ujumbe kwenda Garcia. Na katika Isha yake hiyo, kuna mambo muhimu sana ya kujifunza kutoka kwake. Kama unamfanyia mtu, mfanyie kazi kweli. Kama anakulipa mshahara unaoweza kukukupatia mkate na siagi, mfanyie kazi. Mwongelee vizuri, fikiria mazuri kuhusu yeye, simama upande wake na tetea taasisi yake. Nadhani kama …

Nia Yako Itakupa Kile Unachotaka

Waswahili wanasema, penye nia pana njia. Ukiamua kuwa vile unavyotaka kuwa unakuwa kwa sababu nia yako ndiyo inaamua wewe uwe nani. Nia yako ya kutaka kitu, itakusukuma kupata hicho kitu. Mtu mwenye nia huwa hashindwi kitu. Je, una nia ya kupata nini? Kama una nia ya kitu fulani, ifanyie kazi nia yako na utaweza kuona …

Hakikisha Unakuwa Navyo Vyote

Rafiki, Uko msemo unaosema kwamba, haijalishi unajua nini, bali unamjua nani. Ni msemo wa kweli kabisa. Sina uhakika kama itakufaa lakini ninakushauri kuwa na vyote. Hakikisha unajua sana, yaani unabobea kwenye kitu fulani.Ubora wako utakukutanisha na koneksheni mbalimbali. Kama ukitegemea kupata dili halafu hujui, siyo muda mrefu utapoteza dili ulilopewa. Watu wanaokujua na kukupa koneksheni …

Huyu Ndiyo Mtu Anayekuchelewesha

Kuna familia, jamii, taasisi na maeneo mengi yanashindwa kupiga hatua kwa sababu moja tu. Na sababu hiyo ni kukosa mtu wa kufanya maamuzi. Watu wengi hawaendi mbele au hawarudi nyuma kwa sababu ya kufanya maamuzi. Maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanaamuliwa na maamuzi anayofanya mtu na hatua anazochukua. Watu wanaogopa kufanya maamuzi, kitu kinachopelekea watu …

Hujachelewa Bado

Pale tunapokuwa tumejua kitu kwa mara ya kwanza, huwa tunajihisi kama tumechelewa vile. Tunakuwa tunajilaumu kabisa nilikuwa wapi, ningekuwa nimejua haya mapema ningekuwa mbali. Katika hali ya kawaida unaweza kuona umechelewa. Lakini hujachelewa. Kwa sababu kwa sasa ndiyo muda wako mzuri wa kufanya kile ambacho umejua sasa. Wanasema miaka 20 iliyopita ndiyo ulikuwa muda mzuri …

Kile Kinachokupa Amani Kinalipa Bili ?

Watu wengi wanapenda kufanya kile wanachopenda. Na ni kweli kabisa, mtu anayefanya kazi anayoipenda huwa haoni kama ni kazi tena. Kama unataka kupata amani basi fanya kazi unayoipenda. Je, kama kwa sasa kile unachokipenda kufanya na hakikupatii fedha za kulipa bili unafanyaje? Jibu ni fanya kile usichopenda ili upate mahitaji.Pale unapopata pesa, na unajiweza kiuchumi …

Tatizo Ni Wewe

Huwa tunaajiri watu wa kutusaidia majukumu yetu. Kwa sababu peke yetu hatuwezi kufanya kila kitu.Umoja ni nguvu. Na kidole kimoja hakivunji chanya. Huwezi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako, kama unafanya kila kitu wewe. Lazima upate watu wa kukusaidia. Hata kama unajitegemea kiasi gani, kumbuka kujitegemea siyo kujitosheleza. Unapoajiri mtu, anakuwa hajui nini unataka wewe …

Kila Maamuzi Unayofanya Yana Vitu Hivi Viwili

Rafiki, Uko hapo ulipo kwa sababu mbili,Moja kwa maamuzi ambayo uliwahi kufanya huko nyumaNa mbili ni kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi ambayo yamepelekea leo kuwa na maisha ambayo unayo sasa. Kwa kila maamuzi utakayofanya, jua kuna maumivu ndani yake. Hivyo basi, mara zote fanya maamuzi ambayo utakuwa tayari kuvumilia maumivu yake. Kila maamuzi unayofanya, …

Hakuna Kazi Ngumu Kama Hii

Waswahili wanasema ukiona vya elea, ujue vimeundwa.Matunda mazuri ambayo unayaona kwa mtu jua kuna kazi kubwa nyuma yake imefanyika. Ukiona mtoto wako anafanya vizuri katika masomo yake, jua kuna kazi ambayo imefanyika kwa wazazi wenyewe au walimu shuleni. Na kazi hiyo ni ufuatiliaji endelevu. Matokeo ya kitu chochote kile, hakiji mara moja, bali yanahitaji ufuatiliaji …

Design a site like this with WordPress.com
Get started