Usiwaruhusu Watoto Wako Wafanye Kitu Hiki

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi huwa wanakuwa na upendo mkubwa na watoto wao pale wanapokuwa wanawapata kitu ambacho ni kizuri. Sina uhakika kama itakufaa lakini watoto wa zama hizi wanakua bila ya malezi bora, wazazi wanaogopa kuwaadhibu watoto kwa kuhofia kuchukiwa na watoto hao. Lakini kitu chema ambacho mzazi anaweza kufanya kwa mtoto …

Lazima Utoke Nje Ya Mazoea

Rafiki, Ili ufanikiwe kwenye maisha yako, lazima ufanye kitu kimoja nacho ni utoke nje ya mazoea. Mazoea huwa yanaleta matokeo yale yale mara zote.Lazima utoke nje ya mazoea ili upate matokeo mazuri.Lazima uende hatua ya ziada ili upate matokeo ambayo hujawahi kuyapata. Huchoki kupata matokeo yale yale kila siku? Kama unachoka basi fanya mabadiliko.Matokeo yale …

Falsafa Ya Utajiri

Kama unataka kufanikiwa kwenye elimu ya msingi ya fedha na kujenga utajiri, ishi kanuni hii. PATA PESA, WEKEZA.Lakini, tukoea tumezaliwa tumeshazoeshwa kwamba ukipata pesa tumia. Falsafa ambayo inawafanya watu wengi kuendelea kuwa masikini. Ni tabia ambayo imeshajijenga kwa watu wengi kwamba ukipata pesa, kinachofuata ni kutumia tu.Falsafa ya utajiri ni PATA PESA WEKEZA. Kwa kila …

Kitu Cha Kwanza Kuangalia Kabla Hujamsaidia Mtu

Rafiki yangu nikupendaye, Waswahili wanasema, ukiona ndugu wanagombana shika jembe ukalime. Maana yake ni kwamba, usijiingize kwenye matatizo ya watu ambayo hata hujui chanzo chake. Unaweza ukajiona wewe ni mwema na uko sahihi kabisa kufanya hivyo lakini kufanya hivyo ni kununua matatizo ya wengine. Yaani ya kwako hujayamaliza halafu unataka kuongeza mengine. Ukiona moshi unatoka …

Kitu Wanachotafuta Watu Wengi Kwenye Maisha

Tumetoka kwenye zama za nenda shule, soma kwa bidii, pata alama nzuri na utapata kazi ya uhakika. Kipindi cha nyuma, AJIRA kwa mtu aliyesoma ilikuwa ni kitu cha uhakika sana. Na watu walivutiwa na hilo kiasi cha watu wengi kupambana na wao wapate elimu nzuri ili wapate uhakika wa kazi. Kwenye jamii, mtu akienda kuajiriwa …

Sijui Hata Nitavaa Nguo Gani Leo?

Asubuhi ndiyo muda ambao unapaswa kuulinda kwa gharama kubwa. Ukipoteza mwanzo wa asubuhi yako maana yake umepoteza siku yako. Muda wa asubuhi siyo muda wa kupanga bali ni wa kufanya yale mambo ambayo ni muhimu tayari ulishapangilia tokea jana. Asubuhi ni muda wa utekelezaji na siyo kuanza kujiuliza nitafanya nini. Lala kabisa ukiwa unajua kesho …

Usipojitambua Unakuwa Mzigo Kwa Wengine

Rafiki, Kujitambua ni zawadi kutoka kwa Mungu. Siyo kila mtu amepata hiyo zawadi. Wako wengi mpaka sasa hawajapata zawadi hiyo na hawajui nini wanachopaswa kufanya kwenye maisha yao. Unapaswa kujitambua, kujua nini unachopaswa kufanya. Wewe kama baba au mama unapaswa kujua wajibu wako wa msingi ni upi na unapaswa kutekeleza majukumu yako ipasavyo bila kuambiwa. …

Kuwa Mtu Wa Kuchunguza

Rafiki yangu nikupendaye, Waswahili wanasema asiyejua maana haambiwi maana.Unapaswa kuwa na njaa ya kujua kile ambacho hukijui kwa sababu watu wanatumia ujinga wako kunufaika. Ukikaa na kuacha kujifunza, utakua mteja mzuri kwenye kila eneo la maisha yako. Badala hata wewe kuuza, utashangaa unaishia kuuziwa kila siku. Ukiwa unajua vitu vingi, utakua bora hata watu ambao …

Unahangaika Na Nini?

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha wewe siyo kiranja wa dunia wa kutaka kuhangaika na kila kitu.Kazi yako moja ni kuhangaika na yale ambayo yako ndani ya uwezo wako. Hangaika na mambo ambayo yanafanya maisha yako yaende. Mambo ambayo yanakupa kipato na siyo kuwa kiranja wa dunia wa kutaka kuhangaika na kila kitu. Kwenye maisha unapaswa …

Wewe Ni Mkombozi Wa Wengine

Kila unapoamka, amka ukiwa na hamasa kubwa sana kwamba wewe ni mkombozi kupitia kile unachofanya, unapaswa uende ukakifanye, ili ukoe watu.Dunia inakusubiria wewe mkombozi kupitia kile unachofanya.Kwa chochote kile unachofanya, jua unafanya siyo tu kwa sababu yako wewe mwenyewe, bali kwa sababu ya wengine. Wewe ni mkombozi, watu wanakutegemea wewe ili maisha yao yaende. Usijichukulie …

Design a site like this with WordPress.com
Get started