Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Lead To The Field

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini umekuwa na siku nzuri rafiki huku ukiendelea kusherekea sikukuu.

Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Leo nitakwenda kukushirikisha uchambuzi wa kitabu baadhi ya mambo niliyojifunza kupitia kitabu nilichosoma. Wiki jana nilisoma kitabu kiitwacho Lead To The Field kilichoandikwa na Earl Nightingale.

Mambo niliyojifunza katika kitabu cha Lead The Field kilichoandikwa na mwandishi Earl Nightingale ni kama ifuatavyo;
Karibu rafiki uweze kujifunza.

1. Mimi na wewe ndio tunawajibika katika maisha yetu.
Tupo hivi tulivyo leo kulingana na kile ulichokitoa nje.
Kumbe basi, maisha yetu kuwa mazuri au mabaya inatokana na jinsi tunavyowajibika kila siku.
Na tuko hivi kulingana kile tunachotoa. Kama ukipanda haba utavuna haba hivyo basi, ni utapata kile unachotoa kwa wengine.

2. Ni muhimu sana katika maisha kuweza kujizuia au kusimamia mitazamo yetu juu ya kitu fulani yaani state of our mind. Ni muhimu sana kusimamia mitazamo yetu iwe katika hali nzuri au bora zaidi.
Kwa mfano, mwingine anaweza kuwa mtazamo hasi juu ya kujifunza kama vile kusoma vitabu hata kusoma makala na kujifunza kwa wengine. Sasa ukishakuwa na mitazamo kama hii ya kushindwa kujifunza ni dhahiri unajifungia katika shimo.
Tunaalikwa kuwa na mitazamo chanya katika maisha yetu kwani ndio ina nguvu ya kuijaza dunia kwani dunia ina njaa bado.

3. Mwanasaikolojia wa kimarekani kutoka chuo kikuu cha Harvard William James anasema, binadamu anaweza kubadilisha maisha yake kama akibadilisha mtazamo wake wa akili.
Mwandishi na Mhamasishaji Brian Trancy naye aliwahi kusema badilisha mtazamo wako wa kufikiri badilisha maisha yako.
Kumbe basi, maisha yetu yatabadilika kama tukibadilisha mitazamo yetu ya kufikiri.
Kama utafikiria maisha katika hali ya mtazamo chanya basi maisha hayatokuwa magumu. Lakini kama ukishachukulia maisha yako katika hali ya mtazamo hasi utakuwa uko sehemu hatari sana.
Hivyo basi, badilisha mtazamo wa kufikiri badilisha maisha yako.

4. Katika maisha unatakiwa kuwa na vitu viwili muhimu navyo ni ;
1. Shukurani (gratitude)
2. Matarajio (expectant)
Kwa mfano mwandishi anatualika kuwa unapoamka asubuhi lazima uwe na vitu viwili kwanza, kwa mfano, yeye anaanza kwa kushukuru kwa fursa ya kuwepo katika dunia nzuri na ya ajabu ambayo ni sayari ya dunia.
Pili, anaamka na hisia za kutarajia kupata kilicho bora yaani wakoloni wanasema I expect the best.
Hivyo anza leo, unapoamka asubuhi anza na kushukuru kwanza halafu tarajia kupata kilicho bora katika malengo uliyojiwekea ya siku husika.

5. Hakuna kitakachobadilika katika maisha yetu bila kukibadilisha.
Lazima tubadilike ili tupate mabadiliko kwenye maisha yetu.
Dunia hawiezi kubadilika kama watu hawataki kubadilika katika maisha yao.
Maisha ni mabadiliko hivyo chagua kubadilika mpendwa rafiki ili tuweze kuifanya dunia kuwa sehemu salama na bora kuishi kwa kila mmoja wetu.

6. Mwambie mtu yoyote ambaye una mahusiano naye kuwa yeye ni mtu muhimu sana katika dunia hii.
Mwanafalsafa mkubwa na mwandishi wa kijerimani Goethe aliwahi kusema kabla hujafanya kitu lazima uwe kitu kwanza.
Hii ina maana kwamba kama unataka kufanya kitu lazima ujiandae kwanza. Ukitaka kuibadilisha dunia wape watu kwanza elimu. Before you can do something, you must be something.

7. Fanya msamaha katika Marsha yako. Wasamehe wale waliokukosea na sahau yaliyopita.
Kumbuka, kujisamehe hata wewe usije ukasahau kujisamehe mwenye kama yaliyomkuta ndugu Yuda eskari yote aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.
Tunapaswa kujisamehe na kuepuka hata kujilaani sisi mwenyewe.

8. Usipoteze muda wako kuongea na mtu ambaye hawezi kutatua matatizo yako.
Usipoteze muda wako kumwambia mtu matatizo yako ya kiafya labda awe dokta wako. Kwasababu haitowasaidia wengine na hata wewe mwenyewe.

9. Akili yako ndio rasilimali utajiri.
Je unaweka nini katika akili yako.
Kile unachoingiza katika akili yako ndicho unachokitoa wakati wa kuongea.
Wekeza katika akili yako. Wekeza katika maarifa kwani mtaji wa mambo yote.

10. Changamoto ndio zinaonesha ubora wetu.
Changamoto anatufanya sisi binadamu kuwa bora kila siku.
Changamoto ndio inapika akili ya mwanadamu.
Usizikimbie wala kuziogopa zifurahie kwa kukabilianza nazo.

11. Binadamu hatakiwi kutulia na kuridhika.
Kwa ng’ombe, kuku, paka ni sawa kukaa lakini siyo binadamu.
Tunahitaji mabadiliko kwa binadamu lakini siyo kukaa hayo ni sawa kwa viumbe vingine lakini siyo binadamu.

12. Uhuru ,Uhuru , Uhuru.
Uhuru binafsi yaani personal liberty ni kitu cha thamani duniani.
Uhuru umekuwa ni kitu adimu sana miongoni mwa watu wengi.
Nchi nyingi zilitawaliwa hivyo walipigana kuhakikisha wanapata Uhuru wao na kujikomboa.
Kumbe watu wanapenda uhuru, je ni kwanini watu wengi wanaishi maisha utumwa na vifungo kama vile wako gerezani?
Kama uko katika gereza hilo tafadhali tafuta Uhuru wa maisha yako.
Huwezi kufanikiwa kama hauko huru kiakili yaani huwezi kujifanyia maamuzi wewe mwenyewe.

13. Siri ya furaha hapa duniani ni Uhuru. Huwezi kuwa na furaha kwenye maisha yako kama hauna Uhuru.
Na siri ya Uhuru ni kujiamini.
Kumbe basi, kutokujiamini katika maisha yako ni wazi umekosa Uhuru. Hivyo basi, unahitaji ukombozi na kupata Uhuru wa kujiamini.

Mpendwa msomaji, nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Washirikishe na mwenzako maarifa haya uliyopata.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

2 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: