Hapa Ndiyo Mahali Ambapo Dunia Inazaliwa

Kila mmoja wetu hapa duniani amezaliwa katika familia. Ni mpango wa Mungu kila mwanadamu kuzaliwa katika familia.Na kupitia familia ndiyo mahali dunia inapozaliwa. Kupitia familia zetu, tunajipatia miito mbalimbali duniani. Familia ndiyo nyumba ya dunia ambayo kila mmoja wetu anaishi na kujifunza misingi ya dunia. Familia zetu zikiwa takatifu zinafananishwa na mbingu ndogo hapa duniani. …

Nimewashinda Maadui Zangu Kwa Kuwafanya Kuwa Marafiki Zangu

Dalai Lama enzi za uhai wake aliwahi kusema kuwa nimewashinda maadui zangu kwa kuwafanya kuwa marafiki zangu. Hii ni kauli yenye nguvu sana katika mambo ya msamaha. Moja ya mbinu nzuri ya kuwavuta maadui zetu ni kuwafanya kuwa marafiki zetu kwa njia hii tunakuwa tunawamaliza bila kutumia nguvu. Hatuwezi kumaliza chuki kwa chuki bali tunaweza …

Kuanza Upya Siyo Ujinga

Hutakiwi kujilaumu pale mambo yanapokuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Kwa lolote tunalofanya , basi chochote kinaweza kutokea. Hakuna mkataba kuwa kila tunalofanya basi mambo yataenda kama vile tunavyotaka sisi. Huko ni kujidanganya kweli, Mambo yanaenda vile yanavyotaka yenyewe. Unapo,pokea na kupoteza shukuru na jifunze tena. Na ikibadi anza upya kwani kuanza upya siyo ujinga. Huenda ulipanga …

Kuwa Kiherehere Wa Maisha Yako

Kama kila mtu angekuwa kiherehere wa maisha yake, basi mambo yangekuwa mazuri kweli. Watu wengi siyo vinara wa kufuatilia mambo yao binafsi bali watu ni vinara kwa kufuatilia maisha ya watu wengine. Tunatumia muda na gharama kubwa katika kufuatilia mambo ya watu wengine huku ya kwetu tukiyaacha bila kuyafanyia kazi. Kabla hujaanza zoezi la kumfuatilia …

Hiki Ndiyo Kitu Cha Uhakika Katika Biashara

Mara nyingi tunapoanza kufanya kitu tunakuwa na mategemeo fulani. Kama ni kufanya biashara huwa tunategemea kupata faida. Ni kawaida ya watu wengi kujiandaa na kuwa na mategemeo ya kupata faida kwenye kile wanachofanya. Ni kweli faida ni ushindi tunaopata baada ya kufanikiwa katika kile tunachofanya. Lakini kitu cha uhakika kabisa katika biashara ni changamoto. Kama …

Hii Ndiyo Njia Ya uhakika Ya Kipato

Kipato ni kile ambacho mtu analipwa baada ya kutoa thamani fulani. Iko njia moja inayopendwa na watu wengi ya kuingiza kipato ambayo ni njia ya moja kwa moja yaani active income. Kwa mfano, ajira au mtu aliyejiajiri ambaye asipokuwepo kazini moja kwa moja hakuna kipato kitakachoingia. Njia hii inapendwa na wengi na wengi ndiyo wako …

Mambo Mawili Ambayo Yanakukwamisha Kwenye Maisha Yako

Kama unaweka juhudi kila siku halafu hupati kile unachotaka basi ziko sehemu mbili zinazokukwamisha na leo ndiyo siku pekee ya kuzijua sehemu hizo. Kama umekwama kuna vitu viwili vinavyokuwa vimekukwamisha navyo ni ; Moja ni kile unachojua au kutokujua. Huenda kile unachojua hujakifanya inavyotakiwa ndiyo maana umekwama au unapata matokeo hasi labda kwa sababu ya …

Mtu Anayepaswa Kulaumiwa Kwenye Matatizo Yako Ya Kifedha

Siku zote huwa nina amini kuwa matatizo yote ambayo mtu anayo mtu mwenye ndiyo anaweza kuyamaliza lakini siyo mtu mwingine. Mpaka mhusika mwenyewe aamue, hata katika mafanikio yoyote yale lazima mhusika aamue kile anachotaka kwanza kwani kanuni ya kwanza ya mafanikio ni kujua haswa kile unachotaka ndiyo utaweza kufanikiwa. Katika suala la fedha pia,tunaamini kuwa …

Haya Ndiyo Mambo Mawili Ambayo Huwezi Kuyarudisha

Sijawahi kusikia mtu analalamika kuwa bubu yaani mtu ambaye haongei amegombana naye kwa sababu amemwambia moja mbili tatu. Lakini sisi ambao tumepewa midomo inayotoa sauti ndiyo tumekuwa shida sana. Ukiwa mtu wa kukaa kimya na kufunga mdomo wako utaweza kujiepusha na mengi kwani karibu matatizo mengi tunayokutana nayo kwenye mahusiano yetu chanzo chake ni kauli. …

Ni Sisi Binadamu Pekee Ambao Tuna Sifa Hii…

Sisi binadamu tumekuwa ni watu tunaotengeneza picha ya vitu ambavyo hata havipo muda mwingine katika uhalisia. Tunaipa akili picha ambayo inakuja kututesa hapo baadaye.Mara nyingi mambo yote tunayohofia mchezo mzima unatengenezwa kwenye akili. Wanyama wengine wote wanaendesha maisha yao kwa hisia tangu wanazaliwa lakini sisi binadamu tumepewa uwezo wa kufikiri na kubadili mazingira yetu. Uwezo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started