Rafiki,
Zama zimebadilika sana, watu wamekuwa na tabia ambazo huwezi kuziamni. Changamoto ya sasa kila mtu anaweza kuwa rafiki yako na adui yako. watu wanavaa ngozi ya kondoo kujifanya wao ni watu fulani kumbe siyo ili waweze kukutapeli.
Katika zama hizi unapaswa kuwa makini kwanza na wewe mwenyewe. ukishakuwa makini kwanza wewe mwenyewe utaepuka kutapeliwa vitu vingi. Usiwe mtu kila mtu na kumwamini kila mtu, uaminifu umekuwa ni zawadi ghali na usitegemee kuupata kwa mtu wa kawaida.
Watu wamekosa uaminifu kabisa, ndiyo maana watu wamekuwa wakiibiwa au kutapeliwa na watu wanaweza kutumia hata jina lako bila wewe kutapeli watu wengine.
Unatakiwa kuwa makini kwanza na wewe mwenyewe zama hizi. Kuwa makini kuanzia wewe mwenyewe na hata wale waliokuzunguka. Usiwe mtu wa kuongozwa na hisia, bali ongozwa na akili.
Hizi siyo zama za kumwamini kila mtu. Zimekuwa ni zama ambazo watu wana uhuru wa kufanya chochote kwa sababu wa ujio wa teknolojia unawasaidia kufanya hivyo.
Kuwa makini na fedha zako, usiwe mtu wa kutoa fedha kwa hisia. Kabla hujamtumia mtu kitu iwe ni fedha au nini jiridhishe sana. kitendo tu cha wewe kuwa makini ni ulinzi tosha katika maisha yako. utakapokuwa wewe makini utapunguza baadhi ya matatizo yanayotokana kwa sababu ya uzembe.
Jilinde wewe mwenyewe na walinde wengine. wajibika ili uishi na wengine pia waishi. Jitahidi kuwa mtu sahihi ili na wengine wawe watu sahihi kama wewe.
SOMA; Hizi Ndio Athari Za Kutokuwa Makini Katika Kazi Unazofanya Kila Siku
Hatua ya kuchukua leo; kuwa makini kwa kitu chochote kile, usimwamini mtu mara moja. Adui wa binadamu ni binadamu mwenzake na siyo samba. Ila ukianza wewe kuwa makini na wale wanaokuzunguka watakua makini pia.
Kwahiyo, usiruhusu ujinga kwenye maisha yako. usiambatane na mtu ambaye unaona siyo sahihi kwako. Unapopatwa na jambo fulani au unapohitajika kufanya kitu fulani au kutoa kitu fulani jipe muda kidogo wa kutafakari je kile unachokwenda kufanya ni sahihi? Kujiridhisha ni mama wa umakini hivyo penda kujiridhisha kwa faida yako mwenywe.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.