Huyu Ndiye Adui Mbaya Wa Mafanikio Yako Yoyote Yale.

Yuko adui ambaye anatufanya turudi nyuma badala ya kwenda mbele. Ni adui hatari sana kiasi kwamba ukiwa naye katika maisha yako lazima utaanguka tu kama siyo kubaki hapo hapo ulipo. Maisha yetu ni safari na kama tunavyojua safari ina mambo mengi na mwisho wa safari ni pale tutakapokuwa tunavuta pumzi yetu hapa duniani na habari …

Tegemea Fedha Zote Lakini Siyo Hii Hapa

Linapokuja katika suala la fedha, fedha ambayo uko nayo mkononi mwako ndiyo una uhakika nayo. Lakini pesa ambayo haiko mikononi mwako siyo kabisa ya kuitegemea hata siku moja. Huwa tunapanga mipango mingi kwa kutegemea pesa ambazo haziko mikononi mwetu, tunaweka bajeti mbalimbali na muda mwingine tunawaahidi watu wetu wa karibu nitakupatia kiasi fulani cha pesa …

Hata Kama Ni Mtoto Wako Wa Kumzaa Usimfanyie Kitu Hiki

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wote ambao tuko hai sasa hivi hatujawahi kuandika barua ya kuomba kuzaliwa na tena hatujawahi hata kuomba kuzaliwa na wazazi fulani lakini sisi wote tumejikuta tumezaliwa na wazazi ambao tunao sasa. Hakuna zama ambazo zinasumbua katika changamoto za malezi kama hizi, hii ni kwa sababu ya dunia inazidi kukua …

Jinsi Ya Kupata Bahati Katika Maisha Yako

Njia nzuri ya kutaka kupata bahati katika maisha yetu ni kujiandaa tu. Hakuna njia nyingine kwa sababu bahati yoyote inakuja pale inapokutana na maandilizi. Kama ulijiandaa kukabiliana na mabadiliko mapema kabla ya mabdiliko kutokea basi yakija kutokea utajiona mwenye bahati. Watu wanaweza kukushangaa katika maisha yako una bahati kiasi gani kumbe ni maandalizi uliyofanya wewe …

Hakuna Hatari Mbaya Katika Masuala Ya Kifedha Kama Hii Hapa

Hata kama wewe ni mzalishaji mzuri kiasi gani lakini ukikosa kuishi na kufuata misingi ya fedha lazima utashindwa. Tuna watu wazuri wanaopambana kila siku kuhakikisha wanapata kile wanachokitaka lakini tumekuwa na watu ambao wanaishi kinyume na kile wanachokifanya. Hakuna hatari mbaya katika masuala ya kifedha kama kuishi juu ya kipato chako. Hata kama wewe ni …

Jinsi Unavyojikatisha Tamaa Wewe Mwenyewe

Kama tunaishi maisha ya kujilinganisha ni rahisi kujiona maisha yetu kuna kitu yamekosa na ya wengine ndiyo yamekamilika. Kumbe tungejua ya kuwa kila mtu ana maisha mazuri kama akiwa anaishi maisha yake. Pale tunapoanza kujiona sisi hatuna hiki na fulani anacho tunaanza kupoteza ladha ya maisha na kuweka maisha yetu katika thamani ya vitu. Kila …

Jinsi Ya Kumkataa Shetani Na Mambo Yake Yote

Miongoni mwa viumbe waliopendelewa hapa duniani ni bindamu. Binadamu tumepewa nguvu ya kutawala kila kitu katika maisha yetu, sisi ndiyo tuna uwezo hata wa kutawala viumbe vingine. Kuna kitu cha kipekee ambacho kina tutofautisha na wengine ambacho hata viumbe wengine hawana. Licha ya binadamu huyu kupendelewa lakini bado wengine wanaendelea kuishi maisha ya tabu sana …

Usifanye Kosa Hili Katika Fedha Zako

Hakuna utumwa mbaya kama wakufurahisha watu ambao hata hawajali. Watu wengi wamekuwa wakikaza kufurahisha watu ambao hata hawajali. Tumekuwa na maisha ya utumwa ya kutaka kuonekana kwa nje sisi ni watu bora kwa kununua vitu vya gharama ili tuonekane na sisi ni watu tunaokwenda na fasheni. Wengine hata wanadiriki kwenda kukopa ili tu maisha yake …

Ukitaka Kujua Tabia Ya Mtu Mchunguze Kwenye Maeneo Haya Mawili

Haiba ni tabia ya mtu yaani jinsi ulivyo hivyo tabia yako ndiyo haiba yako ilivyo. Ukitaka kujua asili ya mtu ni mtu wa namna gani basi endelea kusoma hapa. Huwezi kujua tabia ya mtu kama hujakaa naye vizuri, unaweza ukawaona watu ni wastarabu sana kwa nje lakini kwa ndani ni watu wakorofi sana. Mara nyingi …

Jinsi Wafanyabiashara Wanavyofukuza Wateja Wao

Hawajakosea wahenga waliposema mteja ni mfalme. Hivi unajua mfalme ni mtu anayetaka kile anachokitaka yeye bila sababu yoyote kwa sababu ni mfalme. Mfalme hajiulizi nitapate kitu fulani ila yeye akitaka kile anachokitaka anakipata ndivyo hivyo ulivyo. Maisha yetu kwa kiasi kikubwa yametawaliwa na biashara, huwezi kupita sehemu na ukakosa kuona watu wakifanya biashara. Biashara zilikuwepo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started