Faida Kubwa Ya Kukutana Na Mtu Chanya

Mpendwa rafiki, Ili uweze kufanikiwa unatakiwa kuangalia sana marafiki waliokuzunguka,watu waliokuzunguka wana mchango mkubwa sana kwetu sisi ili tuweze kufanikiwa. Tunaalikwa kuchangamana na watu wanaoendana na ndoto zetu kwa lugha rahisi tuambatane na watu ambao tayari wameshakuwa kile ambacho sisi tunataka kuwa. Kila siku angalia watu ambao unakutana nao na unaotumia muda mwingi kukaa nao, …

Hii Ndiyo Kinga Bora Dhidi Ya Mwili Wako

Aliyekuwa mtawala wa ufarasa, mbabe wa kivita na jemedari jeshi Napoleon Bonaparte aliwahi kusema kufa siyo kitu lakini kuishi kushindwa ,kupigwa na kutokuwa na neema ni kufa kila siku. Wengi wetu wanakufa kila siku kwa kupigwa au kushindwa kila siku na hali ya kutokuwa na shukrani. Tuna vifo vya watu wengi sana ambao kila siku …

Huyu Ndiye Muuzaji wa Kumuogopa

Mpendwa rafiki, Maisha yetu kiujumla ni kuuza na mauzo ndiyo yanafanya maisha yetu yaende kwa sababu kupitia mauzo tunapata kile tunachokitaka. Mauzo ndiyo yanalipa kila kitu katika maisha yetu, kama huna kitu unachouza maana yake huna thamani unayoitoa na kama huna thamani unayoitoa utawezaje kupata fedha? Kwa sababu fedha ni mbadilishano wa thamani yaani lazima …

Bora Kusema Ukweli Kwa Kitu Hiki Kuliko Kujiharibia Sifa Zako

Mpendwa rafiki yangu, Dunia ya leo kuna watu ambao wanajua kufanya kila kitu hata kama kitu hawawezi watakuambia wanajua kufanya, huwezi kuwa bora kwenye kila kitu bali unaweza kuwa bora sehemu moja tu ambayo umechagua kuwa. Mtu ambaye kila sehemu anagusa gusa na kuacha ni wazi bado mtu hajajitambua anafanya nini hapa duniani. Hakuna kitu …

Kujua Mema Ni Kutenda Mema

Mpendwa rafiki, Kila mmoja wetu anajua mema, hivyo kama unajua mema je unayatenda mema kweli? Ulishawahi hata kusema leo acha iwe ni siku yangu ya kutenda mema? Mwanafalsafa wa kigiriki Socrates aliwahi kusema, kujua mema ni kutenda mema je wewe unajua mema na unayatenda? Kila mmoja wetu leo ajue mema na ayatende mema kama inavyotakiwa. …

Kwanini Kila Mtu Anapaswa Kunywa Maji Ya Kisima Chake Mwenyewe Katika Maisha Ya Ndoa

Mpendwa rafiki yangu, Maisha ya ndoa yana dai uaminifu, maisha ya ndoa yakikosa uaminifu yanakuwa hayana maana na kukosa ladha. Wote tunajua kuwa chakula kikikosa chumvi kinakuwa hakina ladha vivyo hivyo katika maisha ya ndoa.  Uaminifu unatakiwa kujengewa ukuta, je ukuta huo unatakiwa kujengewa wapi? Ukuta wa uaminifu unajengewa moyoni. Mwanaume au mwanamke hawezi kumzua …

Kabla Hujalala Leo Hakikisha Unafanya Kitu Hiki Muhimu Kwako

Mpendwa rafiki, Huwa tunafanya mengi ndani ya siku na huwa tunachoka na mwili ukichoka dawa yake ni kupumzika hivyo tunapolala tunakuwa tunaupa mwili nafasi ya kupumzika na kukusanya nguvu mpya za kwenda kufanya kazi tena siku inayofuata. Kimsingi huwa tuna aina mbili za akili ambazo ni; conscious mind na subconscious mind. Akili ambayo inafanya kazi …

Kama Unataka Kujua Kama Kuna Watu Wanakufuatilia Katika Maisha Yako Fanya Kitu Hiki

Mpendwa rafiki, Ukitaka kuwajua watu vizuri katika maisha yako basi pata tatizo au mataizo. Kwenye matatizo ndiyo sehemu ambayo itakuonesha una watu wa namna gani nyuma, kama una ndugu, rafiki, jirani au jamaa. Kumbe basi, muda mwingine, changamoto zinatokea iki ziweze kutushepu na kuwa watu bora kama vile vyombo tunavyopikia vikichafuka huwa tunavisugua tena na …

Jifunze Kukomboa Kitu Hiki Muhimu Kwako

Mpendwa rafiki, Ukitembea hata ukiwauliza watu watakuambia siku hizi wako bize sana. Na kweli ukiwaona watu wako bize je uko bize kwa vitu gani? Kuna wengine wako bize lakini bize ya kutozalisha kitu. Wengi tunafurahia kusema tuko bize lakini siyo kuzalisha matokeo yenye tija na ufanisi wa hali ya juu. Tunafanya ili tumalize kazi lakini …

Huu Ndiyo Muda Mzuri Wa Kuuza na Kununua Katika Uwekezaji

Kila mtu anapenda kunufaika na uwekezaji anaofanya au kwa lugha rahisi ni kwamba kila mtu anapenda kupata faida katika kile anachofanya. Maisha ni mchezo na ili uelewe mchezo na kuushinda unapaswa kujua kanuni za mchezo. Vivyo hivyo katika kazi, biashara na uwekezaji lazima ujue kanuni ili uweze kushinda. Muda mzuri wa kununua ni pale ambako …

Design a site like this with WordPress.com
Get started