Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huu Ndio Ugonjwa Unao Ua Watu Wengi Katika Safari Ya Mafanikio

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumani yangu kuwa hujambo u buheri wa afya kabisa na kama hauko vizuri nichuke nafasi hii kukupa pole mpendwa rafiki yangu. Katika hali ya kawaida huwezi kuwa vizuri kila siku kuna wakati mwingine mwili unakuwa hauko sawa. Leo ni siku nyingine ya kipekee kwetu tumeweza kustahilishwa mimi na wewe kuweza kuiona bure kabisa bila gharama kwahiyo tunapaswa kumshukuru Mungu na kuitumia vizuri siku hii ya leo. Kumbuka kutumia vizuri muda wako katika mambo chanya na yenye tija kwako.

Image result for never satisfied
BE HAPPY BUT NEVER SATISFIED – BRUCE LEE

Mpendwa msomaji, natumaini leo umeanza na lile zoezi la kufanya ndani ya siku kumi kabla ya mwaka 2016. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile ya jana bonyeza hapa ili uweze kuisoma na kuanza leo hilo zoezi mapema bila kukosa. Kama umeisoma hongera na karibu tuendelee kwenye malengo mahususi ya makala ya leo. Maisha yetu yanahitaji nidhamu kila kona ya kile tunachofanya kila siku. Najua kuna wengine hawana hata nidhamu ya kujisimamia wao wenyewe hata ukiwapa zoezi la kufanya inakuwa ni kazi bure. Maisha ni nidhamu hivyo jitahidi kujisimamia wewe mwenyewe.

Rafiki, napenda kuchukua nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo. Leo tutakwenda kujifunza ugonjwa unao ua watu wengi katika safari ya mafanikio. Je ungependa kujua ni ugonjwa gani? Basi karibu katika makala yetu ya leo nzuri niliyokuandalia ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Hivyo basi, nakusihi sana tusafiri kwa pamoja mpaka mwisho wa makala hii ili uweze kujifunza mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo. Karibu sana rafiki.

Katika safari ya mafanikio kitu kinachowaua watu wengi ni kuridhika. Kuridhika amekuwa ni ugonjwa unao watesa na kuua watu wengi katika safari ya mafanikio. Wapo watu wengi wanaanza na kuifia njiani bila hata kufika kileleni. Kuna wale watu ambao wakifanya kazi na kupata hela ya kutosha siku mbili tatu basi anaacha kufanya kazi kwanza na kuendelea kutumia kile alichonacho kwanza mpaka kiishe.

SOMA; Hizi Ndizo Sababu Zinazokuhamasisha Wewe Kuwa Na Mafanikio

Watu wanaridhika na mafanikio madogo waliyopata na kuona kuwa wamefika badala ya kusonga mbele zaidi. Yule aliye juu zaidi kifedha duniani anakazana kupambana kuwa juu zaidi licha ya kuwa na fedha nyingi za kutosha kuliko mtu mwingine yeyote duniani. Sasa kwanini wewe uridhike na kusema hiki kinanitosha na kuacha kwenda mbele zaidi?

Inawezekana unaridhika na mengi katika maisha yako kwa mfano, mwingine anaweza kuwa kiburi wa kutojifunza na kusema yeye anajua vitu vingi hivyo hana haja ya kujifunza. Kumbe basi mtu huyu ameridhika na maarifa aliyonayo. Kumbe ni busara na hekima kuchukua na kutumia maneno aliyowahi kusema mwanafalsafa Socrates, kuwa hekima ya kweli na ya kipekee ni kujua kuwa hujui kitu. Hivyo basi katika jambo lolote usiridhike na tumia falsafa hii kusonga mbele zaidi ya hapo ulipo sasa.

Hatua ya kuchukua leo, usiridhike na hali uliyonayo katika safari ya mafanikio. Hakuna mipaka ya kukuzuia kwenda mbele zaidi ya hapo ulipo sasa. Chochote unachotaka katika maisha yako kipo kama raba bendi unaweza kuivuta kulingana na saizi unayotaka wewe kwenye maisha yako kwahiyo vuta raba bendi kadiri uwezavyo.

SOMA;  Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yao

Kwa kuhitimisha, kuridhika kwenye jambo lolote ni ugonjwa unaweza kuridhika kwenye eneo lolote la maisha yako na kujiona kuwa uko vizuri kumbe hauko vizuri. Kama ndoa yako iko vizuri basi usiridhike endelea kupambana kuifanya kuwa bora zaidi, kama biashara yako iko vizuri na wateja wako vizuri usiridhike endelea kuboresha zaidi huduma yako, watoto wako wako vizuri kimaadili basi endelea kuwapa malezi bora kila siku wala usiridhike na hali waliyonayo sasa hivi. Yaani usiridhike na chochote katika maisha yako bali songa mbele zaidi kama unataka kufika mbali kwenye kilele cha mafanikio.

Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: