Vitu vingi au mambo mengi unayoahirisha kufanya ni kwa sababu siyo muhimu kwako. Hakuna mtu ambaye ni makini anaweza kuthubutu kuahirisha kitu ambacho ni muhimu kwake. Anajua akiahirisha hawezi kupata kile anachotaka. Kwa mfano, unaanzaje kuahirisha kwenda kazini? Ni ngumu kwa sababu unajua kupitia kazi unapata kile unachotaka. Vitu vingi ambavyo huwa unavipotezea vinakuwa siyo …
Usiyanyamazie Mambo Muhimu
Unapoona jambo haliko sawa na ni la muhimu basi, usilinyamazie. Yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako usiyanyamazie kabisa. Lakini kama kitu kipo nje ya uwezo wako wala usijisumbue nacho. Hapa ninataka upambane na yale tu yanayokuhusu na ambayo hayakuhusu waachie wale ambao yanawahusu. Usiyanyamazie mambo muhimu kwa sababu, maisha yetu yanaanza kufikia mwisho …
Vitu Vitatu Vinavyokukwamisha Kupata Kile Unachotaka
Sisi binadamu ni watu wazuri sana wa kutafuta sababu. Tukiona kitu hatuwezi kukosa maoni juu ya kile kitu. Ni rahisi kutafuta sababu kwanini asifanye kuliko kwa nini afanye. Moja ya vitu vinavyowasababisha watu kutokamilisha mambo yao mengi ni hivi hapa vifuatavyo; Moja ni uzembe. Watu wanashindwa kuzalisha matokeo mazuri siyo kwamba hawajui ni kwa sababu …
Continue reading "Vitu Vitatu Vinavyokukwamisha Kupata Kile Unachotaka"
Haya Ndiyo Mambo Muhimu Ya Kufikiria Kama Unataka Kupata Fedha Zaidi
Ni nani ambaye hapendi kupata fedha zaidi?Hakuna, wote tunapenda kupata fedha zaidi kwani inatusaidia kuendesha maisha yetu ya kila siku hii ni pamoja na kulipa bili mbalimbali. Iko njia rahisi ya kuweza kuzivuta fedha na zikaja kwenye maisha yako. Fuata yafuatayo ile uweze kuvuta fedha na zije kwako. Moja, acha kufikiria yale usiyotaka kwenye upande …
Continue reading "Haya Ndiyo Mambo Muhimu Ya Kufikiria Kama Unataka Kupata Fedha Zaidi"
Nitawezaje Kufanya?
Imani ina nguvu ya kukuwezesha wewe kuchukua hatua. Kuna mahali inafikia unajiuliza je, nitawezaje kufanya? Unawezaje kufanya? Ni pale tu wewe unapoweza kukiri imani yako unaweza na kujiaminisha kuwa unaweza bila wasiwasi. Kuamini inawezekana ni jambo zuri sana katika maisha yako. Nitawezaje kufanya inakusaidia kufikiria njia za kuweza kufanikiwa kile unachotaka kufanya. Lakini pale unaposema, …
Mbinu Itakayokusaidia Kuongeza Mauzo
Naomba nianze na kukuuliza swali, je, watu wanajua kile unachofanya? Kile unachouza? Huenda ukawa na bidhaa nzuri sana lakini kama wateja husika hawajui kuhusu wewe ni kazi bure. Wanasema biashara ni matangazo, ili watu waje kununua kwako na wasiende sehemu nyingine hakikisha unaweka kazi ya kutosha kuhakikisha watu wanajua kile unachofanya. Fanya masoko ya kutosha …
Hakuna Malipo Kwenye Hili
Leo nataka uondoke na kitu kimoja muhimu na uende ukafanyie kazi. Kwamba hakuna malipo kwenye wasiwasi. Kumbe basi, tunaweza kusema wasiwasi hauna malipo badala ya kuendelea kuwa na hofu na wasiwasi ishi maisha yako. Hofu na wasiwasi ndiyo unaua zaidi kuliko unavyofikiria. Wasiwasi haukusaidii kutatua tatizo. Bali chukua hatua sahihi juu ya kitu kinachokupa wasiwasi. …
Huwezi Kupumua Kwa Kutumia Pua Ya Mtu Mwingine
Ni methali ya Vietnam. Kwani ni uongo? Unaweza kupumua kwa kutumia pua ya mtu mwingine? Hapana haiwezekani. Hapa nataka kukuonesha ni kwa jinsi gani ilivyo shida mtu kufanikiwa kwa kuwa tegemezi. Kusubiria wengine wawajibike halafu wewe maisha yako yaende vizuri. Yaani mtu x akipumua kwa pua yake na wewe unapumua. Hii ni sawa na kusema …
Continue reading "Huwezi Kupumua Kwa Kutumia Pua Ya Mtu Mwingine"
Anza Kuona Thamani Yake Mapema Kabla Hajaondoka
Ni kawaida ya sisi binadamu kuchukulia poa vile tulivyonavyo. Huwa hatuangalii faida tunayoipata kwa vile ambavyo tunavyo na kuona umuhimu wake na kuvithamini. Ni mpaka pale tutakapovipoteza ndiyo tunaona umuhimu wake. Jifunze kuthamini wale ambao uko nao wanaokusaidia kukamilisha ndoto zako. Mtumie vizuri sana yule anayekusaidia majukumu yako kwenda vizuri maana peke yako huwezi lakini …
Continue reading "Anza Kuona Thamani Yake Mapema Kabla Hajaondoka"
Kazana Na Hiki Tu Mengine Achana Nayo
Kazana na yale unayotaka tu. Na mengine achana nayo. Kwenye maisha unapata kile unachokipigania. Kile ambacho unaweka mawazo, nguvu na muda mwingi. Jitoe kwa kile unachopenda kwenye maisha yako. Kwa sababu kwa chochote kile unachofanya na kukipenda utakifanya vizuri sana. Watu wanaopenda wanachofanya huwa hawafanyi kazi. Kwa sababu wanapenda kile wanachofanya hivyo na anafanya kwa …