Njia Rahisi Ya Kupuuzwa

Asili ya binadamu ni kupenda vitu vizuri.Watu wanapenda kuambatana na watu ambao ni bora hata kama wao siyo bora. Kila mtu anapenda kitu kizuri. Kila mtu anapenda kufanya kazi na watu bora. Hakuna anayependa vitu ambavyo siyo bora. Kama unataka watu wakupuuze, kuwa mtu ambaye unazalisha vitu ambavyo havina ubora. Kama unataka uwe bora ha …

Kama Hujawahi Kupitia Hali Hii Usikosoe

Yeyote ambaye unamuona leo yuko bora, hapo mwanzoni alikuwa hana anachojua. Kwa hiyo, kwa nafasi uliyonayo sasa, usiitumie kuwakosoa walio chini yako.Bali wape moyo, kumbuka hata wewe ulikuwa kama wao hapo awali. Kama hujawahi kujaribu kitu, usikosoea wale waliofanya.Kama unaona wewe huwezi kukaa bila kukosoa, basi fanya na wewe kitu chako na kisha kikosoe. Huwezi …

Bado Hujakielewa Vizuri

Lengo la mawasiliano yoyote ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Kama mawasiliano unayofanya hayaeleweki, huwezi kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Mwalimu mzuri, ni yule anayeeleweka. Ni yule ambaye anatumia lugha rahisi kufikisha ujumbe. Njia rahisi ya kuwa mtu anayeeleweka ni uwezo kuelezea kitu kwa urahisi. Kama huwezi kueleza kwa urahisi bado hujakielewa vizuri.Njia rahisi ya kujipima kama umekielewa kitu …

Uwekezaji Uliosaulika

Dunia inaenda kwa kasi sana. Watu wanahangaika na mengi kiasi wanashindwa kufanya vitu kwa ubora. Kabla hujaenda kasi, jiulize kwanza je uko njia sahihi? Usiongeze mwendo kabla hujajua kule unakokwenda. Ongeza kasi, huku ukijua uko sehemu sahihi. Uwekezaji uliosaulika zama hizi ni uwekezaji wa kusoma vitabu na malezi ya watoto. Watu wengi wanakosa maarifa sahihi …

Jinsi Ya Kuwa Na Siku Bora

Kwenye maisha yetu ya kila siku, hakuna kitu tunachopenda na kufurahia kama ushindi. Ushindi ni ushindi tu. Uwe mkubwa au mdogo unampa mtu hamasa ya kuendelea kufanya kile anachofanya. Ili uwe na siku bora na yenye ushindi, jitahidi kuwa mkamilishaji bora wa kile ulichopanga kufanya. Watu wanapenda ushindi, kila jukumu ambalo umepanga kamilisha mapema na …

Kama Unataka Dunia Ikupishe Fanya Hivi

Kuna vichekesho nimekutana navyo mtandaoni, huenda hata wewe umeviona.Kulingana na mambo ya dunia yanavyoendelea, vichekesho hivyo vinasema, dunia simama nishuke. Wakiwa na maana kwamba, kwa mambo yanayoendelea duniani, ni watenganayo ili waiache. Dunia ina mambo mengi, tokea enzi na enzi, huwezi kuidhibiti dunia. Bali unaweza kujidhibiti wewe mwenyewe. Kuwa mtu sahihi katika dunia yenye watu …

Njia Rahisi Ya Kushinda Mabishano

Mwanamafanikio, Kiasili sisi binadamu ni wabinafsi. Tunapenda kuona mambo yetu ndiyo ya muhimu kuliko ya wengine. Sasa katika suala kubishana, ni kila mmoja anapenda kushikilia msimamo wake.Hakuna anayependa kuonekana mjinga kwenye kile anachokiamini. Mabishano mengi ambayo tunayokutana nayo, mengi hayana mashiko.Hakuna mtu anayeweza kukubali ashindwe kwenye kile anachokiamini.Kila mtu anapenda kuona ni BORA. Njia rahisi …

Muda Mzuri Wa Kufanya

Rafiki, Supu ni tamu pale inapokuwa ya moto.Supu ikipoa, inakuwa haina tena ile ladha ya supu. Na vile vile katika maisha yako, muda mzuri wa kufanya kitu ni pale unapokuwa na hamasa ya kufanya kitu hicho. Pale unapokuwa na wazo, hapo hapo lifanyie kazi kabla halijapoa. Ukimfikiria mtu na ukamkumbuka, usiseme baadaye, chukua hatua na …

Usifanye Kitu Kwa Makubaliano Haya

Jambo lolote unalofanya , hakikisha kila upande unapata ushindi. Makubaliano hatari zaidi ni yale ya wewe kujali maslahi yako kwanza bila kujali maslahi ya upande wa pili. Kitu chochote ambacho unafanya na mtu mwingine, hakikisha mmeelewana vizuri, kuweni na utaratibu ambao upo wazi na kila mtu ajue majukumu yake na matarajio ya mwenzake. Usifanye kitu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started