Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ujumbe Muhimu Sana Kwako Kutoka Kwa Papa Francis

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri rafiki yangu na hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo basi, tunaalikwa sisi sote kuweza kumshukuru Mungu na kutumia muda wetu vizuri katika mambo chanya.
Kumbuka kuwa ukipoteza siku ya leo huwezi kuipata tena mpaka pale unapoaga dunia.

Image result for pope francis

Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja.
Rafiki, katika somo letu la leo napenda kukualika uweze kuachilia fundo lililoumbika ndani ya moyo wako. Leo tutajifunza somo la msamaha kwa sababu miongoni mwa matatizo yanayowasumbua watu basi ni majeraha ya moyo.

Wengi wamejereuliwa mioyo na watu wamegeuka kuwa miiba katika maisha yao. Leo ni siku ya kuachilia fundo au uchungu  ulioumbika ndani ya moyo yaani leo ni siku ya kusamehe na siyo kubeba mizigo moyoni.

Pia, nitakushirikisha ujumbe wa Papa Francis ambao unatualika wote kuweza kusamehana.
Huenda unamaliza mwaka na hauongei na jirani yako lakini leo nakwenda kukutibu kupitia maandiko yangu ya leo.

Nitakushirikisha link za makala zangu nilizoandika mwaka huu kuhusu msamaha. Tafadhali uzisome ili uweze kutibu majeraha yako na pia na ujumbe wa papa Francis ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani.

Rafiki, katika kujifunza mambo hapa duniani tunatakiwa kuweka pembeni tofauti zetu na kutafuta chakula cha ubongo wetu ambacho ni maarifa. Najua una njaa ya maarifa kama unasoma hapa basi karibu tushibishane maarifa haya kupitia mtandao huu.

Usiposamehe unakuwa huna Amani ndani ya moyo wako. Maisha yako yanakuwa yametawaliwa na maumivu huku ukiwabeba moyoni watesi wako. Kwanini sasa unakubali kutawaliwa akili na watu waliokukosea ? Usipo samehe unakuwa unamruhusu adui wako aendelee kutawala hisia zako. Tiba ya haya yote ni kusamehe tu kwani kusamehe ni kuachilia fundo lililoumbika ndani ya moyo kwa hiyari yako mwenyewe.

SOMA MUHIMU; Mambo Mawili (2) Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Msamaha Wa Kweli

Unapokwenda kuumaliza mwaka huu nakusihi sana achilia maumivu yaliyokuwa ndani ya moyo wako ili mwaka mpya uwe huru. Kutokusamehe ni kujiweka mwenyewe gerezani na kujiunga na utumwa wa akili ramsi.

SOMA;  UJUMBE MZITO WA MSAMAHA KUTOKA KWA PAPA FRANCIS

”Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung’uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.

Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.

Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.”

Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu umfikie kila mmoja wetu leo katika familia yake. Leo basi tuutafakari ujumbe huu muhimu.”

Hatua ya kuchukua leo; inuka nenda kasamehe leo. Samehe hata kwa kulia machozi lia kabisa kuachilia uchungu uliombika ndani ya moyo na anza maisha mapya. Inuka nenda kazike jeneza la kutosamehe katika maisha yako. Kabla hujamaliza mwaka nenda karudishe uhusiano uliovunjika na watu wako wa karibu kwa njia ya msamaha.

Mwisho, kumsubiri aliyekukosea aje akuombe msamaha ni hali ya mtazamo hasi ambayo itakufanya uendelee kubaki na uchungu ulioumbika ndani ya moyo. Kumbuka upendo haukasiriki pale unapomfikiria mwenzako mema. Upendo haukasiriki pale unapomsamehe ndugu yako,jirani, mke, mume wako, rafiki, na wengine wanaohusiana na hao.
Upendo haubagui bali upendo huvumilia yote.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Washirikishe na wengine maarifa haya uliyopata ila usifute chochote wala kuongeza chochote. Wala usifute haki miliki ya mwandishi.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: