Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tafsiri Ya Mtu Mwenye Roho Nzuri Na Mbaya

Kifupi, hakuna mtu mwenye roho nzuri au mbaya.

Mwenye roho nzuri au mbaya anakuja kutokana na tafsiri ambayo wewe unayo juu ya yule mtu.

Kwa mfano, kama ukimuomba mtu kitu na akakusaidia utasema ana roho nzuri na akitokea mtu mwingine akienda kumuomba na kumwambia hapana utasema ana roho mbaya.

Kumbe basi, roho nzuri au mbaya inatokana na tafsiri zetu wenyewe.

Yule ambaye kwako ana roho mbaya kwa mwingine atasema ana roho nzuri.

Na kipimo kikubwa ambacho watu huwa wanapimia watu ni kwenye kutoa. Mtu akipewa kile anachotaka atasema ana roho nzuri na akinyimwa atasema ana roho mbaya.

Siyo sahihi kuwapima watu kwa vile tunavyotaka sisi na kwa tafsiri zetu wenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; kile kinachopelekea wewe kusema mtu fulani ana roho nzuri au mbaya ni tafsiri zako mwenyewe.

Usiwatafsiri watu vile unavyotaka wewe kwa sababu wamekunyima kile unachotaka kutoka kwao.

Mtu kukusaidia wewe ni hiyari yake na wala siyo lazima hivyo ikitokea mtu hajakupa kile unachotaka kutoka kwake wala usimlaumu na kusema ana roho nzuri au mbaya.

Ni hiyari ya mtu kutumia kile alichonacho vile apendavyo na sivyo unavyotaka wewe mwenyewe.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: