Kila siku tunakutana na watu wapya—katika kazi, biashara, safari, hata mitaani. Wengi huwa tunawapima juu juu: mavazi yao, kazi wanazofanya, au maneno yao ya kwanza. Lakini ukweli ni huu: huwezi kujua nani yuko mbele yako. Ndiyo maana ni hekima kubwa kumchukulia kila mtu kwa adabu, heshima, na uaminifu. Yule mtu unayemdharau kwa sababu anaonekana hana …
Siri Kuu ya Kufanya Makubwa
Kila mtu ana ndoto kubwa moyoni mwake. Wengine wanataka kuanzisha biashara kubwa, wengine kutengeneza mali ya kudumu, na wengine kubadilisha maisha ya jamii zao. Lakini siri kubwa ya kufanikisha hayo yote siyo kusubiri kesho, siyo kuanza pale kila kitu kitakapokuwa sawa, bali kuanza sasa – kidogo ulipo, na kwa kile ulicho nacho. Ukikaa ukifikiria ukomo, …
Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Nne
Katika sehemu zilizopita tuliona mitazamo mitatu inayoweza kukuzuia kupata fedha na utajiri mkubwa: Uhaba – kuamini fedha ni chache na lazima uzifiche. Kufa na kupona – kuamini ukizikosa fedha ni mwisho wa maisha. Ushindani – kuamini mafanikio yako lazima yatokane na kushindwa kwa wengine. Leo tunakamilisha kwa Sehemu ya Nne: mtazamo wa kuchukua. Mtazamo wa …
Continue reading "Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Nne"
Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Tatu
Katika sehemu ya kwanza tulizungumzia kuhusu uhaba na namna ya kuubadili kuwa utele. Kisha kwenye sehemu ya pili tuliona mtazamo wa kufa na kupona na namna ya kuubadili kuwa mtazamo wa mchezo na utulivu.Leo tunaendelea na Sehemu ya Tatu: ushindani. Mtazamo wa Ushindani Wengi wamefundishwa kuamini kwamba ili wao washinde, basi wengine lazima washindwe. Huu …
Continue reading "Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Tatu"
Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Pili
Katika sehemu ya kwanza tulianza na mtazamo wa uhaba na jinsi wa kubadilisha kwa mtazamo wa utele. Leo tunaendelea na Sehemu ya Pili — mtazamo unaoendelea kuwakwamisha wengi kifedha: kufa na kupona. Mtazamo wa "Kufa na Kupona " Wengi wanaona fedha kama kitu cha kufa au kupona — kama ukipoteza, maisha yamekamilika. Wazo hili linajenga …
Continue reading "Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Pili"
Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Kwanza
Kila mtu anatamani kuwa na fedha nyingi na maisha bora. Lakini mara nyingi tatizo si fedha yenyewe, bali mtazamo wetu kuhusu fedha. Kuna mitazamo minne ambayo lazima uibadili kabisa kama kweli unataka kufanikisha safari yako ya kifedha. Mtazamo wa Uhaba Wengi huamini fedha ni haba. Wanafikiri njia pekee ya kuendelea nazo ni kuzificha na kuzikumbatia.Matokeo …
Continue reading "Mitazamo 4 ya Kubadili ili Kupata Fedha na Utajiri Mkubwa – Sehemu ya Kwanza"
Maana Halisi ya Aibu
Robin Sharma aliwahi kushirikisha mstari alioupokea kwa nguvu kubwa kutoka kwenye kitabu Meditations cha Marcus Aurelius. Anasema: "Aibu: roho kukata tamaa wakati mwili bado una nguvu ." Ukikaa na kuutafakari huu mstari, unagundua mara ngapi tumewahi kujiwekea aibu sisi wenyewe. Mara ngapi umekata tamaa haraka ilhali bado ulikuwa na uwezo, nguvu, na nafasi ya kusonga …
Mbinu ya Kujijengea Kujiamini
Huwezi kufika kwenye mafanikio makubwa kama hujiamini. Kujiamini ni nguzo ya kila mafanikio, kwa sababu bila kujiamini hata fursa kubwa ikikujia, utaiona ni kubwa sana kuliko uwezo wako. Lakini kujiamini hakujengwi kwa maneno matupu. Kujiamini kunajengwa kwa vitendo na hatua za kila siku. Anza kwa kujitambua Jiulize: Nataka kuwa mtu wa aina gani? Ukishajua jibu, …
Tafuta Furaha, Shida Huwa Zinakuja Zenyewe
Kuna ukweli mmoja wa maisha ambao kila mmoja wetu anaouona kila siku: shida huwa hazihitaji mwaliko. Hazihitaji ratiba, wala mipango. Zenyewe hujitokeza—mara nyingine kwa ghafla, mara nyingine kwa taratibu—lakini bila shaka huja. Lakini furaha siyo kitu kinachokuja yenyewe. Furaha ni kitu kinachohitaji kutafutwa, kutengenezwa na kulindwa. Watu wengi hukaa wakisubiri mazingira yabadilike ndipo wawe na …
Continue reading "Tafuta Furaha, Shida Huwa Zinakuja Zenyewe"
Huwezi Kushinda Kama Haujajaribu
Mara kwa mara tumekuwa tukipata mawazo mazuri sana—mawazo yenye uwezo wa kubadilisha maisha yetu, kazi zetu na hata biashara zetu. Wakati mwingine ni wazo dogo la kuboresha kazi ya kila siku, na mara nyingine ni ndoto kubwa ya kuinua biashara au huduma kwa kiwango cha juu kabisa. Lakini mara nyingi, kadiri tunavyoendelea kuyatafakari mawazo hayo, …