Usitake Usichokuwa Nacho

Na shida yetu kubwa sisi binadamu iko hapa, tunapenda kutamani au kutaka vile ambavyo hatuna na matokeo yake tunakuja kusahau hata vile ambavyo tunavyo. Tunaweza kuwa na kile ambacho tunacho, lakini hatukitumii vizuri sana badala yake tunajikuta tunatamani vile ambavyo hatuna. Ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha. Badala ya kuangalia vile ambavyo huna hebu anza …

Hii Ndiyo Dhambi Unayopaswa Kuacha Kuitenda

Ukichunguza ndani ya mioyo yetu, utakutana watu wengi wana dhambi moja ambayo inawamaliza watu wengi katika zama hizi. Na dhambi hiyo siyo nyingine bali ni kulalamika. Tumekuwa ni watu wa kuwalalamikia wengine hata kama makosa ni ya kwetu kabisa tunakataa kukubali kukosa na tunatafuta ni nani ambaye tunaweza kumsingizia. Binadamu tunayo asili ya ukaidi, hii …

Tarajia Mazuri Lakini Tegemea Hiki

Hakuna mtu mwenye uhakika wa kitu chochote katika maisha yake zaidi ya kifo. Tunapanga mipango mingi lakini hatuna uhakika wa kufanikiwa mipango tuliyopanga. Falsafa ya ustoa inatualika sisi sote kama binadamu tupange mambo makubwa lakini tutarajie kinyume chake pia. Yaani chochote tunachokipanga tujiandae na matokeo yoyote yale. Umepanga kupata mazuri sawa, tegemea na kinyume cha …

Jiandae Kuishi Maisha Haya

Hivi ulishawahi kujiuliza maisha yako yatakuwaje kama usipokuwa na kile ambacho unacho sasa? Vipi cheo au wadhifa ulionao sasa ukinyang’nywa ghafla itakuwaje? Ulishawahi kujiandaa kuishi maisha ya kinyume cha kile unachoishi sasa? Yaani kama kwa sasa una kazi je ulishawahi kuishi maisha ambayo kama mtu ambaye hana kazi? Umejiandaaje na yale maisha ambayo hukuyategemea kuyaishi? …

Usivumilie Kitu Chochote Ambacho Hukipendi

Kila maisha utakayoamua kuishi tayari yana maamumivu yake. Hakuna maisha ambayo hayana maumivu ila ni kuchagua tu aina ya maumivu ambayo uko tayari kuyaishi. Ila nakushauri usivumilie kitu chochote ambacho hukipendi kwenye maisha yako. Hata kama kila mtu anavumilia na anachukulia kawaida. Kama kitu hukipendi au hukubaliani nacho au siyo viwango vyako usikubali kuwa navyo. …

Jinsi Ya Kuwasaidia Watu Wengi

Kiasili kila mtu ni mfanyabiashara, uwe umeajiriwa au la na kuajiriwa ni biashara nayo ila iko katika daraja sifuri katika ngazi ya biashara. Unapokuwa unataka kuwasaidia watu basi kuwa na biashara kwani hata kama umeajiriwa kama mwajiri wako asingefungua biashara leo hii ungepata ajira? Kumbe basi, biashara ni moja ya njia ya kuwasaidia watu wengi …

Dalili Inayoonesha Kuwa Unarudi Nyuma Kiuchumi

Fedha ni jawabu la mambo yote na hilo halina ubishi kabisa kwani kila mmoja analiona hilo katika maisha yake ni namna gani fedha ilivyo muhimu. Anayekuambia fedha siyo muhimu basi akili yake haiko sawa. Ni muhimu sana kujipa tathimini katika kipato chako kila mwezi, siku, wiki au hata mwaka. Kama kipato chako hakiongezeki na matumizi …

Jinsi Ya Kuwa Na Siku Bora

Unapoianza siku yako ni maamuzi yako kutaka siku yako iweje na wewe ndiyo mkurugenzi wa siku yako kwa kupanga kile unachotaka kitokee. Asubuhi unapoamka una amua na kusema leo ni siku bora sana kwangu na nimechagua kuwa na furaha. Kama hujui nguvu ya kukiri, jaribu leo kukiri kuwa leo ni siku bora sana kwangu, nimechagua …

Njia Ya Pekee Ya Kutojiumiza

Katika wakati ambao watu huwa wanajiumiza na kujivuruga basi ni zama hizi tunazoishi. kwa sababu watu wanakuwa wanaweka matumaini yao kwenye vitu ambavyo viko nje ya uwezo wao na ndiyo maana ni rahisi kujiumiza. Iko njia pekee ya kutojiumiza na njia hiyo ni kutumia falsafa ya ustoa ambayo moja ya falsafa zake zinasema kuwa, usiweke …

Tathimini Ya Siku Yangu Ya Kuzaliwa Na Viwango Vitano Vya Kupima Afya Yako Ya Kifedha

Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, nilizaliwa miaka 31 iliyopita tarehe 18/7/1989. Huwa nina kawaida ya kujifanyia tathimini katika kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwangu. Leo asubuhi nilianza siku yangu tofauti kabisa na huwa navyoanza. Huwa ninaanza siku yangu kwa sala au tahajudi, kusoma kidogo, kuandika na mazoezi. Lakini katika vyote hivyo, huwa ninahakikisha kabla dunia …

Design a site like this with WordPress.com
Get started