Haya Ndiyo Maisha Bora Ya Kuishi

Asilimia kubwa ya watu wengi hawaishi maisha yao. Wengi wamezoea kuishi maisha ya kuona watu wengine wamefanya nini na siyo wao wanataka nini. Maisha bora ya kuishi ni yale ya kuishi vile unavyotaka wewe na siyo vile wanavyotaka watu. Unatakiwa kuishi vile unavyotaka wewe na siyo vile wanavyotaka wengine.Kuishi vile unavyotaka wewe ndiyo kuishi maisha …

Njia Ya Kufikia Uhuru Wa Kifedha Lazima Iwe Hivi

Wote tunajua kuwa fedha ni muhimu sana katika maisha yetu. Karibu kila kitu katika maisha yetu ya sasa kinaendeshwa na fedha. Na hewa tunayoivuta bure, ukiumwa kama huna fedha utakufa haraka sana. Ukiwa mzima hewa ni bure lakini ukiumwa utalipia hewa ya oksijeni ambayo haipatikani bure. Hapa nilikuwa ninaelezea ni namna gani pesa ilivyokuwa na …

Hiki Ndiyo Kitu Muhimu Kinachopatikana Kwenye Kazi Yako

Asili ya binadamu ni kazi. Kila siku unapoamka unatakiwa kufikiria leo unaendaje kuwahudumia wale wanaokutegemea. Kupitia kazi zetu, ndiyo mahali ambapo tunategemeana. Ujuzi uliokuwa nao au kazi au biashara unayofanya ndiyo mahali ambapo unaweza kutengeneza maisha yenye maana. Kwenye kazi yako unayoifanya kuna kitu muhimu sana. Kwenye kazi yako kuna nyota yako. Kila mmoja ana …

Jinsi Ya Kupata Tabasamu Kutoka Kwa Wengine

Chochote kile tunachotaka kutoka kwa wengine kinaanza na sisi kukitoa kile tunachotaka kutoka kwa wengine. Tunaweza kupata kile tunachotaka kama tutaweza kuwasaidia wengine kile wanachotaka. Tukitaka upendo, tunapaswa kutoa upendo. Usitegemee kutoa chuki halafu ukapata upendo. Asiyepoteza kitu haokoti, mkulima akitaka kuvuna gunia la mahindi, lazima apoteze debe moja chini ya ardhi.Kumbe basi, tunapotoa ndiyo …

Huyu Ndiyo Shujaa Wa Kweli

Watu huwa wanafikiri mpaka uwe shujaa basi uwe mtu jasiri sana.Yako mambo madogo madogo ambayo yanaweza kukufanya kuwa shujaa. Shujaa wa kweli ni yule anayeshinda hasira zake mwenyewe na chuki. Ukiweza kutawala hasira zako basi wewe ni shujaa wa kweli. Maana hapa watu wengi wanaongozwa na hisia kama vile hasira.Watu wakiwa na hasira wanakuwa ni …

Kama Umeshindwa Kuwasaidia Wengine Fanya Hiki

Kila mtu yuko hapa duniani kwa kusudi maalumu, hakuna ambaye yuko duniani kwa bahati mbaya. Asili ya binadamu ni kusaidiana , kama ilivyokuwa kwa viungo vya binadamu vinasaidiana na sisi pia tunatakiwa kusaidiana. Kila mmoja anamtegemea mwenzake, unapoamka asubuhi jua kabisa kuna watu wanakutegemea hivyo unapaswa kwenda kuwahudumia. Lakini Dalai Lama anasema hivi kama umeshindwa …

Kama Unataka Kujiona Hujui Fanya Haya

Hapa duniani unatakiwa kuishi kwa akili sana. Siyo tu kuishi kwa akili bali kuishi maisha yako. Kila mmoja wetu amepewa akili na akili ndiyo kitu kilichokutofautisha wewe na mnyama. Mnyama hana akili wala Imani uliyokuwa nayo wewe. Hivyo basi, kama unataka kujiona hujui basi anza kujifananisha na wengine. Kujifananisha na wengine ni utumwa, utajiona huna …

Hiki Nacho Kinahusika Katika Safari Ya Mafanikio

Ukisikiliza hadithi nyingi za mafanikio utasikia alianza na moja kisha akawa na tatu.Ni rahisi kusimulia ila hizi hadithi nyingi za mafanikio huwa zinakosa kitu kimoja ambacho kinampata kila mmoja wetu. Wanasema bahati ni pale maandalizi yanapokutana fursa.Ni kweli wala sina pingamizi juu ya hilo. Katika safari ya mafanikio kuna kitu kikubwa huwa watu hawakisemi ambacho …

Anza Mwaka Na Fikra Mpya

Fikra zilizotengeneza tatizo mwaka jana haziwezi kukusaidia kutatua tatizo jipya mwaka mpya. Unatakiwa kuwa mtu mpya katika kila eneo la maisha yako. Uache maisha ya mazoea na mbinu ulizotumia kushindwa mwaka jana usiendelee kuzitumia mwaka huu mpya. Badilisha gia kama gia uliyotumia mwaka jana haijakusaidia. Usiendelee kung’ang’ania kitu ambacho hakina msaada kwako na weka nguvu …

Kuhesabu Baraka Ni Kushukuru

William Arthur Ward aliwahi kusema, “kujisikia kutoa shukrani na kutoitoa ni kama kufunga zawadi na kutoitoa.” Rafiki yangu, Natumia nafasi hii kukushukuru kwa kuwa mshirika mkubwa wa kazi zangu za uandishi katika mwaka 2019.Bila wewe kazi zangu hazina kazi. Kushukuru ni kuomba tena. Hivyo ninakuomba tena tuendelee kuwa pamoja mwaka 2020 tuendelee kushirikishana maarifa mazuri …

Design a site like this with WordPress.com
Get started