Sifa Moja Unayopaswa Kuwa Nayo

Rafiki, Kuna wakati mwingine hupati kile unachotaka kwa sababu tu ya sifa ulizokuwa nazo. Unaweza kuwa na sifa ambazo zikakusaidia kupata kitu fulani au kukosa kitu fulani. Mara zote unapaswa kujijengea sifa zinazo kufanya uaminike bila shaka, kiasi cha kupata dili nzuri. Sifa moja unayopaswa kuwa nayo ni; Uaminifu usiotiliwa shaka kwa mara zote kufanya …

Ikatae Hii Sauti

Rafiki, Ingekuwa ni mtu wa kupanga na kufanya basi suala la mafanikio kwako siyo shida kabisa. Kuna wakati unakosa ushindi kwa sababu tu ya kuahirisha yale uliyopanga kufanya. Na ya kitu kinachokuzuia usikamilishe uliyopanga ni ile sauti unayokuambia kwamba nitafanya baadaye. Wewe ni shahidi, umeshajiambia utafanya baadaye na hata hujakamilisha kufanya kile ulichopanga kufanya hiyo …

Yafanye Maisha Yako Kuwa Rahisi

Rafiki, Kiasili maisha tayari ni magumu, lakini sisi wenyewe ndiyo huwa tunafanya maisha kuwa magumu zaidi. Huwa tunakataa uhalisia wetu, na kuhangaika na mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu kabisa. Pale tunapohangaika na mambo ambayo yako nje ya uwezo, tunajikuta tunajilaumu baadaye kwa sababu ya kushindwa au matokeo tunayopata. Hapa duniani, kuna mambo ya …

Ukiambiwa Maneno Haya Utajisikiaje?

Rafiki yangu nikupendaye, Kama leo utaambiwa una miezi sita tu ya kuishi, baada ya hapo utakufa, je vitu gani utabadili kwenye maisha yako? Je utaendelea kupoteza muda wako kuzurura kwenye mitandao au kufuatilia habari?Je utaendelea kusumbuka na mambo madogo madogo yasiyo na tija kwako? Je utaendelea kuahirisha yale ambayo umekuwa unasema utafanya kesho lakini hufanyi?Ni …

Utapata Nafasi Kulingana Na Hiki

Rafiki, Nafasi nyingi ambazo watu huwa wanapata ni kwa sababu ya nafasi zao. Yaani unapata nafasi kulingana na nafasi yako.Hakuna maneno zaidi. Nafasi yako ikoje? Watu wengi wanaopata nafasi mbalimbali ni kwa sababu wana nafasi hizo.Usitegemee kukutana na bahati kama hujatengeneza mazingira ya kukutana na bahati unayotaka. Tengeneza nafasi, ili upate nafasi kadiri ya nafasi …

Uzuri Wa Kazi Ya Mauzo

Rafiki, Kwenye maisha, kila kitu kinaamuliwa na mauzo.Na mauzo ndiyo kila kitu.Kwenye kila makubaliano unayofanya, maana yake mauzo yamefanyika. Ukitaka upate kile unachotaka au ulipwe kiasi gani, nenda kwenye mauzo. Mauzo ndiyo yanaamua wewe ulipwe kiasi gani. Njia rahisi ya kukuza kipato chako ni kupitia kuuza.Kwenye mauzo huwa hakuna kipato cha ukomo. Kama unataka fedha …

Epuka Kiburi Kwenye Safari Ya Mafanikio

Rafiki, Kuna hali fulani huwa tunakuwa nayo sisi binadamu. Pale tunapoanza kuona tayari unajua na unaweza kila kitu. Unaona hakuna mtu anayeweza kukushauri au kukufundisha chochote.Unakuwa na hali ya ujuaji mwingi na kupelekea kuwa na kiburi. Unaona wewe ndiyo unayeweza kila kitu na hakuna mwingine kama wewe. Ukiwa kwenye kilele cha mafanikio ni rahisi kuingiwa …

Kinachoua Mafanikio Yako

Rafiki, Kabla hujafanikiwa ulikuwa umejiwekea viwango vya juu na kuhakikisha unavifikia mara zote. Lakini baada ya kufanikiwa unaachana na viwango hivyo na kuruhusu mazoea. Mazoea yanaua mafanikio makubwa. Angalia watu ambao kabla ya kuingia kwenye mahusiano walikuwa makini kuhakikisha kila mmoja anajali maslahi yake. Watu wakishakuwa kwenye kilele cha mafanikio kwa muda, wanaanza kufanya mambo …

Hivi Ndivyo Unavyopaswa Kuwa

Rafiki, Maisha ni yako. Ishi vile utakavyo ili mradi usivunje sheria za asili, nchi na kanuni za maadili. Kundi linapokulazimisha uwe kama wao, kataa na baki kuwa wewe halisi, kuwa mkweli kwako. Siyo kosa lako kujikuta katika kundi fulani kwa sababu sisi binadamu ni viumbe vya kijamii, tunapenda kuwa ndani ya kundi.Lakini,kama umejitambua na kuona …

Design a site like this with WordPress.com
Get started