Design a site like this with WordPress.com
Get started

Maeneo Matatu (03) Muhimu Ya Kufanyia Usafi Ndani Ya Siku Kumi Zilizobaki Kabla Ya Mwaka 2016 Kuisha

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri kuboresha maisha yako na kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka hapa duniani.

Mpendwa rafiki kuishi maisha ya ubinafsi ni kuishi maisha ambayo hayana maana hapa duniani. Natumaini wewe ni mwanamafanikio unatambua kuwa ili ufanikiwe unahitaji kuwasaidia wengine kupata kile wanachohitaji na wewe utapata kile unachohitaji. Kama unataka kuwa tajiri wasaidie wengine kuwa matajiri pia.

Aidha, leo ni siku bora yenye tumaini kwetu sote hivyo ni zawadi ya kipekee tumepewa na Mungu yatupasa tuitumie vizuri bila kuipoteza.

Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu nzuri ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Katika makala yetu ya leo nzuri niliyokuandalia tutakwenda kujifunza usafi muhimu unaotakiwa kuufanya ndani ya siku kumi zilizobakia kabla ya mwaka 2016 kuisha.
Rafiki uko tayari kufahamu usafi huo? Basi, karibu tujifunze hapa wote kwa pamoja.

Natumaini unaelewa kuwa tumebakiza siku kumi (10) tu kuweza kumaliza mwaka huu wa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. Sasa kabla hatujamaliza mwaka 2016 yatupasa tufanye usafi wa maeneo matatu muhimu ili kuweza kuukaribisha mwaka 2017 tukiwa wasafi.

Ndugu msomaji, kama tunavyojua hakuna mtu anayependa vitu vibaya lakini kila mtu anapenda vitu visafi. Maeneo tunayoishi kwa ndani na nje yote yanatualika tuweze kuyafanyia usafi ili tuweze kufurahia kukaa sehemu safi.

Mpendwa rafiki, maeneo matatu unayopaswa kuyafanyia usafi ni kama ifuatavyo;
Kwanza usafi wa akili, inawezekana tokea mwaka wako uanze na mpaka unakaribia kuisha hujawahi kusafisha akili yako. Hujasafisha akili yako kwa kuondoa uchafu wa habari hasi na kuingiza habari chanya. Pengine unaweza kujiuliza unawezaje kufanya usafi wa akili? Swali zuri sana rafiki unaweza kusafisha akili yako kwa kusoma vitabu, makala makini siyo za udaku, kuhudhuria semina na kuzungukuwa na watu makini waliofanikiwa.

Je mpaka sasa mwaka unaisha umesoma vitabu vingapi rafiki? Unajivunia nini katika kuulisha ubongo wako ndani ya mwaka huu? Kama huna mafanikio yoyote uliyowekeza katika akili yaani huna maarifa sahihi uliyopata ndani ya mwaka huu uko sehemu mbaya na ya hatari. Huwezi kufika kokote kama huna maarifa sahihi na huna watu sahihi wa kukuonesha njia ya kupita.

Sasa ufanye nini ili uweze kupata maarifa ya kulisha ubongo wako? Karibu katika klabu yetu ya kusoma vitabu inayojulikana kwa jina la Tanzania Voracious Reader s (TVR) uweze kusafisha akili yako kwa kusoma vitabu ndani ya siku hizi kumi ili uanze mwaka 2017 kwa mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka huu. Wasiliana na Mimi kupitia namba hii 0717101505 ili uweze kujiunga. Hujachelewa kufanya usafi karibu tukusafishe akili yako kupitia TVR.

Pili, ni kufanya usafi kimwili, hapa tunaanzia kuanzia kufanya usafi wa mwili pamoja na mazingira yanayotuzunguka. Inawezekana unakula vyakula vya hovyo ambayo haviupi mwili kinga dhidi ya magonjwa. Inawezekana umechoka umechakaa kulingana na vileo unavyotumia. Jinsi ulivyo na unavyoonekana ni matokeo ya chakula unachokula kila siku.
Sasa unatakiwa ufanye usafi wa mwili wako kila idara.

Mpendwa msomaji, vilevile unatakiwa kufanya usafi wa eneo unaloishi chumbani kwako na maeneo unayoishi. Pangilia kila kitu mahali pake na safisha kila sehemu ya nyumba au chumba chako na fungua madirisha kupata hewa safi. Wewe ndio unajijua kama chumba au nyumba yako ni safi au vitu vimekaa shaghalabaghala au la.

Tatu, eneo la tatu ni kufanya usafi wa kiroho, inawezekana maisha ya chumba chako cha kiroho kimejaa vumbi ambayo inakufanya upumue vibaya kwa sababu ya kuvuta hewa chafu.
Inawezekana uhusiano wako na Mungu siyo mzuri sasa huu ndio muda wa kufanya usafi wa kiroho.
Wewe ndio unajijua vizuri maisha ya kiroho upo sehemu gani?
Hakikisha unasoma maandiko mbalimbali yanayohusiana na imani yako.

Hatua ya kuchukua leo, Fanya usafi wa maeneo matatu katika maisha yako nayo ni usafi wa akili, kimwili na kiroho.

Kwahiyo, Maisha ni usafi na siyo uchafu. Usafi ni ishara ya kuonesha kuwa sehemu fulani ni salama na uchafu ni ishara ya wazi kabisa kuonesha sehemu fulani si salama. Somo letu la leo limetualika kuweza kufanya usafi katika maeneo muhimu kwenye maisha yetu hivyo tufanye usafi kwa kufanya duniani kuwa sehemu salama kuishi.

Nakutakia usafi mwema na utekelezaji mzuri kwa haya uliyojifunza leo. Washirikishe na wengine maarifa haya uliyopata leo. Sharti moja ni usibadilishe hatimiliki ya maandiko haya.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: