Natumaini maneno haya kazi na sala siyo mara yako ya kwanza kuyasikia, umeshayasikia sana watu mbalimbali wakisema na kuwekea msisitizo. Maana rahisi ya kazi na sala ni kama vile kusema imani na matendo. Imani bila matendo imekufa, kama una imani ya kuwa na kitu fulani basi vizuri sana. Lakini imani uliyonayo unatakiwa kuiweka katika kazi.Usikeshe …
Category Archives: Uncategorized
Je Umejitoa Kafara Katika Kile Ulichochagua kufanya?
Elon musk anasema kuwa kama wewe unafanya kazi sana basi kuna mtu anayefanya kazi zaidi yako. Ukijiona wewe ni bora jua kuna bora zaidi yako. Hapa unatakiwa kujituma sana katika kile unachofanya kwa sababu usipojituma kuna mtu anajituma zaidi yako. Kwa chochote kile unachofanya jua kuna mtu anakwenda hatua ya ziada zaidi yako. Watu hawajajitoa …
Continue reading “Je Umejitoa Kafara Katika Kile Ulichochagua kufanya?”
Wape Watoto Vitu Vyote Lakini Usisahau Kuwapa Kitu Hiki Muhimu Kwao
Rafiki yangu, Kila mmoja alikuwa mtoto na huenda hukufundishwa vitu vingi na wazazi wako katika maisha yako lakini vitu vingi dunia imekufundisha. Usipofundishwa na wazazi dunia inakufundisha. Wazazi wetu ni watu muhimu sana duniani tunapaswa kuwashukuru kwa zawadi yao ya kutulea mpaka kufikia mahali ambapo sisi tunajitegemea. Watoto huwa wanahitaji vitu vingi kutoka kwa mzazi …
Continue reading “Wape Watoto Vitu Vyote Lakini Usisahau Kuwapa Kitu Hiki Muhimu Kwao”
Haya Ndiyo Masoko Yanayofanya Vizuri Kuliko Masoko Yote
Kila mmoja wetu ni muuzaji na mnunuaji. Katika masoko watu wanapenda sana kusikia uhakika kutokana na kile unachouza. Watu wanapenda sana kusikia ushuhuda wa kile unachouza. Na masoko yanayofanya vizuri kupita masoko yote ni masoko ya neno la mdomo yaani word of mouth. Ni rahisi kusikiliza tangazo la bidhaa kwenye radio, ni rahisi kuona tangazo …
Continue reading “Haya Ndiyo Masoko Yanayofanya Vizuri Kuliko Masoko Yote”
Kitu Ambacho Hakijawahi Kumsaidia Mtu
Watu huwa wanajidanganya na kusema kuwa ukweli huwa unaumiza lakini ni kitu ambacho siyo sahihi. Kifalsafa ukweli huwa haumuumizi mtu bali ukweli huwa una msaidia mtu. Ni mara ngapi ukweli huwa unakusaidia? Ni mara nyingi tu, hivi mtu akikuambia ukweli kwa mfano, ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako acha kuwa mvivu amekusaidia au hajakusaidia? Atakuwa amekusaidia …
Huyu Ndiye Mwizi Mkuu Unayepaswa Kumshinda
Rafiki yangu, Unapanga mwenyewe kile unachotaka kufanya lakini baadaye unakuja kujidharau kwa kile ulichopanga halafu una tafuta sababu za kwanini usifanye kile ulichopanga. Mwizi pekee unayepaswa kumshinda ni wa tabia ya kuahirisha mambo. Kuahirisha mambo ni mwizi wa muda wetu na kujichelewesha mwenyewe kwenye kile tunachotaka. Unajua kabisa unachotaka, unaweka malengo, mipango lakini inapofika wakati …
Continue reading “Huyu Ndiye Mwizi Mkuu Unayepaswa Kumshinda”
Tafuta Mafanikio Lakini Usikubali Mafanikio Yakufanyie Kitu Hiki
Wengi tunakuwa bize sana kutafuta mafanikio lakini huwa tuna sahau kitu kimoja ambacho kinatufanya kitutenganishe na mafanikio tuliyopata. Mafanikio ni mazuri lakini usikubali mafanikio uliyopata yavunje mahusiano yako. Mafanikio yanakuwa mazuri pale tunapokuwa na watu wa kusherekea nao mafanikio tuliyopata. Ndiyo maana ni muhimu sana pale unapoweka juhudi katika kutafuta mafanikio usisahau mahusiano yako. Haina …
Continue reading “Tafuta Mafanikio Lakini Usikubali Mafanikio Yakufanyie Kitu Hiki”
Ujumbe Muhimu Kutoka Kwa Mtu Tajiri Kuliko Wote Duniani
Jeff Bezos kwa sasa ndiye mtu tajiri kuliko wote duniani yaani kwa lugha rahisi yeye ndiyo bilionea namba moja duniani. Bezos ana kitu kimoja ambacho anapenda kutushauri mimi na wewe ambacho yeye kilimsaidia na kupiga hatua na hatimaye kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani. Ni kitu cha kawaida sana na siyo kwamba hujawahi kusikia umesikia …
Continue reading “Ujumbe Muhimu Kutoka Kwa Mtu Tajiri Kuliko Wote Duniani”
Hii Ndiyo Staili Ya Kuishi Zama Hizi
Rafiki yangu, Mambo huwa hayawi kama unavyodhania. Wewe unapanga hivi na dunia inapanga vile inavyotaka yenyewe. Usipoifahamu asili unaweza ukalia kila siku na kuhisi dunia inakuonea kumbe la. Dunia huwa haimwonei mtu kwani yenyewe inafanya vile inavyotaka , haiangalii tumepanga nini ili itupendelee. Zama hizi unatakiwa kuishi staili ya kutarajia usiyoyatarajia. Unajiandaa kupata matokeo usiyoyatarajia …
Usiwe Kama Mkulima Kichaa
Rafiki yangu, Kwa dunia ya sasa watu wengi wanaongozwa kwa hisia kuliko kufikiri. Watu wamekosa kitu kinachoitwa subira. Watu wanataka mafanikio na matokeo ya hapo kwa hapo na kwa asili hatuwezi kupata kile tunachotaka hapo hapo. Tusiwe kama wakulima kichaa ambao wanapanda mbegu leo kesho wanataka wakafukue na kwenda kupanda sehemu nyingine. Wakati mwingine tuache …