Njia rahisi ya kujiona kama vile huna maana hapa duniani ni kujifananisha wengine. Tunapoteza ubora wetu, pale tu tunapoanza kujilinganisha na wengine.Kila mtu ana upekee wake, hivyo kutaka mtu afanane na mwingine maana yake ni kutaka apoteze upekee wake na kuishi upekee wa mwingine. Jikubali vile ulivyo. Watu watakupenda na kukukubali vile ulivyo kwa sababu …
Majaribu Yanapimwa Na Hiki
Rafiki, Hakuna mtu ambaye yuko salama. Kila mtu anapimwa kulingana na kiwango cha imani yake. Majaribu mengi huwa yanapimwa kulingana na kiwango cha imani yetu.Majaribu yanakuja kupima kiwango cha imani yetu. Ubora wa mtu unaonekana wakati wa changamoto. Namna anavyozitatua kwa utulivu. Tuzipokee changamoto kadiri zinavyokuja na kuzitatua. Kwa sababu maisha yetu hapa duniani yapo …
Fanya Kazi Na Wateja Hawa
Rafiki, Siyo kila mteja ni mteja kwako.Kuna wateja wengine wanaweza kuja kwako lakini siyo sahihi. Na siku zote kwenye biashara na hata maisha kwa ujumla.Fanya kazi na kitu kinachofanya kazi tayari. Wateja wazuri ni wale ambao wana uwezo wa kumudu gharama ya kile unachouza.Usihangaike na wateja ambao hawana hela, ambao hawana uwezo wa kumudu gharama …
Kazana Kuwa Wewe
Huwezi kuona ladha ya maisha yako, kama kila siku unakazana kujikimbia. Ni ajabu mtu kuwasikiliza watu wengine lakini anashindwa hata kujisikiliza yeye mwenyewe. Ndani yako kuna maisha ambayo unayataka kuishi lakini unashindwa kuishi kwa nini? Kuna mambo ambayo unayafanya, unajua kabisa hayakupendezi, ila unafanya tu ili kuwafurahisha watu wengine. Mpaka unaondoka hapa duniani, hautakuja kufanikiwa …
Jifunze Kwa Mpenzi Mtazamaji wa TV
Kwenye haya maisha hakuna kitu kizuri kama kuishi kwa amani. Tunaweza kuwa na kila kitu, lakini maisha yetu yakawa hayana maana kama tu tumekosa Amani ya ndani ya maisha yetu. Amani hii hailetwi na vile tulivyokuwa navyo bali Amani hii inakuja kwako pale unapojua maana ya mafanikio kwenye maisha yako.Watu wanaopata shida ni wale ambao …
Kama Unataka Kuuza Fanya Hiki
Kila biashara inataka ukuaji. Moja ya sifa ya viumbe hai ni kukua. Hivyo biashara nayo ina sifa ya ukuaji. Na kama kitu hakikui, maana yake hakuna uhai.Kama biashara haiendi mbele, maana yake inarudi nyuma.Hakuna kusimama. Kwenye biashara, zoezi la kuongeza wateja wapya linapaswa kufanyika mara zote. Sababu ya biashara nyingi KUTOKUUZA ni kwa sababu ya …
Usikubali Mteja Huyu Akukwamishe
Kwenye maisha ili ukue lazima ukuaji wako utawakera baadhi ya watu.Wale ambao wanapenda mambo ya kawaida, watependa kukuona ukiwa pale pale kila siku. Kuna watu huwa hawapendi kitu kinachoitwa mbadala kwenye maisha yao.Wanapenda kuwa katika hali fulani ya kuridhika(comfort zone).Mtu ambaye yuko katika hatua hii, hapendi tena ukuaji anataka kubaki na kile ambacho ameshazoea kukipata. …
Vitu Ambavyo Tunapenda
Rafiki, Vitu ambavyo watu huwa wanavipenda na vinawapa manufaa mazuri kwao, huwa hawakosi muda wa kuvifanyia kazi. Mtu ambaye haoni umuhimu au thamani ya kitu, hawezi kupata muda wa kitu hicho.Kama kitu kinakupa matokeo, maana yake ni kizuri na utaendelea kukifanya. Mara nyingine licha ya kujua vitu muhimu vya kufanya, bado watu wanafanya vitu ambavyo …
Hoji Kila Kitu Kupata Ukweli
Usiwe mtu wa kukubaliana na kila jambo kirahisi bila kuhoji. Uwe mtu wa kufanya udadisi, peleleza mpaka ujue ukweli na kisha fanya maamuzi. Ukishakuwa na taarifa sahihi, zitakusaidia kupata majibu sahihi na kufanya maamuzi. Vitu vingi ambavyo watu wamezoea kufanya siyo sahihi. Ni rahisi kukubali kufanya kitu kwa sababu kila mtu anafanya, na kuona kwa …
Hisia Na Fikra
Kwenye maisha kila kitu kina mtegemea mwenzake.Kiasili, tumeumbwa kwa ushirikiano.Kwa mfano, mwili unafanya kazi kwa ushirikiano. Mfano, mikono, miguu na nk. Vile vile kama binadamu, unahitaji kuwa na hisia na fikra. Huwa tunafanya maamuzi kwa hisia, halafu tunakuja kuhalalisha kwa fikra. Hisia na fikra ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja.Mtu asipokuwa na hisia ni shida, na …