Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ujumbe Muhimu Wa Kristmas Kutoka Kwa Wiston Churchill

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini hujambo na unaendelea vizuri. Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo.

Mpendwa msomaji, mtandao wa Kessy Deo unapenda kutumia nafasi hii kukutakia heri ya sikukuu ya kristmas. Leo ni siku ya kristmas ambapo wakristu wote duniani wanaadhimisha sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristo. Heri ya kristmas mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo popote pale ulipo.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo. Leo nitakwenda kukushirikisha ujumbe muhimu kwako wa kristmas kutoka kwa Winston Churchill.

Mpendwa msomaji, nakusihi sana ungana nami ili tuweze kusafiri pamoja mpaka mwisho ili uweze kufahamu ujumbe mzuri sana wa kristmas niliokuandalia.

Leo nitakushirikisha ujumbe mzuri kutoka kwa Winston Churchill ambaye alikuwa ni waziri mkuu nchini uingereza mnamo mwaka 1940-1945 na awamu nyingine tena mwaka 1951 mpaka 1955.

Winston Churchill aliwahi kusema hivi “Christmas is a season not only of rejoicing but of reflection”
Akiwa na maana ya kwamba kristmas ni msimu sio tu wa kufurahia bali pia wa kufanya tafakari.
Kumbe basi, tunaalikwa sisi sote kuweza kufurahia kristmas lakini pia ni muda mzuri sana kwetu kuweza kufanya tafakari ya maisha ndani ya mwaka mzima maisha yako yalikwendaje.

Leo sio tu siku ya kusherekea sikukuu bali pia ni siku ya kufanya tafakari na tathimini juu ya maisha yako.

Leo ni siku ya kukaa na familia yako, wote kwa pamoja mkisherekea sikukuu ya noel yaani Christmas.

Leo kaa na ndugu zako,marafiki,jamaa na watu wa karibu kwako kama mlikuwa mmetofautiana basi huu ndio muda muhimu wa kusameheana na kurudisha uhusiano wa awali.

Usitumie siku hii ya leo vibaya bali tumia vizuri. Sherekea kwa utaratibu bila kufanya fujo, kuvunja sheria zilizowekwa na mamlaka husika hapo ulipo.

Hatua ya kuchukua leo, tenga muda wako binafsi leo wa kujitafakari na kujitathimini juu ya maisha yako. Sherekea katika hali ya kumpendeza mwenyezi Mungu na bila kuvunja sheria za nchi.
Kama una ndugu, jamaa,marafiki na nakadhalika hujawasiliana naye tokea mwaka uanze wasiliana naye leo na muanze maisha mapya.
Leo ni siku ya kuzaliwa upya katika maisha yetu hivyo itumie vema kwa mabadiliko chanya.

Mwisho, tumealikwa sisi sote siku hii ya leo kuweza kufurahia na kusherekea sikukuu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Lakini pia, tumealikwa kuweza kuweza kufanya tafakari na kujitathimini sisi mwenyewe. Tuingie katika tafakari ya ndani zaidi. Unahitaji muda wa upweke kuweza kufanya haya.

Mpendwa msomaji nakutakia tena heri ya sikukuu ya Noel yaani Kristmas usherekee kwa Amani bila kusahau kufanya tafakari juu ya maisha yako ndani ya mwaka mzima.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: