Huwezi Kumpima Mtu Huyu Hapa

Kwenye maisha huwa tunaamini kwamba, pale unapokuwa na mtu karibu ndiyo unaweza kumjua kwa undani na hata kama unataka kumchunguza ni rahisi. Sina uhakika kama itakufaa lakini, huwezi kumpima mtu ambaye anajua anapimwa.Kama unataka mtu sahihi na mchunguze wakati yeye mwenyewe akiwa hajui kama anachunguzwa. Kwa mfano, kwenye usaili wa kazi, mtu anajua anapimwa hivyo …

Ifahamu Tabia Ya Watu

Asili ya binadamu ni kupenda matokeo na siyo sababu. Hata kama watu unaowataka wakupe matokeo lakini wanakupa sababu, usipowasimamia na kutaka matokeo, baadaye watakuja kukulaumu pia. Hata kama mtu yeye ni mvivu lakini licha ya uvivu wake, bado anapenda kuona matokeo mazuri. Wale ambao wako chini yako na unawasimamia kwenye kitu fulani, linapokuja kwenye suala …

Haya Mambo Mawili Ni Faya Kama Ukiyajua

Mwanamafanikio, Bado watu wanaamini kuwa mafanikio ni bahati. Ni kweli bahati inahusika kwenye maisha yako. Hata wewe kuwa hai ni bahati sana ambayo wengine wameikosa.Kwenye suala la mafanikio, bahati inatengenezwa. Bahati inakuja na maandalizi. Usitegemee bahati itakuja ukiwa umeweka mikono mifukoni. Kwa mfano, kwenye mchezo wa mpira wa miguu, kuna timu ambazo zinakuja kupata ushindi …

Ushindi wa Biashara Yoyote Ile Ni Huu Hapa

Rafiki, Wote tunajua kwamba kwenye kila mchezo huwa kuna timu. Timu ndiyo inaleta ushindi kwenye mchezo wowote. Kama unashabikia timu fulani ya mchezo, ukiona namna timu inavyocheza, unajiambia kabisa kwamba tunapata ushindi au hatupati ushindi. Wakati mwingine wewe kama shabiki, unasema kabisa hapa inabidi tubadilishe mchezaji au wachezaji fulani ili kuweza kupata ushindi. Kwenye biashara, …

Hiyari Yashinda Utumwa

Rafiki, USIPENDE kuwa mtu wa kukumbushwa kufanya kila kitu.Ukitaka kuwashawishi watu kuwa mtu wa kujituma na kufanya bila kuambiwa.Ukiona kitu ni wajibu wako basi jitume bila kusubiri kuambiwa. Kama uko kwenye mahusiano, fanya kile ambacho unapaswa kufanya kwenye mahusiano uliyopo.Ukijituma na kufanya bila kuambiwa, dunia itakuheshimu. Hakuna utumwa mbaya kama wa kuambiwa kila kitu.Ili ufanye …

Msaada Ambao Hauwezi Kukusaidia Wewe

Rafiki, Duniani hakuna jeshi la mtu mmoja. Kwa sababu, tunawategemea watu wengine ili kukamilisha mambo yetu muhimu. Msaada ni muhimu sana kwenye maisha yetu. Lakini, msaada wa nje hauwezi kumsaidia mtu yeyote ambaye ameshajiwekea ukomo ndani yake. Mtu ambaye ameshajiwekea ukomo ndani yake, ni ngumu kumsaidia. Kwenye fikra zetu, huwa tunajifunga na fikra zetu wenyewe. …

Mtu Ambaye Hajawahi Kuzuiwa Na Chochote Kile

Rafiki, Kama hujapata kile unachotaka kwenye maisha yako, maana yake bado hujajitoa vya kutosha kupata kile unachotaka. Mtu anayedhamiria kukitaka kitu, huwa anakipata kweli bila kuzuiwa na chochote kile. Mtu mwenye nia ya kufanya kitu au kutaka kitu fulani kwenye maisha yake, hajawahi kuzuiwa na chochote kile.Kwenye maisha yako, ukitaka kitu ongozwa na tamaa ya …

Vitu Viwili Muhimu Sana Utakavyovipata Kwenye Mauzo

Rafiki yangu nikupendaye,Lengo kubwa la kila mmoja wetu hapa duniani anapokuwa anafanya kitu ni kupata matokeo fulani. Mtu anapokuwa anafanya kazi, anategemea kupata fedha na hata kujega koneksheni mbalimbali na watu wengine.Habari njema ni kwamba, hata kwenye biashara au ajira tunafanya ili tupate fedha hilo ndilo linakuwa lengo letu kuu. Sasa kwenye mauzo, ambapo kila …

Komesha Tabia Ya Watu Hawa

Rafiki, Sina uhakika kama itakufaa lakini, kuna watu watakuja kwako wakiwa wanataka kitu kutoka kwako. Kuna mtu ambaye hamjawahi kuwasiliana kwa miaka mingi, siku moja anakupigia simu, anakuambia nakusalimia tu, halafu kwenye simu hiyo hiyo anakuomba umfanyie kitu, au umsaidie kitu. Hii ni tabia ya watu ambayo unapaswa kuijua, kwamba watu watajaribu kukutumia, watu watakuja …

Rafiki Ambaye Hawezi Kukusaliti

Rafiki yangu nikupendaye, Watu ambao unapaswa kuwaheshimu sana hapa duniani ni wateja wako na bosi wako.Kwa sababu hao ndiyo wanafanya maisha yako yaende kwa kukupa fedha ya kuendesha maisha yako.Bila fedha, hata watu wako wa muhimu utashindwa kuwahudumia na hata kukosa heshima yako. Waswahili wanasema, mkono mtupu haulambwi. Bila fedha utakua ni wa kupuuzwa.Ni bora …

Design a site like this with WordPress.com
Get started