Ifahamu Ratiba Ya Washindi Inavyokuwa ( 12/4/2018)

Mpendwa rafiki, Ushindi wa siku yetu unapatikana pale tu mtu anapoamka salama. Kama umeamka salama basi wewe tayari ni mshindi kwa sababu bila kuwa mzima utawezaje kupata ushindi unaotafuta. Kupitia tu kuamka salama tunakwenda kutekeleza yale yote tuliyoyapangilia kuyafanya siku hii ya leo. Lakini wengine ndiyo hivyo tena huwa hawakosi shukurani kulalamika kwao imekuwa ni …

Kitu Cha Kufanya Pale Unapokutana Na Mtu Ambaye Hana Tabasamu

Wakati unatoka nyumbani asubuhi basi utakutana na watu mbalimbali njiani hebu leo katika hao watu kumi waangalie usoni halafu utaniambia ni wangapi wanaonekana wana nyuso za tabasamu na furaha. Wengi utakao kutana nao utawaona wana nyuso za visirani, yaani mtu asubuhi amenuna na sijui sasa anamnunia nani. Utafikiri mtu kalazimishwa kuishi au kuamka asubuhi. Kama …

Tukiwa Na Kitu Hiki Katika Maisha Yetu Tumepata Yote

Tunaweza kufanya kila kitu katika maisha yetu lakini kama tukikikosa kitu hiko kwenye kila eneo la maisha yetu tunakuwa watu waajabu sana.  Ni kitu cha kipekee kinachowatenganisha na wengine , ndiyo kitu pekee kinachotufanya sisi tuonekane ni watu wa aina gani. Huenda ni kweli tunajifunza katika maisha yetu juu ya mambo mbalimbali  lakini kama tumekosa …

Uchambuzi wa kitabu; Philosophy of Happiness( Falsafa Ya Furaha)

Furaha ni kitu muhimu kwetu sote. Kwa mtu binafsi na dunia kwa ujumla wote tunahitaji furaha. Mwandishi Avitus N Leonard anatushirikisha umuhimu wa kuwa na furaha katika maisha yetu. Hiyo ndiyo sababu iliyomsukuma kukaa chini na kuandika kitabu hiki kizuri juu ya falsafa ya furaha. Mwandishi ameandika mengi na nimejifunza mengi na yafuatayo ni machache …

Kama Unataka Mafanikio Basi Usiache Kujenga Urafiki Na Mtu Huyu

Mpendwa rafiki, huwa tunakatishana tamaa kutokana na kuwaambia watu ndoto zetu ambao hawafanani na sisi kimaono na hata kimtazamo kabisa. Ukienda kumuomba ushauri mtu aliyekata tamaa ya maisha sidhani kama utapata tumaini la maisha kutoka kwake. Kuna watu ukienda kuongea nao unajihisi tayari wewe ni mwanamafanikio  lakini kuna wengine ukiongea nao wanakutoa katika hamasa ya …

Tatizo Lolote Huwa Linaanza Na Kitu Hiki

Mpendwa rafiki, Kansa huwa inaanzia sehemu ndogo ya mwili na kuenea mwili mzima kama ukichelewa kuitibu itasambaa mwili mzima. Vivyo hivyo hata kwa matatizo yanayotukabili kila siku, tatizo moja usipolitatua litaendelea kukusumbua kila siku na litakuwa kubwa na kusambaa kama kansa inavyosambaa mwilini. Hata siku moja mti hauwezi kuanguka kwa kukatwa shoka moja bali huwa …

Vitu Viwili Pekee Ambavyo Havifundishwi

Mpendwa rafiki, Kuna mambo ambayo tumeshazoea kufundishwa na muda mwingine kuna kuwa na maeneo mbalimbali ya kutolea elimu kama vile shule au vyuo mbalimbali. sasa licha ya kuwa na sehemu hizo za kufundishia basi kuna vitu viwili ambavyo huwezi kumfundisha mtu. Ndiyo, vitu hivyo huwezi ukaenda kukaa darasani na kusema sasa nimekuja kujifunza na kwanza …

Jaribu Kufanya Kitu Hiki Leo Na Anza Maisha Haya Ambayo Hujawahi Kuishi

Mpendwa rafiki, Heri ya mwezi aprili na pasaka pia. Leo wakristu wote duniani wanasherekea sikukuu ya kufa na kufufuka kwa Bwana wao Yesu Kristu hivyo natumia nafasi hii kuwatakia heri ya sikukuu ya pasaka kwa wote na msherekee kwa amani na utulivu. Mpendwa rafiki , huenda tulikuwa tumekufa kimwili, kiroho na hata kiakili kwanini sasa …

Jinsi Wanandoa Wananvyowekana Uchi Hadharani Na Kuleta Matokeo Hasi Katika Mahusiano Ya Ndoa

Mpendwa rafiki, Hata siku moja mti hauwezi kuangushwa kwa shoka moja. Ukiona mpaka mti unaanguka chini basi ujue umekatwa na shoka zaidi ya mara mbili. Hata katika maisha yetu ya kawaida ukiona mpaka mtu anafikia mahali anakata tamaa juu ya kitu fulani basi ujue kuna sababu nyingi zilizomfanya aamue kukata tamaa. Kwa asili duniani hakuna …

Anayesema Hana Kitu Hiki Ni Muongo

Mpendwa rafiki, Wiki hii nilikuwa najitafakarisha mwenyewe baada ya kusoma makala ya mwandishi mwenzangu Makirita Amani aliyoandika kwamba watu wanakosea sana kujiambia kauli mbaya katika fedha na matokeo yake huwa inawanyima au kuwawekea ukuta wa kutopata fedha zaidi. Kauli ya kusema natafuta fedha imekuwa ikiwanyimwa watu wengi sana kupata fedha. Utawasikia watu wengi tu bwana …

Design a site like this with WordPress.com
Get started