Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo 20 Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Start With Why

Habari mpendwa Rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama.  Rafiki, tumebakiza masaa machache kuukaribisha mwaka mpya na kuuaga rasmi mwaka 2016.

Mpenzi msomaji, katika masaa haya yaliyobakia Fanya kitu ambacho hukuwahi kufanya cha kuleta maendeleo kwako binafsi na kwa jamii nzima. Usikubali leo ipite bila kuacha alama.

Image result for start with why simon sinek

Mpendwa msomaji, leo nitakwenda kukushirikisha uchambuzi wa kitabu Yale mambo machache kati ya mengi niliyoweza kujifunza.

Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha Start With Why kilichoandikwa na Simon Sinek ni kama ifuatavyo;

1. Unapokuza biashara yako unakuwa unafanya ongezeko la thamani. Anza na kujiuliza kwanini wateja ni wateja wako. Ukuzaji wa biashara ni muhimu kwani unapokuza biashara unaongeza thamani na kupata faida.

2. Usifanye vitu kwa kuiga. Kama ukimwona rafiki yako anaweka kichwa kwenye oven na wewe utaweka? Kwahiyo, hatutakiwi kuiga kila kitu. Unaweza kuiga mambo chanya ambayo yatabadilisha mwenendo wako wa maisha. Mfano,kama mwenzako anasoma sana vitabu basi ni jambo zuri la kuiga.

3. Ugunduzi au uvumbuzi umeleta mambo makubwa duniani. Uvumbuzi ndio umeleta simu tunazotumia leo. Simu iliyokuwa inatumika mwaka 2000 na simu ya 2016 zina utofauti mkubwa sana hii yote ni uvumbuzi. Mtoto aliyezaliwa leo hawezi kujua kama tulikuwa tunatumia tepu za mikanda katika radio. Tunashukuru kwa wagunduzi wetu kutulea mabadiliko haya.

4. Wadanganyaji wamekuwa wengi siku hizi. Watu wanadanganya ili waweze kutimiza mahitaji yao. Viongozi wengi wanadanganya kuliko kuhamasisha. Mfumo wa uongo umeenea kila mahali katika jamii zetu. Watu wanadanganya hata maisha yao wanayoishi.
Tuishi katika ukweli na siyo udanganyifu.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Lead To The Field

5. Watu, kampuni na taasisi mbalimbali duniani wanajua nini wanafanya. Kujua nini unafanya na kwanini unafanya ndio msingi wa kitu chochote unachofanya. Ndio thamani ya kazi yako, biashara yako. Jua nini unafanya na kwanini unafanya.

6. Watu hawanunui Nini unafanya bali watu wananunua Kwanini unafanya. Watu wanaangalia kwanini unafanya. Kwanini unafanya ndio ina nguvu na kuleta matokeo mazuri. Kama unasoma lazima ujiulize kwanini unasoma. Hivyo basi, tujitafakarishe kila siku kwanini unafanya hicho unachokifanya. Kwanini itakuwezesha kuleta ubora katika huduma au bidhaa.

7. Kwanini ni kama imani. Imani yako ndio mauzo yako inayokusukuma kuuza kile unachoamini kwanini unafanya. Kama huna kwanini huna uhakika na huduma au bidhaa unayotoa.
Kwanini yako ndio ufungui wako wa kufanya vizuri.

8. Amka kila siku na nenda kafanye kile kitu unachokipenda. Wahamasishe watu kufanya kile kitu wanachokipenda. Ukitaka kufanikiwa fanya kile kitu unachokipenda kwasababu utafanya kwa moyo wote. Ubunifu na umakini utaongezeka ukilinganisha na mtu ambaye anafanya kazi asiyoipenda kwa shingo upande.

9. Tafuta watu wanaoamini kile unachoamini. Fanya kazi na watu wanaoamini falsafa yako. Ukifanya kazi na watu ambao wanaamini kile unachofanya ni kuwa na watu chanya ambao mnaambatana kifalsafa. Hivyo basi,ambatana na watu unaoendana nao.

10. Ukweli ni kwamba kila mtu ana shauku katika hii sayari. Lakini ukweli ni kwamba shauku zetu zimetofautina. Shauku ya kufanya jambo ni nguvu katika sehemu yoyote ile ili kuleta maendeleo husika. Tutumie shauku zetu kuleta ufanisi.

11. Kazi ya kiongozi siyo kuja na mawazo kubwa yote peke yake. Bali kazi ya kiongozi ni kutengeneza mazingira ya mawazo makubwa ambayo yanaweza kutokea. Kiongozi ni mwezeshaji ambaye anatoa mwanga kwa watu wengine na siyo kila kitu kufanya yeye kwani watu anaowaongoza wana vitu vizuri pia.

12. Uaminifu ni kitu kinachooneka. Uaminifu ndio unatusaidia sisi binadamu kufanya kazi na watu wengine. Uaminifu ndio unawafanya watu wengine kupata pesa na kutengeneza mitandao na watu. Uaminifu unaleta amani katika maisha yetu. Uaminifu unaleta matokeo mazuri na ufanisi wa kazi.

13. Kuwa na maono na amini katika ndoto yako.
Mfano, Martin Luther king aliwahi kutoa hotuba yake juu ya kuwa na ndoto fulani japo wengi waliona ni kama kitu ambacho hakiwezekani lakini yeye aliamini hivyo juu ya ndoto yake japo wengi walimbeza. Tunajifunza tuamini katika ndoto zetu bila kuwasikiliza watu wanasema nini wewe a mini katika kwanini yako inayokusukuma kutoka ndani na siyo nje.

14. Kwanini ni malengo mahususi yanayokusukuma kutimiza lengo fulani.
Kama huna kwanini basi huna kitu kinachokusukuma kufanya kitu. Kwanini ni kama vile una njaa au kiu inayokusukuma kwenda kufuata chakula au maji ili utimize njaa au kiu yako.

15. Kiongozi hawezi kuleta mabadiliko mwenyewe. Kiongozi analeta mabadiliko kwa kuwaha
masisha watu wengine kuleta mabadiliko. Kama unataka kufanya mabadiliko hamasisha watu kufanya kile unachoamini kitaleta mabadiliko.

SOMA; Moto Wa Hamasa Utakaokuwezesha Kupata Nafasi Ya Kazi Sehemu Yoyote Duniani

15. Ni vema kuwakuza watoto wadogo katika hisia za kuamini katika uwezekano. Watoto warisishwe fikra chanya tokea wakiwa wadogo. Changamoto ya jamii zetu watu wenye mtazamo chanya ni wachache ukilinganisha na watu hasi. Wazazi wanatakiwa kubadilika ili kuwarisisha watoto wao fikra chanya. Kama wazazi hawatobadilika ni ngumu kwa watoto kurithishwa mtazamo chanya.

16. Kitu kinachotengeneza eneo la masoko ni wateja na wateja muhimu. Wateja wanaweza kuwa wengi lakini sio wote watanunua kile unachouza.
Wateja muhimu ni wale wanaonunua kile unachouza. Je biashara yako ina wateja au wateja muhimu?

17. Jamii yetu imekuwa ni ngumu sana katika suala la kusoma vitabu. Watu wanapitwa na mengi kwa kutokusoma vitabu. Jamii ingekuwa inabidii ya kusoma vitabu ingekuwa mbali. Kila mmoja awe balozi wa mwenzake kwa kumhamasisha juu ya usomaji wa vitabu.

18. Mawasiliano siyo kuongea bali ni kusikiliza. Unapokua unasikiliza ndio unatajua kwanini unasikiliza. Unagundua dhumuni la kusikiliza ni nini hasa. Tunaposikiliza tunajifunza vitu vingi. Kama wewe siyo msikilizaji anza na kwanini husikilizi. Ukianza na kwanini
Utajua umuhimu wa kusikiliza.

19. Wazazi siku hizi hawawapi watoto wao aina moja wapo ya kuonesha upendo kwa watoto wao kwa njia ya muda. Watoto nao wanahitaji muda wako kama vile wewe unavyojali kazi zako. Familia yako inakuhitaji sana kuliko unavyofikiria. Zawadi ya kujitoa muda wako kwa familia yako ni zaidi ya kuwapatia fedha. Kwani zawadi ya muda huwezi kwenda kununua dukani wala kuitafuta kama unavyotafuta pesa.

20. Umebeba tochi sahihi?
Ili uweze kuwa mwanamafanikio unatakiwa kubeba tochi sahihi itakayokupa mwanga wa kule unakoenda. Tochi sahihi ya wewe kufika kule unakokwenda ni kuwa na maarifa sahihi. Maarifa sahihi ni tochi kwako inayokuongoza kwa kukupa mwanga katika safari ya mafanikio yako.
Nishati ya safari ya mafanikio ni kuwa na maarifa sahihi yatakayo kuongoza.

Mwisho, tunajifunza mambo mazuri kila siku. Hivyo basi, jukumu letu ni kuyaishi yale tunayojifunza na kuwa mabalozi wazuri katika jamii yetu. Kuwashirikisha kile tunachojifunza na kuwaalika kujifunza.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: