Fanya Kazi Na Wateja Hawa

Rafiki, Siyo kila mteja ni mteja kwako.Kuna wateja wengine wanaweza kuja kwako lakini siyo sahihi. Na siku zote kwenye biashara na hata maisha kwa ujumla.Fanya kazi na kitu kinachofanya kazi tayari. Wateja wazuri ni wale ambao wana uwezo wa kumudu gharama ya kile unachouza.Usihangaike na wateja ambao hawana hela, ambao hawana uwezo wa kumudu gharama …

Biashara Inayolipa Zama Hizi

Rafiki, Ukiangalia maisha ya watu wengi kwa nje utaweza kusema kwamba wametulia. Lakini, maisha ya watu wengi kwa ndani hawajatulia. Ukifanikiwa kutulia kwenye maisha yako, utaona raha ya maisha.Kama hujatulia kiroho, kimwili na kiakili, unaweza ukajikinai hata wewe mwenyewe na kuona hakuna maana ya maisha. Kwa kuwa watu wengi hawajatulia kwenye maisha yao, hawajutulia kwenye …

Fuatilia, Usilalamike

Watu wengi pale wanapoona wamepata changamoto ambayo imesababishwa na watu wenye mamlaka ya kitu fulani, huishia tu kulalamika. Usiishie tu kulalamika, bali fuatilia.Matatizo mengi yanashindwa kutatuliwa katika jamii zetu kwa sababu ya watu kushindwa kufuatilia kwa watu mwenye mamlaka husika wa kutatua shida zao. Badala yake wanaishia kulalamika kwa watu wasiokuwa na mamlaka na matokeo …

Kama Siyo Muhimu Usiongee

Kwenye maisha usiwe muongeaji sana. Ongea yale ambayo ni muhimu tu. Unapoongea sana, utajikuta unaongea yale yasiyokuwa na maana.Kama watu walikuwa wanakuheshimu, wanaweza kukushusha kwa yale unayoongea. Hata mpumbavu akikaa kimya, huwa anaonekana mwenye hekima. Ongea kama ni muhimu tu na kama siyo muhimu usiongee. Changia pale unapoona usipochangia mambo yataenda kuwa vibaya. Mara zote …

Usiogope Kushindwa

Kama bado hujapata kile unachotaka, endelea kuweka kazi. Usiishie njiani, atafutaye hachoki na akichoka ameshapata. Je, wewe unataka kuchoka umeshapata?Pambana ufanikiwe na mafanikio yako yatafuta kabisa kushindwa kwako ambako umepitia. Ni kupitia kushindwa ndiyo utafanikiwa na ukishafanikiwa hakuna atakayekumbuka yale uliyoshindwa. Hatua ya kuchukua leo; Nenda kawaoneshe wale wote ambao wanakuambia umeshindwa kwa kufanikiwa zaidi. …

Mtu Anayependa Wengine Wafanikiwe

Mtu aliyefanikiwa, huwa anapenda wengine wafanikiwe. Ni mtu asiyefanikiwa, ndiyo huwa hapendi kuona wengine wakipiga hatua. Mtu aliyefanikiwa kwa njia sahihi, huwa anapenda kuwawezesha wengine kupiga hatua.Huwa wanapenda kuwaelimisha wengine mbinu za kufanikiwa zaidi. Wakati mwingine huwa wanajitoa kwa ajili ya wengine pasipo hata kulipwa ili watimize lengo lao la kuona watu wanafanikiwa. Kuwa mtu …

Jinsi Ya Kujitambulisha Kwa Sekunde 30

Rafiki, Umakini wa watu umeshuka sana katika zama hizi. Hivyo watu hawana muda wa kusikiliza kwa muda mrefu kama hutafanikiwa kuteka akili zao. Pale unapokutana na watu, unapaswa ujitambulishe vizuri ili watu wakujue wewe ni nani, unafanya nini. Ukipata fursa ya kuonana na watu wengi, jitambulishe vizuri na kuibua shauku kwa watu wengine kukutafuta kwa …

Adui Mkubwa Wa Imani Yako

Maisha ni imani. Kama unaamini itakuwa na kama huamini haitakuwa. Imani yako inafunga au kufungua milango ya baraka. Kama ukijiamini wewe mwenyewe, hata watu wengine watakuamini.Kitendo cha wewe kutokuwa na imani na wewe mwenyewe, kinapelekea hata watu kutokuamini kile unachofanya. Kuwa na imani na amini bila shaka yoyote ile na mambo mengi yataenda vizuri sana. …

Bado Hujakielewa Vizuri

Lengo la mawasiliano yoyote ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Kama mawasiliano unayofanya hayaeleweki, huwezi kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Mwalimu mzuri, ni yule anayeeleweka. Ni yule ambaye anatumia lugha rahisi kufikisha ujumbe. Njia rahisi ya kuwa mtu anayeeleweka ni uwezo kuelezea kitu kwa urahisi. Kama huwezi kueleza kwa urahisi bado hujakielewa vizuri.Njia rahisi ya kujipima kama umekielewa kitu …

Usijisahau Wewe Mwenyewe

Ni kawaida ya watu wengi kufanya kazi na kuwasaidia watu wengine lakini wao wenyewe hawajisaidii.Hii siyo nzuri, pale unapofanya kazi mtu wa kwanza kumkumbuka unapaswa kuwa wewe mwenyewe.Unapata hela, unawalipa watu wengine, lakini unajisahau hata kujilipa wewe mwenyewe. Watu watafurahia vile unavyowapa sasa lakini baadaye utakapokua huna nguvu za kufanya kazi hawatakukumbuka kama vile unavyowafanyia …

Design a site like this with WordPress.com
Get started