Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kujihamasisha Wewe Mwenyewe

Mpendwa rafiki yangu,

Watu wengi wanakata tamaa kwa sababu ya kukosa hamasa, wako ambao wanayaona maisha yao hayana maana ya wengine ndiyo yenye maana. Wengi wanayadaharau maisha yao na kushindwa kujikubali hata kwa kile kidogo walichonacho.

Tusipojifunza jinsi ya kujihamasisha sisi wenyewe na kusubiri watu wegine ndiyo waje kutuhamasisha tutazidi kuyachukia maisha yetu na mwisho wa siku tutaona hakuna maana ya kuishi. Ukiona mtu anafikia mpaka hatua ya kusema hana haja ya kuishi ni kwa sababu amekosa hamasa, hakuna mtu ambaye yuko naye karibu anayemwasisha na kumtia moyo.

Wako watu wanaishi tu, lakini hawana wala hawapati upendo kama wanavyopata watu wengine. wengi wako katika umasikini wa upweke, wanapokataliwa na mtu mmoja basi wanajiona kwamba wao hawana bahati au wana mkosi na kuanza kujiambia maneno ambayo hayana maana kwenye maisha yako.

Image result for encourage yourself quotes

Unatakiwa kujifunza namna ya kujihamasisha wewe mwenyewe, kujitia moyo. Na tunatakiwa tujikubali kuwa sisi ni washindi licha ya changamoto tunazopitia. Hakuna ambaye hana matatizo au hakuna ambaye hapitii changamoto fulani katika maisha yake, hivyo unapojikuta katika matatizo usifikirie uko peke yako, au Mungu amekuacha bali jifunze kuwa chanya  katika kila changamoto unayopitia kuna jema ndani yake. Ukiziangalia vizuri utagundua tu, usiwe mtu wa kutoroka changamoto bali kuwa mtu wa kujifunza na kujiuliza kwanini hii imetokea na nimejifunza nini.

SOMA; Kama Unapitia Changamoto Yoyote Ile Usiache Kusoma Hapa

Kama hakuna ambaye anakupongeza katika maisha yako, anza kujitia moyo wewe mwenyewe. unaweza kujiandikia barua nzuri ya kujipongeza katika maisha yako. na pale unapokuwa unakosa hamasa irudie kuisoma ile barua utapata hamasa.

Kaa chini na fikiria yale mambo mazuri yote uliyofanya, yale yaliyokupa ushindi na yaandike sehemu halafu kila siku yasome na pale unapohisi kukata tamaa au hakuna anayekuunga mkono basi jihamasishe kwa kusoma ujumbe huo.

Kuna mambo mengi ya kushukuru kila siku hata kama kuna mengine yameenda mrama, unaweza kujipongeza kwa kila hatua au kwa yale uliyofanya wewe mwenyewe, nenda kwenye kioo chako jiambie fulani hongera sana kwa kazi nzuri uliyofanya leo, hongera sana kwa ushindi uliopata leo. Hamasa inakuja pale tunapoanza sisi wenyewe kujitia moyo na kujipongeza.

Kama hakuna mtu anayekuambia wewe ni mzuri au kukuambia nakupenda usijali jifunze kujipongeza na kujihamasisha na kujitoa moyo, yaani learn to encourage  yourself, nenda kwenye kioo chako jiambie Deo nakupenda, au Deo wewe ni mzuri sana hiyo ni mifano ya kujiambia na jiambie kadiri ya jina lako.

Usiwe mtu wa kujilinganisha na wengine kwa sababu utapoteza nguvu na kujiona wewe ni mtu wa hovyo pale unapoanza kujilinganisha na watu wengine. yaone maisha yako ni bora, jione kama uko porini uko peke yako na huna wakujilinganisha naye. Watoto wadogo wanafurahia maisha kwa sababu hawana mambo ya kujilinganisha kama sisi watu wazima. Usijione wewe ni mtu wa chini bali jione wewe ni mtu wa juu.

Kila mmoja wetu ameuona mkono wa Mungu katika maisha yake, hivyo unapofikia wakati wa kukata tamaa, hebu rudi nyuma na anza kumshukuru Mungu kwa yale mazuri ambayo amekusaidia mpaka hapo ulipo leo. Yaani ukifikiria tu mazuri ambayo Mungu amekufanyia hiyo inakuwa ni hamasa tosha kwenye maisha yako. Tukikaa chini na kufikiria makuu ya Mungu hiyo ni hamasa tosha katika maisha yetu.

Hatua ya kuchukua leo; jifunze kujihamasisha wewe mwenyewe kila siku. Jipongeze na jione wewe ni malkia au mfalme katika maisha yako. jivunie vile ulivyo na usijilinganishe na wengine. rudia kusoma hii makala kwa kujipa hamasa.

SOMA; Jinsi Ya Kupata Hamasa Na Kufanikiwa Kwenye Kile Unachofanya

Kwahiyo, tunatakiwa tuwe ni watu wa kushukuru, tukikosa kuwa na shukrani tumepoteza fadhila. Na tukipoteza fadhila tumepoteza matumaini, imani na mapendo juu yetu. wewe ni sehemu ya maajabu ya ulimwengu, hakuna mtu kama wewe duniani kote, una kitu cha kipekee ambacho mtu mwingine hana, hivyo jipende na jikubali katika kile unachofanya kwenye maisha yako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: