Ukifanya Kazi

Rafiki yangu nikupendaye , Ukifanya kazi, kazi yako itakusaidia kufanya kazi. Kazi nzuri huwa inajitangaza yenyewe bila kukutegemea wewe. Unapofanya kazi nzuri, inakuwa ni njia nzuri ya kujiuza kwa wengine. Acha kazi yako iwe msemaji wako. Kama unafanya kazi nzuri, utapunguza kujielezea na badala yake kazi yako itakuwa msemaji wako. Kazi yoyote ile inayopita mikononi …

Jaribu Kwanza

Rafiki yangu nikupendaye, Huwa tunatengeneza vikwazo mbalimbali kwenye maisha yetu, huku sisi wewe wenyewe tukiwa ndiyo vikwazo vyenyewe. Mara nyingi huwa tunahalalisha kitu kwa mdomo na siyo kwa vitendo.Tukiambiwa kitu, tunaishia KUHUKUMU tu kwamba hiki hakifanyi kazi au hakuna kitu. Njia nzuri ya kujua kama kitu kinafanya kazi au hakifanyi kazi ni kukifanyia kazi kitu …

Unapotafuta Furaha Zingatia Hili

Watu huwa wanaweka juhudi ili kutafuta furaha na hata wengine raha.Yote hii ni kutaka kujisikia vizuri.Kupata ile hali fulani ridhiko kutoka ndani. Katika kutafuta huko raha au furaha huwa tunazalisha homoni inayoitwa dopamine. Hii huwa inazalisha kilele cha raha fulani unayoitafuta. Rafiki, ni vizuri kutafuta furaha au raha lakini furaha au raha yako unayoitafuta, isiwaumize …

Asiwepo Mtu Akuzidi Hapa

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye haya maisha, asiwepo mtu ambaye anachukua hatua kuliko wewe. Mtu anayechukua hatua mara zote huwa anakuwa mshindi. Kama kuna mtu anachukua hatua kubwa kuliko unazochukua wewe, mtu huyo yupo mbele yako mbali sana, kwa sababu kwa hatua kubwa anazochukua, anajiweka kwenye nafasi ya kufanikiwa kuliko wewe. Hakikisha wewe unakuwa ndiye mtu …

Ukishakuwa Na Fedha Utakutana Na Hiki Hapa

Rafiki yangu nikupendaye, Huu ni msimu wa sikukuu. Na watu wengi tunaongozwa na hisia ya kufanya manunuzi kwa kipindi hiki. Fedha ikiwepo, huwa haikosi matumizi. Kila mmoja anaingia kwenye mtego wa manunuzi. Huwa tunanunua vitu na baadaye tunakuja kujilaumu. Kitu kikubwa unachotakiwa kuzingatia kwa kipindi hiki ni umakini tu. Unajua kwa nini? Kwa sababu, ukishakuwa …

Acha Watu Wakuzidi Maeneo Yote Lakini Siyo Kwenye Hili

Rafiki yangu nikupendaye, Asiwepo mtu yeyote ambaye anafanya kazi kukuzidi wewe. Hakikisha unafanya kazi kuliko wengine wote, weka juhudi kubwa kwenye kazi zako, iwe ni kwenye ajira, kujiajiri au biashara. Hakikisha watu wanapotaka kitu fulani kikamilike basi wanakuja kwako. Na hili linawezekana kama utaweka muda na umakini kwenye kila unachofanya, na kama utaacha kutafuta njia …

Ijue Kanuni Ya Mafanikio Makubwa

Rafiki yangu nikupendaye, Kanuni ya mafanikio makubwa inasema hivi, ushawishi wako ni matokeo ya jinsi gani unaweka mbele maslahi ya wengine kabla ya maslahi yako. Hii ni kanuni inayohusu mtandao wako, wale watu wanaojua kuhusu wewe, wanaokuamini na ambao wanapenda kukuona wewe unafanikiwa. Hawa ni watu ambao watakutetea kwa lolote na kwa yeyote. Kadiri unavyokuwa …

Ung’ang’anizi Unaleta Bahati

Rafiki, Unaweza kusema watu wana bahati na wewe labda una kisirani, lakini bahati au kuwa na kisirani ni chaguo lako mwenyewe. Ukikaa kwenye, bahati inakuja yenyewe. Hata kama mchakato haujakulipa leo, utakuja kukulipa kesho. Ung'ang'anizi wa kukomaa kwenye mchakato, huwa unaleta bahati. Bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi.Endelea kukaa kwenye mchakato, utashangaa siku isiyokuwa …

Shirikiana Na Watu Muhimu Kufikia Ndoto Zako./20/12/2024

Rafiki, Watu ambao hawajafanikiwa huwa wanafikiri wanapaswa kufanya kila kitu wao wenyewe ili wafanikiwe. Hivyo wanapokuwa wamekwama kwa kukosa ujuzi au uzoefu fulani huona ndiyo mwisho wa safari yao ya mafanikio. Usikubali ukosefu wa ujuzi au rasilimali kukuzuia wewe kufikia ndoto zako. Kama kuna kitu hujui, au kuna kitu huna tafuta mtu kwenye kujua au …

Design a site like this with WordPress.com
Get started